Thursday, April 24, 2014

MWAKALEBELA AWATAKA WAJASILIAMALI IRINGA KUEPUKA MATAPELI KATIKA MIKOPO YA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA

Wanawake  wajasiliamali mjini Iringa  wakipewa maelekezo kutoka  mkurugenzi   mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela (kulia)  wakati wa  semina  hiyo  inayoendelea katika ukumbi wa maendeleo ya jamii mjini Iringa
Wajasiliama mali  wanaotarajiwa  kukopeshwa na benki ya wanawake Tanzania  wakipewa mafunzo  leo
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi mkoa wa Iringa Mariam Mwakingwe  wa kwanza kulia mwenye suti  akiwasikiliza  wakufunzi kutoka benki ya wanawake Tanzania ambao  wapo mjini Iringa kwa ajili ya kuwakopesha
Mwakalebela  katikati akiwa na wakufunzi wa mafunzo ya ujasiliamali wanaopaswa kupewa mikopo ya benki ya wanawake Tanzania
Mwakalebela katikati akitoa maelekezo kwa  wajasiliama mali wanaohitaji mikopo ya benki ya wanawake Tanzania
  baadhi ya  wajasiliamali wenye ulemavu  wanaoshiriki  semina ya ujasiliama mali chini ya ufadhili wa kampuni ya VANNEDRICK (T) Ltd kwa  ajili ya kukopeshwa fedha na Benki ya  wanawake  Tanzania (TBW) wakimsikiliza mkurugenzi   mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela (katikati)  wakati wa  semina  hiyo  inayoendelea katika ukumbi wa maendeleo ya jamii mjini Iringa


Na  Francis Godwin Blog 
MKURUGENZI  mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela  amewataka wajasiliamali mjini Iringa  kuepuka matapeli  wanaotaka  kuwatoza fedha ili kunufaika na mikopo ya benki ya  wanawake Tanzania (TBW).

Pia Mwakalebela  amepongeza  jitihada za  wanawake na  wajasiliama mali mjini Iringa  kujitokeza kwa wingi katika mafunzo ya ujasiliama mali kabla ya kukopeshwa na benki  hiyo hivi karibuni .

Akizungumza  jana wakati wa mwendelezo wa  semina  hiyo kwa wajasiliama mali katika  ukumbi wa maendeleo ya jamii Kitanzini mjini hapa ,Mwakalebela  alisema  kuwa  amefurahishwa na idadi kubwa ya  wanawake wapatao  zaidi ya 400 ambao  wamejitokea  kutaka  mikopo hiyo  japo  wapo  baadhi ya  watu  wanaweza  kutumia njia  hiyo kwa  ajili ya kujipatia fedha kijanja .

" Neema kama  hizi zinapojitokeza  wapo  baadhi ya  watu wasio na malengo mazuri ambao  wamekuwa  wakitaka  kujinufaisha kwa  kuwachangisha   fedha  wajasiliama mali  hao  ili kupata mikopo .....hivyo  wanawake  wote na wajasiliamali  wanapaswa  kuwa makini wasikubali  kutoa  pesa  yoyote kwa ajili ya mikopo ya TBW "

Mwakalebela  alisifu  utaratibu wa benki  hiyo ya wanawake Tanzania  kuwa haumtaki mwomboji wa mkopo  kuchangia  fedha  yoyote  zaidi ya  kufungua akaunti ya kikundi kwa kiasi cha Tsh 10,000 pekee kabla ya  kukopeshwa mkopo husika.

Hata  hivyo  Mwakalebela kama mdhamini mkuu wa mafunzo hayo  mkoani Iringa  alisema  kuwa amevutiwa  zaidi na mwitikio mkubwa wa  wajasiliama mali  kujitokeza  kushiriki mafunzo hayo tofauti na mikoa mingine ambayo benki  hiyo  imepata  kupita na kuwawezesha  wajasiliamali kama  hao.

Alisema kwa upande  wake  amepata  kuzunguka maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa hasa  yale ya pembezoni na kuwahamasisha  wajasiliamali kujitokeza   kujiunga na vikundi ili  kunufaika na  mikopo  hiyo kupitia benki hiyo ya  wanawake Tanzania.

Pia  alisema  kuwa hadi sasa  tayari  ofisi ya TBW  imefunguliwa katika jengo la benki ya Posta mjini Iringa  ili  kuwawezesha  wananchi  wenye shauku ya maendeleo kuweza  kufika  kujiunga na benki  hiyo na kupewa mikopo.

Mwakalebela  alisema  kuwa  kwa  wale ambao  walianza kupewa mafunzo mapema  zaidi wataanza kupokea  mikopo  yao  wakati  wotote  ndani ya mwezi huu .

No comments: