Friday, August 22, 2014

SERIKALI YAKIPONGEZA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO (UB)

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Mahalu akizungumza wakati wa kufunga  Mafunzo hayo ya siku 14 yaliyoshirikisha maofisa wa juu wa fani ya biashara wa Serikali za nchi nane ambayo yaliratibiwanna Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB) ambayo yalifadhiliwa na Chuo Kikuu Cha  Nordric Africa Institute.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Tunajifunza..........
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Elifuraha Mtalo (wa pili kushoto) akifuatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Mahalu
Professa Francis Matambalya akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.

Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Mahalu (katikati) akiwa na Mkuu wa Shule ya Elimu Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Elias Bayona (kushoto) na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Dk. Jonathan Mbwambo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Dk. Jonathan Mbwambo akizungumza wakati wa kufunga Mafunzo hayo ya siku 14 yaliyoshirikisha maofisa wa juu wa fani ya biashara wa serikali za nchi nane ambayo yaliratibiwanna Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB) ambayo yalifadhiliwa na Chuo Kikuu Cha  Nordric Africa Institute.
Mkuu wa Shule ya Elimu Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Prof. Elias Bayona akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Malawi, Heather Kachingwe akipokea cheti chake.
Picha ya pamoja.

Na Happiness Katabazi

SERIKALI imewataka  washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kujadili  mikataba ya Biashara na uwekezaji  kutumia taaluma hiyo waliyoipata kwaajili ya kuleta manufaa kwa mataifa Yao.


Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Elimu ya Juu ya Wizara ya Elimu ya Juu,  Dk.Jonathan Mbwambo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk.Shukuru Kawambwa  wakati akifunga  Mafunzo hayo ya siku 14 yaliyoshirikisha maofisa wa juu wa fani ya biashara wa serikali za nchi nane ambayo yaliratibiwanna Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB) ambayo yalifadhiliwa na Chuo Kikuu Cha  Nordric Africa Institute, Uppsalla cha nchini Sweeden chini ya Profesa Francis Matambalya na kuwezeshwa na Taasisi ya TANAUP/PATU  chini ya Profesa Vale Karugaba.


Dk.Mwambo Alisema kwanza serikali  inakipongeza Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), kwa kuandaa Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha maofisa wajuu wa serikali mbalimbali Kwani kupitia Mafunzo Hao maofisa Hao wameweza kubadilishana uzoefu wa masuala ya nchi zao kuhusu Sekta ya masoko na uwekezaji.


Dk.Mwambo alisema kila kukicha baadhi ya nchi za Africa zimekiwa zikigundulika kuwa na utajiri mkubwa aridhini na mfano mzuri ni nchi ya Tanzainia ambayo imegundulika kuwa ina nishati ya gesi , madini hivyo kupitia mafunzo hayo  kwa upande wa Tanzania  Wizara ya Viwanda na Biashara iliwakirishwa na maofisa wake Wawili wameweza kupata ujuzi ambao utaki saidia serikali ya kuweza kufanya vizuri Katika uandaaji wa masoko na uwekezaji wafanyabiashara wa Kimataifa watakaokuwa wanakuja kuwekeza nchini.


Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Profesa Costa Mahalu  Alisema UB,  nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zimekuwa  zikikabiliwa na matatizo  ya jinsi ya kuandaa masoko na kuandaa mikataba yenye tija na wawekezaji hivyo kupitia Mafunzo hayo yamesaidia kuwajengea uwezo washiriki kwenda kukabiliana na Changamoto hiyo.


Profesa Mahalu  Alizitaja nchi zilizoshiriki Katika Mafunzo hayo ya Kimataifa Kuwa ni wenyeji Tanzania, Kenya,Uganda, Burundi, Rwanda, Lesoto, Kongo, Malawi ,Ethiopia , Zambia na Madagascar.


Alisema UB Katika Mwaka mpya wa masomo    inaanza kutoa Shahada ya jinsi ya kujadili mikataba ya biashara na uwekezaji  ili iweze kuwajenga wanafunzi wengi wa Watanzania waweze kuwa bora katika eneo hilo la masoko na kuandaa mikataba ya kuiingia na wawekezaji katika sekta mbalimbali.


Kwa upande wake Profesa Francis Matambalya toka  Taasisi ya Nordic Africa  ya Chuo Kikuu Cha Uppsala, cha nchini Sweden ambao ndiyo waliofadhili Mafunzo hayo Alisema Kuwa yeye ni Mtanzania na anampenda nchi yake na ataakikisha kila Mara Taasisi hiyo ya Sweden inaleta Fedha kwaajili ya kuendesha Mafunzo hayo ili nchi za Tanzania na Africa kwa ujumla ziondokane na tatizo la kutokuwa na wasomi waliobobea Katika eneo Hilo la kuandaa masoko na jinsi ya kuandika mikataba na wawekezaji wa kigeni Katika sekta mbalimbali.

No comments: