Afisa Mtendaji Mkuu Dr Kamugisha Kazaura atembelea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Mbeya ikiwa na lengo la kukagua miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa TTCL wa mikoa hiyo.
Dr Kazaura ailijionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa TTCL katika kuhakikisha miundombinu ya TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano inakuwa salama muda.
Hivi sasa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekuwa kampuni pekee ya mawasiliano ambayo imefanikiwa kuunganisha wateja mbalimbali kupitia mtandao wake.
Wateja hao ni pamoja na TAMISEMI, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mabenki, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG),Wizara ya Fedha, watoa huduma za mtandao/intaneti (ISPs) pamoja Makampuni ya Simu
Pia TTCL imefanikiwa kuunganisha nchi jirani katika ukanda huu wa afrika Mashariki (Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda) pamoja na nchi za kusini wa Jangwa la Sahara (SADC) ambazo ni Malawi na Zambia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua mitambo ya TTCL mkoani Lindi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akipokea maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TTCL Mtwara kuhusu juhudi zinazofanyika kulinda na kusimamia mitambo yake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akikagua Mtambo wa Mkongo wa Taifa, pembeni yake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi wa TTCL,Senzige Kisenge
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na mafundi ambao wanajenga Barabara katika mkoa wa Ruvuma, akiwasisitiza walinde Mkongo wa Taifa.
Meneja wa TTCL mkoa wa Lindi- John Nindwa akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatwa na wezi katika hifadhi za Taifa ya Selous na juhudi zilizofanyika katika kurejesha mawasiliano Ruvuma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ufundi Senzige Kisenge na Kushoto Mkuu wa Biashara Nyanda za juu Kusini, Juvenal Utafu.
Hii ni baadhi ya maeneo ambayo awali Mkongo wa Taifa ulikatika kutokana na mmomonyoko wa ardhi, lakini TTCL ilihakikisha inapitissha Mkongo juu kwenye nguzo za Simu ili kurejesha mawasiliano.
Wafanyakazi wa TTCL wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura wakiangalia eneo ambalo Mkongo wa Taifa ulikatika mkoani Njombe kutokana na mmomonyoko wa ardhi , lakini juhudi zilifanyika usiku na mchana kuhakikisha mawasiliano yanarejea katika hali yake ya kawaida.
Hali halisi ya mmomonyoko wa ardhi uliosababishwa na mvua kubwa ailionyesha Mkoani Njombe na kusababisha Mkongo wa Taifa kukatika.
JPG Wafanyakazi wa TTCL Mbeya wakiwa katika mkutano ambao uliitishwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dr Kazaura ikiwa ni sehemu ya kuzungumza na wafanyakazi wake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mkoani Mbeya.
Dr Kazaura akizungumza na Afisa wa Malawi baada ya kutembelea Mkongo wa Taifa eneo la Kasumulo mpakani kati ya Tanzania na Malawi.
Kaimu Meneja Mkoani Mtwara Kilango Bakari akieleza juhudi zinazofanywa na TTCL katika kutoa huduma kwa wateja wake mkoani Mtwara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kazaura akizungumza na wafanyakazi wa TTCL mkoani Lindi. Aliyesimama ni Mkuu Biashara Kanda ya Kusini Hussein Nguvu akieleza juhudi zinazofanywa na Mkoa katika kusimamia mkongo na shughuli za TTCL kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment