Saturday, August 30, 2014

Zijuwe Faida za Mazoezi ya Yoga


Na Sensei Rumadha Fundi
KUTAFAKARI/MEDITATION
Kutafakari "Meditation" au katika lugha ya Sanskrit "Dhyana"  ama mtiririko wa mawazo  ni moja ya sehemu kuu Yoga inasisitiza kuidumisha katika sanaa hii ya upanuzi wa mawazo.
Falsafa  ya Yoga inaamini kwamba ubongo wa mwanaadamu unatoa msisimko wa mawimbi ambayo huwasumbua sana binaadamu kuweza kutumia uwezo wao wa fikra katika asilimia 100, na hatimae mwanadamu hutumia tu asilimia 1, ya fikra zake na zote asilimia 99 hupotea kutokana na upungufu wa utulivu wa mawazo ya mwanaadamu ( Concentration/ Focus).

Hivi karibuni tu, uvumbuzi mpya wa sayansi ya Yoga amegundua kwamba ubongo wa mwanaadam umejengwa katika mchanganyiko wa mabillion ya "Nervr Cells, hatimae kutoa mkondo mdogo wa umeme ( tiny electric current) ijulikanayo kama "Brain waves" ambayo  hubadilika kila sekunde kufatana na mabadiliko ya nguvu za ufahamu wako katika ubongo. Mashine yenye uwezo wa kuweza soma mawimbi hayo ya ubongo hujulikana kama "EEG", au "Electroencephalogram" Chombo hiki kinapo fungwa kichwani mwa binaadamu hutowa mawimbi na kuyasajiri kupitia mashine ya computer screen na kutoa mawimbi yenye kina tofauti kutokana na nguvu za ubongo wa mtu., yaitwayo:

Beta Wave:
 Mawimbi  ya mizunguko 13 kwa dakika ya ubongo : kutokuwa na utulizu wa fikra'Stress/ Restless" 
Alpha Wave:
 Mawimbi ya mizunguko 8 kwa dakika:  msukumo imara kidogo wa nguvu "Steady and rythmic Amplitude". 
Theta Wave:
 Mawimbi ya  4 kwa dakika: Mawazo yenye nguvu za ubongo, ubunifu na usanifu wa kisayansi ubongo umetulia.
 Delta Wave:
 Wimbi la 1 kwa dakika. Hapa nikupitia tu njia ya kutafakari ndio mtu huweza kufikia hatua hii ya wimbi moja kwa dakika. Ubongo wenye nguvu zisizo kawaida " Intuitive mind/ subtler mind". Moja ya ngazi hii ina uwezo wa kuwa utabiri wa matokea ya mbele kutokana na upeo  wa fikra.
Lengo kuu la "Meditation" ni kuwa na uthibiti wa mawimbi ya ubongo kuweza kupunguza kasi yake toke a mawimbi 13 kwa sekunde hadi  wimbi  1 kwadakika na ubongo huo ndio upo katika watu wenye upeo wa fikra zilizotulia kama maji ndani ya mtungi. Maji ya mtungi au kisima yakitulia ina kuwa kama vile kioo, ukiangalia ujiona mwenyewe. Kama maji yakitibuliwa hutoawa mawimbi mengi na kusababisha mvurugano nakutoweza kuona  kimvuli chako mwenyewe au " Reflection."
Kupitia sauti itwayo "Matra", ubongo hutumia mbinu hiyo kama chombo cha kukufikisha pale unakotaka kwenda. Pia Yoga ina masomo ya ngazi nyingi (Lessons).
Moja ya vitu sanaa Yoga inasaidia kuweza kumudu (Control) ya hisia zako mwilini  yaani " Emotion", "propensities"  kusaidia " Secretions  of Hormones" kumudu hasira   kupitia mazoezi  yenye  utafiti wa kuiga mikao ya wanyama  kadhaa na ndege ambayo inaaminika wanatumia kwa  kujitibu  wenyewe. bila kutumia dawa. Mikao yote ya Yoga (Yoga Postures) inasaidia matatizo kama vile:
Shindikizo la damu( High blood Pressure), uzito wa mwili ( Obesity), kisukari ( Diabetes) na matatizo kadhaa ya magonjwa ya wanawake. Hivyo basi, Yoga ina faida nyingi mno ambazo watu wengi hawazifahamu.
Yoga inaamini kwamba, kuna sehemu 7 za nguvu  ndani ya mwili wa mwanaadamu kupitia uti wa mgongo  au "Kun'da'alini " katika lugha ya Sansrit ( Coiled Serpentine). Sehemu hizo ni :
1.Muladhara Chakra: ipo katika mkia wa  ya uti wa mgongo 
2. Sva'dhis;tha'na Chakra:ipo sehemu ya kizazi (Groin area) 
3. Man'ipu'ra Chakra: ipo kitovuni. 
4. Ana'hata Chakra katika ya kifua. 
5. Vishuddha Chakra: ipo koromeo (Thyroid Gland) 
6. A'jna Chakra: ipo katikati ya macho (Pituitary). 
7. Sahasra'ra Chakra: Ipo katika utosi.

Mwafunzi anapozidi kuendelea kwa kina katika sanaa ya Yoga, ndipo anapo pita hizo sehemu ya nguvu 7 katika uti wa mgongo na hatimaye kufikia hatua ya kuwa na udhibiti wa hizo hisia zake mwenyewe au  "Propensities".
Sayansi ya Yoga nipana sana yenye kina kirefu na filosofia yenye karne. Mazoezi ya Yoga husaidia viungo vya ndani ya mwili (Internal Organs) kama vile moyo,figo, maini, kwa kuvikanda ( massage) zaidi ya mwili wanje. Tofauti ya mazoezi ya gym na Yoga ki kwamba: Ukifanya mazoezi  gym ( vigorous exercise) unatumia sana nguvu na kuchoka haraka, wakati mazoezi ya Yoga ( Yoga Asanas) unalinda nguvu za mwili (Conserve Energy) hata kama na umri wa uzee sana na kuwa umetulia (Relax). Yoga ina njia yake ya tiba vilevile ijulikanayo kama: "Yogic treatment and remedies"
Haya ni machache tu kuhusu nini hasa faida ya mazoezi ya yoga na mazoezi aina nyingineyo.
Sensei Rumadha pia ni mkufunzi wa sanaa ya Karate mtindo wa "Okinawa Goju Ryu Jundokan Kyokai". Kabla ya hapo, hususan akiwa nyumbani Tanzania, Sensei Rumadha alikuwa mmoja wa wanafunzi waandamizi wa Marehemu Sensei Nantambu Camara Bomani ambaye ni mwanzilishi wa mafunzo ya karate aina ya Goju Ryu pale Zanaki, jijini Dar es salaam miaka ya 1980.


3 comments:

Anonymous said...

Tunampataje huyu mwl wa yoga? Hajaweka contacts zake. Tafadhali tusaidie. Angedax

anonimous said...

Nahtaji kujua anapatikana wapi na contact zake nazipataje

MICHUZI BLOG said...

Mtaalamu huyu anaishi Marekani mwandikie rfundil@yahoo.com