Balozi
Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine
wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi
Koeler. |
Balozi
Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake
Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata
katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kusifu ukarimu wa
Watanzania. |
Balozi
Kasyanju kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa
nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro
Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia. |
Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler. |
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni
waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye
amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. |
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (katikati)
akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke (kushoto)
pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa hafla ya
kumuaga Balozi wa Ubelgiji. |
Balozi
wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa na Bw.
Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa
Ubelgiji. |
Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo. |
Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
|
|
Balozi Koeler akiteta jambo na Balozi Sokoine. |
Balozi Kasyanju, Balozi Koeler na wageni waalikwa wakitakiana afya njema. |
Balozi
Koeler akifurahia zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju huku
akitamka kuwa "nitarudi Tanzania kuja kupanda Mlima Kilimanjaro". |
Balozi Koeler akimshukuru Balozi Kasyanju kwa zawadi hiyo nzuri.
|
No comments:
Post a Comment