Saturday, December 27, 2014

DK. SHEIN AFUNGA MASHINDANO YA RIADHA UWANJA WA AMAAN,ZANZIBAR

Wanamichezo kutoka wilaya ya Kaskazini A Unguja na Kusini Unguja wakiwa katika uwanja wa Amaan Studium wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium yaliyofungwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Bi Sharifa Khamis (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama (kushoto) baada ya kutoa nishani kwa wakimbiaji wa mashindano ya Riadha wakati wa ufungaji katika uwanja wa Amaan Studiam leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas Chasama alipokuwa akitoa salamu za Chama Riadha mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa ufungaji wa mashindano ya Riadha kwa Wilaya ya Kumi za Unguja na Pemba katika Uwanja wa Amanaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mtoto Sofia Kombo Makame aliyekimbia umbali wa kilomita nyingi kutokana na umri wake katika mashindano ya Riadha zawadi hiyo alipewa wakati wa ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba katika uwanja wa Amaani Studium leo Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikabidhi Kombe la Ushindi wa Jumla kwa Kassim Hussein Saleh na fedha tasilimu Shilingi Millioni Moja akiwakilisha wilaya ya Mjini iliyopata medali 17 za zahabu,13 fedha na 5 za Shaba katika ufungaji wa Mashindano ya Riadha katika Wilaya kumi za Unguja na Pemba aliyoyafunga leo katika uwanja wa Amaani Studium (kushoto) Kaimu Waziri wa Habari,Utalii,Utamadunu na Michezo pia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilahi Jihadi Hassan.Picha na Ikulu.

No comments: