Monday, April 27, 2015

WASICHANA WERUWERU WAASWA

Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi chetu cha uhitimu mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo. Wengine ni Wajumbe wa Bodi ya Shule.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosalia Tarimo (wa pili kutoka kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Akifuatilia ni Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa kwanza kushoto) ambaye pia alikuwa ni Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo.
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa tatu kutoka kushoto – mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru na wageni wengine waalikwa wakati wa mapokezi yake kama Mgeni Rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo.
Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa tatu kutoka kushoto) akitoa hotuba wakati wa mahafali ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakati wa yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo. Pamoja naye ni Mzazi Mwakilishi Cartitas Lengeju (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Paul Uria (wa pili kutoka kushoto), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru, Rosalia Tarimo (wa nne kutoka kushoto) na wa tano kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo.

Wasichana wanaosoma katika shule ya sekondari ya Weruweru iliyopo mkoani Kilimanjaro wametakiwa kufuata nyayo,kujifunza na kupata ushauri kutoka kwa wanawake wenye mafanikio katika jamii ambao utawaongoza kwa maisha yao ya baadaye baada ya kuhitimu masomo ya sekondari.

Ushauri huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Georgia Mutagahywa katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa mahafali wa kidato cha sita ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyohudhuriwa na wazazi,walimu na wageni kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliosoma shule hiyo miaka ya nyuma.

Katika mwendelezo wake wa jitihada za kuwawezesha watoto wa kike kwenye mahafali hayo, taasisi ya Vodacom Foundation imetoa msaada wa mashine ya kudurufu (Photocopy) kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania itakayorahishisha kudurufu kazi za wanafunzi na walimu na kufanya mawasiliano na nukshi.

Vodacom imeona kuwa mashine hii ni moja ya hitaji kubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa itawapunguzia adha ya kupoteza muda mwingi kwenda kufuata huduma hizo kwa umbali mrefu ambapo muda huo wangeutumia kwa masomo yao na shughuli nyingine za kitaaluma na kwa mwaka huu imepatiwa heshima na uongozi wa shule hiyo kutoa mgeni rasmi katika mahafali hayo ya kidato cha sita.

Mkuu wa shule ya Weruweru Bi.Rosalia Tarimo ameishukuru taasisi ya Vodacom Foundation kwa msaada huo . “Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa taasisi ya Vodacom Foundation kwa msaada huu wa mashine ya kisasa,huu ni uthibitisho kuwa Vodacom Foundation ni kinara katika mapambano ya kuwawezesha na kuwakomboa watoto wa kike na tunaomba taasisi nyingine zishiriki katika kampeni ya kuwawezesha watoto wa kike”Alisema.

Safari ya kuwakomboa watoto wa kike ili waweze kutimiza ndoto zao bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini jitihada za kuwakomboa zikifanyika kwa nguvu zote mafanikio yatapatikana hususani kuwafanya watoto wa kike wapate elimu bora waweze kujiamini na moja ya njia ya kufikia mafanikio ni kufuata nyayo,kujifunza na kupata ushauri kutoka kwa wanawake waliofanikiwa kwenye jamii mbalimbali.

Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhi msaada huo,Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bi.Georgia Mutagahywa alisema Vodacom itaendelea kusaidia shule hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali mojawapo ikiwa kupitia wanafunzi waliosoma shuleni hapo. Shule hiyo pia inakabiliwa na matatizo ya kutokuwa na mtandao wa internet ambapo Vodacom imeahidi kulivalia njuga tatizo hilo kuhakikisha linamalizika.

“Tumetoa msaada huu kwa shule ya Weruweru na tumekuwa tukitoa misaada ya aina hii kwa taasisi mbalimbali kwa kuwa tunaamini kuwa kumkomboa mwanamke ni kukomboa jamii nzima na tunaamini kuwa wanawake wakiwezeshwa na kupata elimu bora wanaweze kuleta mabadiliko makubwa kwenye jamii yoyote ile”.Alisema.

Taasisi ya Vodacom Foundation iko chini ya Kampuni ya Vodacom na imekuwa ikijishughulisha na kusaidia jamii kukabiliana na changamoto mbalimbali hususani katika Nyanja za elimu,Afya,kiuchumi.Mwaka 2014 taasisi ya Vodacom Foundation na taasisi ya T-MARC ilizindua kampeni inayojulikana kama ‘Msichana Kwanza’ kwa lengo la kuwawezesha wasichana waweze kujiamini na kuwa katika mazingira bora ya kupata elimu.

Kampeni hii imeanzia mkoani Mtwara na imeonekana kuleta mafanikio makubwa kwa kuwa imeweza kuongeza mahudhurio ya watoto wa kike mashuleni tofauti na hapo awali.Chini ya kampeni hii wasichana hupatiwa pedi za kuwaweka salama wanapokuwa katika vipindi vya hedhi ambapo hapo awali wasichana wengi walishindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo kutokana na kutokuwepo na miundombinu mizuri na mazingira rafiki mashuleni vilevile huweza kupatiwa elimu ya afya na uzazi ili kuwasaidia kuepuka kupata mimba za utotoni.

No comments: