Friday, May 11, 2012

WASHABIKI WA YANGA WACHACHAMAA KUTAKA UONGOZI WA JUU KUJIUZURU

 Baadhi ya Wanachama na Wakereketwa wa Timu ya Yanga ya Jijini Dar,wakiongea na Waandishi wa habari waliofika kwenye Makao Makuu ya Klabu ya Timu hiyo,Mtaa wa Twiga na Jangwani leo.Wapenzi hao wa Timu hiyo ya Soka walifika Klabuni hapo wakidai kuwa wanataka Mwenyekiti wa Yanga,Lyod Nchunga aachie ngazi kwani hana Maslahi na timu hiyo,huku wengine wakikataa kuachia ngazi kwa kiongozi huyo.hali iliyopelekea mpaka askari wa Jeshi la Polisi kufika Klabuni hapo kwa kuhakikisha usalama unapatikana na hakuna madhara yeyote yatakayotokea.
 Kila Mwanayanga aliefika klabuni hapo alikuwa na jazba na uongozi wa juu.huyu nae alikuwa akimlalamikia Nchunga kuwa ndie aliesababisha timu yao kupata kichapo cha bao 5-0 dhidi ya watani wao Simba.
 Afande akiwaamuru wanayanga hao kuondoka klabuni hapo,lakini walikuwa wakiikaidi amri hiyo.
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Klabu ya Yanga, Bakili Makele akiongea na waandishi wa habari.
Bibi huyu alietambulika kwa jina la Bi. Mariam nae ni mkereketwa kweli kweli wa Yanga,nae alikuwa akisema kuwa anamuomba Lyoid Nchunga aachie ngazi kwani anawaharibia timu yao.
Kina Ras Makuna wakiongea na wakereketwa hao kwa upole kabisa.
Wazee wa Yanga hapa wamenuna ni Balaa,yaani wanatamani hata Nchunga awaambia haya timu yenu hii chukueni.
Mabishano ya hapa na pale.
WanaYanga hawataki kusikia lolote zaidi ya Kuondoka kwa Nchunga.
Afande akirudia tena kuwaomba wanaYanga hao kuondoka kwenye eneo hilo.
Sasa ni Mshike Mshike...
Ras Makunja kawa uso wa Mbuzi,anaetaka kibano na asogee hapa: wanaYanga wote kuleeeee...
Kina Ras Makunja wako kamili gado kwa lolote,maana jamaa waliombwa waondoke lakini wakaweka mgomo.

No comments: