Saturday, March 7, 2015

MKURUGENZI MKUU MPYA WA TBL AKAGUA MAJENGO WALIYOYAKABIDHI KWA CHUO KIKUU CHA STEPHANO MOSHI

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiongozwa na mkufunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Gasper Mpehongwa kutembelea vyumba vya madarasa ambavyo vinatumika kwa ajili ya masomo pamoja na mitihanikatika eneo la TBL mjini Moshi.Eneo hilo limetolewa na TBL kwa chuo hicho ikiwa ni kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi.

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin akiwa ameambatana na mkuu wa chuo Kikuu Kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,Profesa Anord Temu,wakati akitembelea majengo ya jengo hilo mjini Moshi.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrinakizungumza wakati wa mkutano wake na waaandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha kimea cha Moshi nachuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrinakizungumza wakati wa mkutano wake na waaandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha kimea cha Moshi na chuo kikuu kishiriki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi,
 Meneja Udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania,(TBL), George Kavishe  akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya msimu wa 14 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni 2015 zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Roberto Jarrin akiwa ameongozana na viongozi wengine wa TBL kutembelea kiwanda cha kutengenezea Kimea kwa ajili ya kutayarisha Bia kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro.
 Baadhi ya viongozi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzimkuu wa TBL ,Roberto Jarrin muda mfupi mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha Kimea cha Mjini Moshi,
 Mkurugenzi mkuu  wa kampuni ya Bia Tanzania ,TBL ,Roberto Jarrin,akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo Kikuu kishirki cha kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMMUCO), Anord Temu (kushoto) wakati alipofanya ziara kutembelea Chuo hicho ambacho eneo pamoja na majengo yanayomilikiwa na TBL yametolewa kwa chuo hicho.

No comments: