Saturday, March 8, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI UPIMAJI WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA AKINA MAMA HAPA NCHINI.

 Mamia ya akina mama na wananchi wa Jiji la Mwanza wakishiriki katika sherehe ya uzinduzi  wa upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Nyamagana ambapo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo 

 Ngoma ya asili ya kabila la Wasukuma ya Bugobogobo ikichezwa kwa umahiri mkubwa hata kumfanya Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hiyo kushuka jukwaani na kuicheza na baadaye kumzawadia  mtoto wa kikundi hicho kutoka Mji wa Magu wakati wa sherehe za uzinduzi wa upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizindua rasmi upimaji wa saratani ya  mlango wa kizazi wakati wa kilele cha siku ya wanawake duniani katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana huko Mwanza
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi aliwakabidhi Waganga wakuu wa mikoa ya Mwanza, Iringa, Mbeya na Mara vifaa  vya kupima saratani hiyo. Pichani Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Valentino Bangi mkoba wenye vifaa vya upimaji.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa Dkt. Nestory Masalu kutoka hospitali ya Rufaa ya Bugando ambaye alikuwa akiwapima akina mama katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani  ya mlango wa kizazi katika uwanja wa Nyamagana na kutembelea kituo hicho ambapo wanawake wengi walijitokeza kwa ajili ya kupima.
 Mamia ya wanawake wa Mwanza walijitokeza kwenda kupima saratani ya mlango wa kizazi kama wanavyoonekana katika picha iliyopigwa katika kituo cha Afya cha Buzuruga huko Ilemela.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzaia, MEWATA, Dkt. Serafina Mkuwa (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa Mwanza Ndugu Magalula Said Magalula, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Profesa  Charles Mapinge na Mama Salma Kikwete wakiteta jambo wakati walipokitembelea kituo cha afya cha Buzuruga ambacho hutoa huduma ya kupima saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama 
 Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanawake na wananchi waliokusanyika katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko wilayani Ilemela, Mkoani  Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya kizazi kwa akina mama leo. 

  Mke wa Rais na Mweyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wanawake na wananchi waliokusanyika katika kituo cha Afya cha Buzuruga kilichoko wilayani Ilemela, Mkoani  Mwanza mara baada ya kuzindua rasmi upimaji wa saratani ya kizazi kwa akina mama leo. Picha zote na John Lukuwi

No comments: