Thursday, September 3, 2015

TANZANIA NA VIETNAM WASHEREHEKEA MIAKA 50 YA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015.
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo.
Afisa Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) 
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo. 
Waziri Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini. 
Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. 
Balozi wa Vietnam, Mhe. Nam (kulia) akimpokea Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kushoto) alipowasili kwenye maadhimisho hayo anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Yahya Simba
Mhe. Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga.
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akisalimiana na raia wa Vietnam waishio nchini waliojitokeza kumpokea alipowasili kwenye maadhimisho hayo.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za mataifa yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia) kwa pamoja na Mke wa Balozi wa Vietnam nchini na Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na Vietnam zikiimbwa. 
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba  nyimbo za Taifa
Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo
Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo.
Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo. 
Picha na Reginald Philip

No comments: