Thursday, April 24, 2014

WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA ASTAAFU SIASA ,JK AMPONGEZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa viongozi wengine wakuu wa serikali chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana (kushoto) katika hafla ya kumuaga aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania mara mbili katika awamu mbili tofauti, Mzee Cleopa David Msuya (wa kwanza kulia kwa Rais) ambaye amestaafu rasmi siasa baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka 33.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM wilaya ya Mwanga leo
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa.
Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.

Kundi la wazee wa kimila wakiongozwa na Mzee Kasim Msemo wakimkaribisha Mzee Msuya kijijini
 Mzee Msuya akiwa amekaa kwenye kiti cha jadi kama ishara ya kurudi rasmi kijijini baada kutangaza kustaafu siasa
 Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.
 Mamia ya Wananchi waliokusanyika kushuhudia hafla hiyo

Picha zote na Dixon Busagaga wa 
Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.

No comments: