Tuesday, March 31, 2015

Frederick Mwakalebela Asema jimbo la Iringa mjini 2015 Mali ya CCM


Kamanda wa uvccm wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela akiwahutubia wananchi ktk uwanja wa mwembetogwa ktk mkutano ulioandaliwa na uvccm Iringa mjini
Wananchi Iringa mjini wakiwa ktk mkutano wa uvccm Iringa mjini
kada  wa CCM Bw Ahmed Mbata  mwenye miwani akimzuia  kijana wa CCM kuendelea  kumthibiti kada wa Chadema  aliyeanguka chini baada ya  kupigwa  kwa  tuhuma za  kutaka  kuvuruga mkutano wa UVCCM
Vijana  wa CCM  wakisogea  kumshambulia  kijana aliyetaka  kuvuruga mkutano  wao
Wananchi  wakimtazama  kijana  wa Chadema aliyetaka  kuvuruga  mkutano wa CCM
Wananchi  wakitazama  tukio  hilo
Askari polisi akizuia  vurugu  hivyo
Mwakalebela  kushoto  akiwa na katibu wa UVCCM  Iringa

Na MatukiodaimaBlog, 
Iringa
KAMANDA  wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa mjini Frederick Mwakalebela atuma   salam kwa  upinzani  jimbo la Iringa mjini  kuwa mwisho wao kuongoza jimbo hilo ni oktoba  mwaka huu hivyo wananchi wajiandae kwa sherehe za kulipokea jimbo.

Akizungumza leo   katika mkutano wa uvccm Iringa mjini uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa.
Alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akikodi majeshi (wanasiasa wenzake )nje ya Iringa mjini ili kusaidia mashambulizi baada  ya  kuona  hali ya  upepo kwakwe  si nzuri.
" naomba kuwahakikishieni kuwa jimbo hili tulikosea mwaka 2010 ila kwa mwaka huu haturudii kosa lazima jimbo lirudi CCM".
Hivyo alisema kuwa ni ukweli usiopingika kuwa lazima Chadema wajipange kukabidhi jimbo hilo kwa Ccm na kuwa maandalizi ya kupokea yamekwisha fanyika.
Akielezea kuhusu umuhimu wa vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura alisema ili Ccm uweze kushinda kuanzia udiwani ,ubunge na Urais ni lazima wakajitokeza kujiandikisha ktk daftari hilo.
Kwani alisema hakuna ushindi bila ya vijana kujitokeza kujiandikisha na kuwa iwapo kila mmoja atajiandikisha ushindi wa CCM upo wazi.
Kwa upande  wake katibu wa CCM mkoa  wa  Iringa  Hassan Mtenga  akihutubia  wananchi hao  alisema  kuwa   mbunge msigwa  anapaswa  kujiandaa kisaikolojia  kwani  CCM imejipanga  vema  kuona  jimbo  hilo  linarudi  mikononi mwa CCM kwa  mwaka  huu.
Alisema  kuwa  jimbo hilo  CCM kililianzimisha kwa Chadema  hivyo muda wao wa  kuendelea  kulikalia  umepitwa  kutokana na  mbunge  kushindwa  kuwatumikia  vema  wananchi wa  jimbo  hilo  wakiwemo  vijana ambao  waliahidiwa ajira  ila hadi leo vijana Iringa mjini  wamegeuka  omba omba kutokana na  kutokuwa na ajira.
Hivyo  alisema  mbali ya  mbunge  wa  sasa  muda  wake  kumalizika  bado anapaswa  kuwaeleza  wananchi  wa  jimbo la Iringa  mjini matumizi ya  fedha za mfuko wa jimbo ambazo amekuwa akizipata  zimefanya kazi gani katika   jimbo  hilo lasivyo CCM itakuja na orodha kamili ya ahadi  zake na  kiwango halisi  cha   fedha za mfuko wa  jimbo.
Mtenga  alisema  Chadema  imekuwa  ikiendesha  siasa  za  vurugu  kwa  kuwatumia  vijana  kuvamia  mikutano wa CCM hasa  pale  wanapoona  wananchi  wamejitokeza kwa  wingi kwa  lengo la kutaka  kuivuruga na kuwa  kuanzia sasa  CCM inawaomba vijana  hao kuacha  kutumika kwa mashali ya  wachache na  kuwa  iwapo  watashindwa  uvumilivu wa  sera za CCM ni  vema  wasifike katika katika  mikutano badala ya  kufika kwa lengo la  kufanya fujo.

No comments: