Saturday, April 18, 2015

vijana wapewa mbinu za kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira

Na Mwandishi wetu
Serikali ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasiadia vijana wa kitanzania kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira na pia kuwapa maarifa ya kujiajiri wenyewe .
Vikwazo vinavyowakabili vinaja katika soko la ajira ni kutokuwa na maarifa ya kupata kazi  maarifa a na tabia ambazo zitamwezesha mfanyakazi  kuwa karibu na wafanyakazi wenzake , kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo , kuweka heshima na mwisho kuwa mwakilishi wa taasisi. 
Kwa kutambua changamoto zinazowakabili vijana serikali ya Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka taasisi ya  Resstless Development organization(ICS) kwa ajili ya kuwafundisha namna ya kupata ajira endelevu .
Wakizungumza katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) walimu hao wa kujitolea wamesema wanawafundisha vijana namna ya kuandika maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu , ujuzi na kujiajiri wenyewe .
 Kiongozi wa walimu wa kujitolea (ICS ) Gemma Bunn ameliambia gazeti hili kwamba  sababu ya wao kuwepo nchini ni kwa kutambua kuwa Tanzania asilimia hamsini ya vijana hawawezi kupata ajira na wengi wanakwamishwa kutokana na vigezo hivyo .
‘’Tunatoa mafunzo kuhusu maarifa ya kupata ajira ikiwemo namna ya kuandika maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu , ujuzi , kujiajiri mwenyewe na namna ya kujiweka wakati wa kufanya usaili , kujiajiri mwenyewe pamoja na namna ya kuanzisha biashara pamoja na kutengeneza bajeti ‘’alisema Gemma .
Naye Wendy Morrissey , mwalimu wa kujitolea kutoka taasisi hiyo  amesema CV ni nyaraka muhimu kwa wanafunzi na mtu yoyote kuiandika . Ni nyaraka itakayokusaidia kupata ajira .
Amesema mambo ya kuyazingatia kuyaweka katika nyaraka hiyo ni pamoja ni pamoja na ujuzi na maarifa kwa nafasi ya kazi unayoombea .
CV haitakiwi iwe ndefu zaidi ya ukurasa mmoja kwasababu mwajiri anachukua muda wa sekunde nane kuiangalia . Kwa hiyo unatakiwa kumvutia mwajiri kwa kutumia muda mfupi kuisoma
Wakati ukiandika nyaraka hiyo unatakiwa uandike kwa weledi na usiandike kwa kutumia maneno ya mtaani .
Mambo mengine ambayo hayatakiwi kuandikwa ni sarufi ambazo sio sahihi kwenye maelezo hayo .  Pitia kwanza maeezo yote pamoja na sarufi kabla ya kuikabidhi .
Jambo lingine ambalo ni muhimu ni kuandika maelezo kwa matakwa yako ambayo hayaendani na kazi unayoomba .
 Jonathan Aqulina , mwalimu wa kujitolea anayefundisha namna ya kujiajiri mwenywe alisema njia rahisi ya kukabiliana na changamoto ya mikopo ni  kujiunga katika vikundi .
‘’ Inaweza kuwa ni kikundi cha marafiki au familia . Kikundi kinapokuwa kikubwa hatari inakuwa ndogo . Hiyo ndio njia rahisi ya kupata mikopo ‘’ alisema Aqulina.
Amesema njia rahisi ya kujiajiri mwenywe ni kulifahamu soko lako . Lazima umjue unaye muuzia bidhaa zako . Lazima ufahamu wanahitaji nini .  Kama hautahamu hutaweza kuuza chechote .  Unatakiwa kufanya utafiti wa soko na kufahamu washindani ni akina nani na bei wanazouza bidhaa .
Jambo lingine ni kutangaza bidhaa zako ili watu wafahamu bidhaa unazouza .  Na pia  ushauri wangu ni kwamba hakikisha kwamba gharama zako ziko chini kuliko faida unayopata . Kama gharama zitakuwa juu zaidi ya faida hutaweza kutengeneza pesa biashara yako itakufa .
Na pia siku zote tathmini biashara yako . Tathimini uimara na udhaifu na pia ufahamu kinachoendelea kwenye soko .

Nao  Philip Luke , mratibu wa mafunzo wa chuo hicho cha KITM na mwezeshaji wa mafunzo Dani Kishimbo walisema mafunzo yamekuwa na umuhimu mkubwa kwa wafanyakazi na wanafunzi kwa sababu wamepata maarifa mapya namna ya kuandika CV na kuanzisha biashara zao. 
‘’ Tumepata maarifa mapya ya namna ya kuanzisha biashara zetu wenywe na pia namna ya kujiweka na kujibu maswali wakati wa usaili . Tunafahamu namna ya kujiweka kujibu maswali inavyotakiwa ‘’ alisema Philip Luke. 
Dani Kishimbo, mratibu wa mafunzo alisema mafunzo yamekuwa na umuhimu mkubwa na maarifa waliyoyapata wanafunzi watayatumia kuomba mazoezi kwa vitendo au ajira. 
Mwishoni mwa mafunzo hayo washiriki walipewa vyeti na mmoja wao Abdala Kipinga aliwashukuru walimu wa mafunzo na kusema amejifunza mengi ikiwemo namna ya kuandaa mikutano , CV pamoja na kuanzisha biashara. 
Restless Development Tanzania (ICS) mtazamo wao ni kusaidia vijana kuchukua jukumu la kuwa viongozi kwa kutatua changamoto zinazokabili nchi zao na dunia kwa ujumla.
Taasisi hiyo inatekeleza mtazamo huo kwa kuwajengea uwezo vijana kimaarifa , kimsukumo na raslimali kuchukua nafasi za kazi ambazo zinachangia sio tu  katika kipato cha familia bali pia uchumi wa jamii pamoja nan chi zao. 
Mafunzo hayo yamekuja huku kukiwa na  ripoti ya baraza la vyuo vikuu vya Afrika ya mashariki ikisema karibia nusu ya wahitimu wanaozalishwa na vyuo vya nchi hizo hawana uzoefu katika soko la ajira.Ripoti hiyo inasema  wakati maelfu ya vijana wanamaliza kila mwaka , sifa walizokuwa nazo vijana wengi haziwezi kuwasaidia kuwapa kazi na waajiri wanawaacha wanawachukua wenye ujuzi jambo linaloleta changamoto la ukosefu wa ajira katika ukanda huu. 

Kwa mujubu wa Katibu wa baraza hilo , Professor Mayunga Nkunya a, waajiri wanasema wahitimu wengi wa vyuo wanakosa kujiamini , hawawezi kujieleza vizuri na hawana ujuzi wa kitaalam unaotakiwa katika kazi wanazotafuta .

No comments: