Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wakikagua moja ya mabehewa mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya serikali wakati alipokwenda kwenye Bandari ya Jijini Dar es salaam leo Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa hayo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba (kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini (TRL) yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye bandari ya jijini Dar es salaam leo Desemba 8,2014.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiangalia jiko ambalo liko ndani ya behewa la daraja la pili kwenye moja ya mabehewa 22 yaliwasili nchini mwisho wa wiki, katika bandari ya jijini Dar es Salaam, leo Desemba 8,2014.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akishuka kwenye moja ya mabehewa 22 yakiyowasili nchini mwisho wa wiki, leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.Mh. Pinda alifika Bandarini hapo kukagua mabehewa hayo. Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Uchukuzi pamoja na watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Kuimarisha usafiri wa Reli nchini. Utekelezaji wa mradi huu ni mojawapo wa Miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa(BRN).
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment