Monday, July 20, 2015

MCHAKATO WA UBORESHAJI WA BOMA LA MKUU WA WILAYA YA IRINGA KUWA KITUO CHA MAKUMBUSHO NA MAONESHO YA SANAA ZA KIUTAMADUNI UMEPONGEZWA KWA KUWA ITASAIDIA KUKUZA SEKTA YA UTALII IRINGA

Meneja wa Mradi wa Kuendeleza Utamaduni Nyanda za Juu Kusini Jan Kuever akitoa taarifa ya Uboreshaji wa Boma la Mkoloni Iringa Kuwa sehemu ya makumbusho na Maonesho ya Kiutamaduni.
Boma lililokuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa linaloboreshwa likwa katika hatua nzuri ya ujenzi.
Makamu Mkuu wa Chuo Cha Iringa akieleza ushirikiwa wa Chuo katika kudumisha Utamaduni.
Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari yetu Bw Jimson Sanga akitolea ufafanuzi juu ya mwenendo wa Mradi.

Bw John Kimaro Mkurugenzi Msaidizi wa mambo ya Kale
Bw Bashir Kiteve mwakirishi wa Mkuu wa Mkoa katika Hafla hiyo.
Jengo la Makumbusho


Wadau mbalimbali wa sekta ya utamaduni Nyanda za Juu kusini hususani mkoa wa Iringa wameelezea kufurahishwa kwao juu ya zoezi linaloendelea la kulihuwisha boma lililokuwa likitumiwa kama ofisi ya mkuu wa wilaya ya ilringa na kubadilishwa matumizi kutokana na umri wake.


Wadau hao waliokutana mwishoni mwa wiki kufanya ukaguzi na kutathimini shughuli hiyo ya uhuwishaji wa boma hilo wakiwemo vingozi wa serikali  mkoani wa Iringa wakizunguzia mwenendo mzima wa Jengo hilo walionesha kufurahishwa na hatua iliyofikiwa Katika ujenzi huo.

Boma hilo ni miongoni mwa majengo makubwa na yaliyojengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita ambapo kwasasa mradi wa Fahari yetu kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Iringa(TUMAINI) Pamoja na serikali ya mkoa wa Iringa kwa ufadhiri wa EU  wameona ni vema jingo hilo likatumiwa kwa shughuli nyingine za kiutamaduni.

Akielezea hatua za ujenzi huo Meneja wa Mradi wa kutunza Utamaduni Nyanda za juu kusini Bw Jan Kuever alisema kuwa mradi wa Fahari yetu ni mradi pekee unaolenga kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini pamoja na vitu mbalimbali vya kiutamaduni ambavyo awali hapakuwepo mahali ambapo vinaweza kutunzwa jambo ambalo liliwafanya waone umuhimu wa kuomba kulifanyika ukarabati Boma la Iringa na kuligeuza kuwa sehemu ya makumbusho na kutunza mambo ya kiutamaduni.

“mradi huu kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Iringa tuliona ni vizuri kuwasiliana na ofisi ya mkoa wa Iringa ili tuweze kulikarabati boma lililojengwa na Mkoloni kuwa jingo la kuhifadhi aseti za kiutamaduni ambapo watu wa Iringa na wageni watakuja kuona kumbukumbu ya mambo ya kale Katika jingo hili zikiwemo picha za zamani” alisema Kuever.

Naye Makamu mkuu wa Chuo mkuu wa Chuo Cha Iringa akizungumzia suala la kuendeleza utamaduni Nyanda za juu kusini alisema kuwa jambo hili lilipaswa kuwa mikono ni mwa wazawa wa maeneo haya jambo ambalo limekuwa kinyume ambapo watu wa nje ndiyo waliyoiona fursa hiyo na kuanza kutukumbusha wazawa juu kuulinda na kuutunza utamaduni kitu ambacho ni faida ya wananchi wenyewe.

“uwepo wa mradi huu wa Fahari yetu ni kwa manufaa ya wananchi wenyewe kwasababu waanzilishi wa mradi huu wanaweza kuondoka ila mradi na jingo hili litabaki wa faida yetu wenyewe”alisema mkuu wa chuo hicho.

Pia Katika Hafla hiyo alikuwepo Mkurugenzi wa masuala ya kale kutoka wizara ya maliasili Bw John Kimaro ambaye pia aliridhishwa na kuwapongeza viongozi wa Mradi huo kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini ambapo alisema uwepo wa Jengo hilo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza sekta ya utalii kwasababu watali wengi watatamani kuja kuona mambo ya kale na namna yalivyofanya kazi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Bw Bashir Kiteve alisema imefika wakati kwa wananchi kushiriki kikamilifu Katika kupigania utamaduni wao ambao kimsingi ulikuwa unapotea hivyo wananchi wanatakiwa kuunga mkono juhudi za wadau za kuendeleza na kulinda utamaduni.
“nitoe rai kwa wananchi sasa wenzetu hawa wamejitolea kutukumbusha utamaduni wetu hebu tuwaunge mkono maana sasa fulsa za kiuchumi zinazotokana na utamaduni zitaongezeka kutokana na uwepo wa jingo la kiutamadu kwa kuwa watu mbalimbali watafanya biashara na kujipatia kipato” alisema Kiteve

No comments: