Sunday, May 10, 2015

RAIS KIKWETE AWASILI ALGIERS, ALGERIA, KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal wakipokea salamu wakati alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal wakikagua Gwaride wakati alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria.

Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal wakati alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria.
Bendera za Tanzania na Algera zikiwa zimepamba jiji la Algiers, Algeria, ambako Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiongea na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, Jumamosi,Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika. PICHA NA IKULU
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, mchana wa leo, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.

Rais Kikwete amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria akitokea New York, Marekani, ambako kwa wiki nzima amekuwa anaendesha vikao vya Jopo la Watu Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inaweza kujiandaa vizuri zaidi kukabiliana na majanga ya afya, na hasa magonjwa ya milipuko, katika siku zijazo kufuatia balaa la ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene mjini Algiers, Rais Kikwete amepokelewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal kabla ya kuelekea kwenye Kasri ya Kirais ya Zeralda ambako amefikia.

Baadaye jana jioni, Rais Kikwete ameweka shada la maua kwenye Mnara wa Taifa kwa heshima ya wanamapinduzi waliopoteza maisha yao katika vita vya ukombozi wa kuwania uhuru wa Algeria kutoka kwa Wafaransa.

Algeria ilipata uhuru kutoka kwa Wafaransa mwaka 1962 baada ya vita kali ya ukombozi ya miaka minane, ambako pia wananchi wanaokadiriwa milioni mbili walipoteza maisha yao.

Baadaye, Rais Kikwete pia amembelea Jumba la Makumbusho la Mashujaa wa Vita ya Ukombozi mjini Algiers.

Kesho, Jumapili, Mei 10, 2015, Rais Kikwete atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa kwa heshima yake na Waziri Mkuu ambaye atafanya naye mkutano rasmi kabla ya dhifa.

Baadaye, Rais atakwenda kwa mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye mwaka jana alichaguliwa tena kwa mara ya nne kuongoza Algeria tokea alipochaguliwa kuwa Rais  kwa mara ya kwanza mwaka 1999 baada ya kutumikia kama Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi yake kwa miaka mingi. Tokea 1999, alichaguliwa tena 2004, mwaka 2009 na mwaka jana.

            Tanzania na Algeria zimekuwa marafiki wa karibu kwa miaka mingi tokea uhusiano ulipoanzishwa na waanzilishi wa mataifa hayo mawili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Ben Bella. Kwa hakika, Algeria ilikuwa moja ya nchi chache duniani zilizoisaidia sana Tanzania wakati wa Vita ya Kagera dhidi ya Idi Amin.

Tanzania pia imekuwa inapata misaada mikubwa kutoka Algeria katika sekta za gesi a elimu na katika kitendo kilichothibitisha ukaribu kati ya Tanzania na Algeria, mwaka 2010, Algeria iliifutia Tanzania kiasi cha dola za Marekani milioni 144. Kiasi hicho kilikuwa ni pamoja na deni la awali la dola milioni 58.03, deni ambalo liliongezeka kwa sababu ya mikopo ya mafuta ambayo Tanzania ilikuwa inapata kutoka Algeria na riba.

No comments: