Thursday, January 22, 2015

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LEO

 Baadhi ya Vijana wa CCM wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake.alipowasili Kikobweni katika ukumbi wa MKorea,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja.

 Ktibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Wanachama wa kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara mara baada ya kushiriki kupanda Migomba,katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mgomba katika shamba la Kikundi cha Ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga  katika Kijiji cha Banda Maji,Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.
 Mbunge wa Jimbo la Chaani,Mh.Ally Juma Haji a.k.a Chepe akizungumza na baadhi ya vijana kuhusiana mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahimiza kupiga kura ya ndio kwa katiba inayopendekezwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa tawi la CCM Chaani Masingini,jimbo la Chaani ambapo pia alipokea taarifa ya ujenzi wa tawi hilo na kusalimiana na Wananchi,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini  Unguja.
 Msafara wa Katibu Mkuu,Ndugu Kinana ukielekea kwenye Mradi huo wa ujenzi wa barabara unaofadhiriwa na TASAF
 Baadhi ya Wananchi wanaoshiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo.Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 ina thamani ya shilingi milioni 26
 Katibu mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kazi ya ujenzi wa barabara katika kijiji cha Kijini kwa Shauripili,jimbo la Shaani,wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa kwa mradi wa TASAF,barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.7 yenye thamani ya shilingi milioni 26
Mradi wa ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80 ukiendelea,Mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini,jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80.Mradi huo huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na viongozi wengine wa CCM,wakitazama mchezo wa sarakasi unaofanywa na vijana mara baada ya kupokea taarifa fupi ya ujenzi wa wa jengo la  ya Nyumba ya Madaktari inayojengwa katika Sheia ya Kijini katika jimbo la Matemwe,Wilaya ya Kaskazini A,mkoa wa Kaskazini Unguja,yenye thamani ya shilingi milioni 80,nyumba mradi huo umejengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali pia.
 Baadhi ya viongozi wa timu za mpira wakiwa na vifaa mbalimbali walivyopokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,mara baada ya kukagua na kushiriki kazi ya ujenzi wa uzio wa Uwanja katika sheia ya Tazari,jimbo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kigunda,mara baada ya kupokea taarifa fupi ya jengo la SACCOS ya vijana yenye Wanachama 114.SACCOS hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuisaidia jamii katika suala zima la kuweka unafuu wa kukopa kirahisi. 
 Balozi wa Shina namba 3,Balozi Khamis Makame Faki akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na baadhi ya wananchi na wanachama,katika jimbo la Nungwi,wilaya ya Kaskazini A,Mkoa wa Kaskazini Unguja,Ndugu Kinana alifika kwa balozi huyo na kukagua uhai wa chama na Wanachama.
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Banda Maji mara baada ya kupokea taarifa ya kikundi cha ushirika wa Tuko Imara unaojishughulisha na Kilimo cha Migomba na Mbogamboga,pia kushiriki kazi ya kilimo cha Migomba na Mbogamboga,katika Wilaya ya Kaskazini A mkoa wa Kaskazini Unguja mapema leo.

No comments: