Askari wa FFU wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana kama njia ya kulinda amani kwa wafanyabiashara ambao waliendelea kutoa huduma baada ya wenzao kuwa katika mgomo |
MOja kati ya maduka mjini Iringa yakiendelea kutoa huduma mbali ya wafanyabiashara wengine kuwepo katika mgomo kushinikiza kuachiwa huru kwa mwenyekiti wa wafanyabiashara Taifa Bw Johnson Minja |
Maduka mtaa wa uhindini mjini Iringa yakiwa yamefungwa jana kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara nchini |
Na matukiodaimaBlog
BAADHI
ya wafanyabiashara mkoani Iringa wamegoma kuungana na
wafanyabiashara wenzao nchini kushiriki mgomo wa kushinikiza
jeshi la polisi kumwachia huru mwenyekiti wao wa chama cha
wafanyabiashara nchini Bw Johnson Minja anayedaiwa kushikiliwa na
jeshi la polisi kwa mahojiano.
Wafanyabiashara
hao waliosusia mgomo huo walifikia uamuzi huo kama hatua ya
kupinga uamuzi wa wenzao ambao walifunga maduka yao kwa siku nzima
kuungana na wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam ambao
walifanya hivyo .
Uchunguzi
uliofanywa na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa
na maeneo ya nje ya mji wa Iringa ulionyesha kuwa mgomo huo
kukosa ushirikiano kutokana na baadhi ya maduka ya pembezoni mwa mji
wa Iringa na yale ya vijijini na baadhi ya maduka ya katikati ya mji
wa Iringa kuendelea na huduma kama kawaida huku wakiomba ulinzi kwa
jeshi la polisi ili wao kuendelea kutoa huduma kama kawaida.
Huku
cha kushangaza hata baadhi ya salun na bucha za nyama katika
baadhi ya maeneo mjini hapa zilifungwa huku baadhi ya maduka
yanazozunguka soko kuu la Iringa pia yakifungwa japo katika soko
hilo umati mkubwa wa wananchi waliendelea kupata huduma kama kawaida .
Mmoja
kati ya wafanyabiashara wa mji wa Iringa Bw JOhn sanga alisema
kuwa ameshindwa kuungana na wafanyabiashara wa mji wa Iringa katika
mgomo huo kutokana na shinikizo kubwa ambalo lilikuwa likionyeshwa
na watu waliokuwa wakisambaza jumbe za mgomo huo juzi na jana
kupitia kikundi cha watu kama 11 ambao wengi wao walikuwa
wakitoa vitisho wakati wa kusambaza taarifa hizo.
"
Kweli nimeshindwa kufunga duka langu leo kutokana na vitisho vya
watu hao ambao wanatulazimisha kufunga kwa nguvu huku wakitambua
kuwa si kila mfanyabiashara ni mwanachama wa chama chao hicho
cha wafanyabiashara ....kutulazimisha kufunga biashara zetu ni
kutunyanyasa sisi tusio wanachama na tambua kila mmoja ana maisha
yake wao badala ya kukutana viongozi kwa ajili ya kulimaliza suala
hilo wanataka wote tufunge maduka huu ni ushauri mbaya kuliko "
Hata
hivyo alisema hajaweza kufunga na ataendelea kutoa huduma wakati
wote wa mgomo wa wafanyabiashara hao kwani si lazima kila
mfanyabiashara kuungana nao katika chama chao na kiongozi wao .
Huku
mfanyabiashara Geofrey kalinga akieleza kusikitishwa na serikali
kushindwa kuchukua hatua kali kwa kikundi hicho cha
wafanyabiashara wachache ambao wanachochea mgomo huo na kuwakosesha
wengine amani ya kufungua biashara zao na kuwa kuendelea
kuchelewa kuchukua hatua ni kubariki migomo kama hiyo kuendelea .
Kwani
alisema ni jambo la kushangaza kuona watu hao wachache wakitumia
nguvu kuwazuia wengine kuungana nao katika mgomo huo huku
wakitambua kuwa chama hicho ni chama cha hiari kujiunga ama
kutojiunga hivyo walipaswa kushughulika na wanachama wao na sio
wafanyabiashara wote.
"
Haya ni mambo ya ajabu sana hivi inawezekana vipi hiki kikundi cha
wachache kutulazimisha wafanyabiashara wote kujiunga na chama chao
......sasa leo wanatutaka kufunga biashara kwa muda usiojulikana
kesho watakuja na jambo jingine lakini swali la msingi hapa hicho
chama chao kinatusaidia nini sisi ambao si wanachama tunapofungiwa
biashara zetu ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa kuchelewa
kulipa kodi....ama wanatusaidia vipi na kodi kubwa ya mapango ya
vyumba vya biashara ambazo tumekuwa tukilipa .....kama jibu hakuna
basi watuache na wao waendelee na migomo yao"
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi wafanyabiashara waliofunga maduka yao
walisema kuwa sababu ya kufunga maduka kwa muda usiofahamika ni
kutoka jeshi la polisi kumwachia huru kiongozi wao kitaifa Bw Minja
anayedaiwa kukamatwa toka juzi na jeshi la polisi na hajulikani
alipo.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Iringa Suzana Ndelwa alisema kuwa
kufungwa kwa maduka katika mji wa Iringa kumewaathiri wananchi
kiuchumi kutokana na baadhi yao kutoka nje ya mji wa Iringa kufuata
huduma za jumla ila kufungwa kwa maduka hayo kumeyumbisha uchimi
wao na wa Taifa kwa ujumla na kuwa ilipaswa kwa upande wa mkoa wa
Iringa mkuu wa mkoa huo kuingilia kati suala hilo .
Mbali
ya baadhi yao kutoma kufunga maduka yao bado ule usemi wa kufa
kufaana ulionekana kutawala katika maeneo mengi ya mji wa Iringa
kutokana na mgomo huo baada ya baadhi ya wafanyabiashara wadogo
maarufu kama machinga kunufaika zaidi na mgomo huo kwa kupanga
bidhaa zao nje ya maduka yanayofanya biashara kama zao na kupata
wateja zaidi kupitia mgomo huo huku baadhi ya wafanyabiashara
wakionekana kuuzia bidhaa zao stoo na wengine kufungua maduka yao
nusu mlingoti na kuendelea kutoa huduma kama kawaida.
Wakati
wafanyabiashara hao wakiwa katika mgomo huo mjini Iringa ,Mafinga
na baadhi ya wachache wa Ilula bado jeshi la polisi lilionekana
kuweka ulinzi wa kutosha katika maeneo ya wafanyabiashara hao
huku askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)) wakionekana
kuzunguka kila kona ya mji wa Iringa ili kuthibiti vurugu iwapo
zingejitokeza.
Jitihada
za kumpata mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ama kamanda wa
polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ili kuweza kuzungumzia
jinsi mkoa ulivyojipanga kumaliza tatizo hilo la mgomo ama jeshi la
polisi lilivyojipanga kuwalinda wafanyabiashara ambao waligoma
kuungana na wenzao katika mgomo huo hazikuzaa matunda baada ya simu
za viongozi hao wawili kuita bila kupokelewa .
No comments:
Post a Comment