Saturday, October 25, 2014

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,LAZARO NYALANDU ATEMBELEA OFISI ZA HIFADHI YA TAIFA YA ARUSHA (ANAPA)

Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akishuka kwenye gari alipowasili ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA).
Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akimuonesha Waziri Nyalandu mfano wa mtambo wa kufua umeme unaotazamiwa kuwekwa katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu ,Hifadhi ya Taifa ya Arusha(ANAPA) Betrita Loibook akitoa taarifa ya Hifadhi hiyo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu.
Waziri Nyalandu akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Hifadhi ya taifa ya Arusha,
Baadhi ya watendaji wa TANAPA,wakimsikiliza Waziri Nyalandu alipotembelea hifadhi ya taifa ya Arusha.toka kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA ,Paschal Shelutete,Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufungulo na Betrita Loibook ,Mhifadhi Mkuu Arusha National Park. 
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akiteta jambo na Mhifadhi Mkuu Arusha National Park,Betrita Loibook.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar walipokutana katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha na kumshawishi kutembelea hosptali ya Africa Amini Hearing Center.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,
Kanda ya Kaskazini.

No comments: