Monday, December 12, 2011

Mh Mbowe azindua taasisi ya Kusimamia Mpango wa Maendeleo ya Wilaya ya Hai ( HAKIDI)

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Hai,mh Freeman Mbowe akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Taasisi ya Kusimamia Mpango wa Maendeleo ya Wilaya ya Hai ( HAKIDI).
Mbunge wa jimbo la Hai mh Freeman Mbowe akiongoza wabunge wenzake Leticia Nyerere mbunge wa viti maalum Mwanza na Joseph Mbilinyi ,mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kupandisha bendera katika ofisi ya taasisi ya kusimamia mpango wa maendeleo ya wilaya ya Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai mh Freeman Mbowe akimwagia maji moja kati ya miti 2000 iliyooteshwa katika jimbo hilo.
Vifaa vya kuhifadhia uchafu vikiwa nje ya ofisi ya taasisi ya kusimamia mpango wa maendeleo ya wilaya ya Hai.Vifaa hivyo pamoja na trekta lenye tela limetolewa na Mh Mbowe kwa ajili ya kukusanyia taka katika
jimbo hilo.
Mbunge wa viti maalum Mwanza Mh Leticia Nyerere akiotesha mti.
Mbunge wa Mbeya mjini Mh Joseph Mbilinyi akiotesha mti.
Dk Lilian Mbowe akiotesha mti.
Meya wa manispaa ya Moshi ,Mstahiki Jafary Michael akiweka udongo katika mti aliootesha katika jimbo la Hai.
Mh Freeman Mbowe akitoa maelekezo kwa dereva wa gari lililokuwa likisambaza miti iliyooteshwa katika jimbo hilo.
Mh Selasini akiwa amebeba reki kwa ajili ya kufanya usafi katika jimbo la Hai.
Mh Susan Lyimo na mh Leticia Nyerere wakifanya usafi katika dampo la Green Belt.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi akifanya usafi katika dampo la Green Belt.
Mh. Mbowe akiwaelekeza wananchi waliofika kusaidia kufanya usafi eneo la kuokota taka kwa ajili ya kuchomwa.
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini,Mh. Joseph Mbilinyi pamoja na mbunge wa jimbo la Rombo,Mh. Joseph Selasini wakiwa wameshikilia vifaa vya kufanyia usafi tayari kwa ajili ya kufanya usafi katika jimbo la Hai.
Waheshimiwa wabunge wa majimbo mbalimbali wakiwemo wa viti maalumu wakijiandaa kusaidia kufanya usafi katika jimbo la Hai ambalo linaongozwa na Mh. Freeman Mbowe.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

No comments: