Thursday, August 31, 2017

HUKUMU YA UCHAGUZI KENYA KUTOLEWA KESHO IJUMAA

Na   Bashir   Yakub.

1. WAHUSIKA
Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza.
Walalamikiwa(respondents) ni watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai Kenyatta.

Pia kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama.

Wa tatu  na  nne  ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa wagombea urais.

2. MUDA WA KESI.

Kwa katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea siku matokeo yalipotangazwa. Na mahakama inazo siku 14 tu za kusikiliza na kutoa hukumu tokea siku shauri lilipofunguliwa.

Kesi  hii  imekuwa  ikisikilizwa  mpaka  usiku  saa  tano  zikiwemo  siku  za  jumamosi  na  jumapili  ili  kuendana na  muda wa  katiba.

3. MAHAKAMA NA MAJAJI.
Mahakama inayosikiliza ni mahakama ya juu( the supreme court).
Majaji wanaosikiliza ni 7 wakiomgozwa na Jaji mkuu David Maraga na naibu wake mwanamama Philomena Mwilu. Wengine ni Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim, Njoki Ndung'u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.

4.  HOJA ZA MSINGI ZINAZOBISHANIWA.

(a)ODINGA : Hawa wanasema walishinda uchaguzi matokeo yakabadilishwa.
UHURU: Hawa wanasema matokeo yaliyotolewa yalikuwa halisi.

(b)ODINGA: Hawa wanasema mapungufu yaliyojitokeza yanatosha kubatilisha. uchaguzi.
UHURU: Hawa wanasema ili mapungufu yabatilishe uchaguzi ni lazima mapungufu hayo yawe yameathiri moja kwa moja namba/idadi ya kura.

(c) ODINGA: Hawa wanasema server ya tume huru ikaguliwe kwa kuwa ilitumika kubadili matokeo.
UHURU: Hawa wanasema haiwezi kukaguliwa kwa kuwa ina code za siri ambazo zikijulikana zitaathiri chaguzi zijazo na usalama wa taifa.

(d)ODINGA : Hawa wanasema fomu nyingi za kukusanyia matokeo 34a, 34b na 34c hazikutumwa kwa njia ya umeme kama inavyotakiwa na hivyo kuwa batili.
UHURU : Hawa wanasema sheria inasema njia ya umeme ikishindwa itumike manual hivyo baadhi ya maeneo njia hii ilifail na ikatumika manual.

(e)ODINGA : Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe ni Kulinganisha kinachowezekana zaidi(balance of probabilities) kwakuwa hili ni shauri la madai kama madai mengine.
UHURU: Hawa wanasema kiwango cha kuthibitisha kiwe "Pasi na Shaka" (beyond reasonable doubt).

(f) ODINGA: Hawa wanasema kuna matokeo yalianza kuingia sa 11 hata kabla vituo havijafungwa.
UHURU: Hawa wanasema kuna vituo vilikuwa na wapiga kura 20 au 50 hivyo wapiga kura waliisha, wakafunga mapema wakahesabu na kutuma.

(g) ODINGA: Hawa wanasema baadhi ya fomu hazikusainiwa na kuwa na mihuri ya wasimamizi.
UHURU: Hawa wanasema uzembe wa wasimamizi hauwezi kufuta matakwa ya mpiga kura aliyesimama juani siku nzima.

(h) ODINGA:Hawa wanasema mwenyekiti alimtangaza mshindi hata kabla ya fomu zote kufika kutoka mashinani.
UHURU: Hawa wanasema aliona hata akizisubiri haziwezi tena kubadili matokeo.
nk, nk, nk.

5. HUKUMU.

Hukumu itabeba jambo moja kati ya mawili. Ni kukubali ushindi wa Uhuru au kuubatilisha. Ikiubatilisha haitasema sasa Raila ndiye rais bali itaamrisha uchaguzi wa rais kurudiwa.
Katiba inasema uchaguzi utarudiwa ndani ya siku 60 tokea siku ya hukumu.

6. ATHARI ZA HUKUMU.

Hukumu itaathiri kesi zote za uchaguzi wa wabunge , seneta nk. zilizofunguliwa nchi nzima.
Kanuni zitakazochorwa na mahakama hiyo(jurisprudence) ndizo zitazotumika katika mahakama zote za chini kutoa maamuzi yake.
Kwahiyo ni hukumu yenye athari kubwa sana na inayosubiriwa kwa hamu na gamu.

NI kesho ijumaa tusubiri tuone.
+255784482959.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA WASASA NA WASTAAFU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika chumba cha mkutano kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha  viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na  viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu wakisimama kwa heshima kuomboleza msiba wa baba wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali  George Waitara wakati  alipokutana nao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na wakuu wastaafu wa Jeshi hilo Jenerali Mirisho Sarakikya (wa pili kushoto), Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) na Jenerali  Robert Mboma (wa pili kulia) alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Mirisho Sarakikya alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu Jenerali Robert Mboma alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro pamoja na IGP wastafu Omari Mahita, Saidi Mwem na Ernest Mangu alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omari Mahita alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Saidi Mwema alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Ernest Mangu alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali  wa Jeshi la Magereza Dkt Juma Malewa (kushoto) pamoja na Wakuu wa jeshi hilo wastaafu Simon Mwanguku (wa pili kushoto), Nicas Banzi (wa tatu kulia) Augostino Nanyaro na  John Casmir Minja (kulia) alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Mstaafu Simon Mwanguku alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Mstaafu Nicas Banzi alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Mstaafu Augostino Nanyaro alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Mstaafu John Casmir Minja alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt.  Modestus Kapilimba (kushoto) pamoja na Wakurugenzi Wakuu wastaafu Cornel Apson (wa pili kushoto) na Kulia Rashid Othman alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa mstaafu Cornel Apson  alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt. Modestus Kapilimba  alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa mstaafu Rashid Othman  alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt Anna Peter Makakala (kushoto) na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mstaafu Kinemo Kihomano alipokutana na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) na Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi hilo Mhandisi Pius Nyambacha alipokutana na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Kamishna Jenerali mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  Mhandisi Pius Nyambacha alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Kamishna jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omari Mahita alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa mstaafu Cornel Apson  alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Saidi Mwema akibadilishana mawazo wa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wakuu wa Jeshi la Polisi wastaafu Saidi Mwema na Omari Mahita alipokutana na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Saidi Mwema akiongea na wanahabari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi baada ya kukutana na  viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017. Picha zote na  IKULU

MABADILIKO YA UNAHODHA KATIKA TIMU NI JAMBO LA KAWAIDA

Na. Honorius Mpangala.

Ilikuwa ni katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi Lipuli nilipomwona Asante kwasi akiwa amevaa 'usinga' wa nahodha. Pale pale kuna vitu vikaanza kunifikirisha nikijaribu kurejea kwenye kauli za wadau na wapenzi wa soka letu.


 Kauli ambazo zinifanya akili izame huko ni katika kumbukumbu ya maneno yaliyotolewa baada ya benchi la ufundi la Simba kunadili uongozi wa wachezaji. Maneno yalikuwa dhidi ya John Rafael Bocco kupewa unahodha msaidizi nyuma ya Method Mwanjale na Mohammed Hussein. Ilikuwa katika kambi ya klabu ya Simba nchini Afrika kusini ambapo benchi la ufundi liliamua kubadili uongozi wa wachezaji. 

Mabadiliko yalifanya Method Mwanjale kuwa nahodha badala ya Jonas Gerrard Mkude na kupewa wasaidizi wake .Katika orodha ya wasaidizi ilikuwa jina la John Rafael Bocco ndilo lililowafanya wapenzi na wadau walitolee hoja tofauti.

 Maswali yalikuwa kwanini Bocco na sio Kazimoto au wengine waliokuwepo klabuni hapo Kwa muda mrefu. Ilichukuliwa kama ni kitu cha kushangaza sana katika tukio lile. Sababu kubwa ilikuwa kutokana na Kuvuliwa unahodha huo mchezaji mwandamizi wa klabu Jonas Gerrard Mkude.

 Lakini moja ya mambo yaliyo nifurahisha ni pale Mkude alipoongea kuwa hata yeye alipopewa kuna mchezaji alivuliwa hivyo amechukulia kawaida kwake. Tukio la mabadiliko ya kiuongozi sio geni Kwa wachezaji wanaojitambua. Hapa kwetu ilionekana tofauti sana kimapokeo. Wako waliofikiria mbali zaidi na kutaka kuuaminisha umma kuwa ni maajabu ya dunia.

 Hii ni kutokana na kutokuwa wafuatiliaji wa karibu wa mambo yanayoendelea katika vilabu vidogo nchini au nje ya nchi. Wakati watu walikichukulia suala la unahodha wa Bocco kama ni maajabu walisahau kama Yusuph Ndikumana wa Mbao aliposainiwa na klabu akapewa na unahodha.

 Ilikuwa ni maamuzi ya benchi la ufundi likiongozwa na Etienne Ndayigiragije kama kocha mkuu. Iliwahi tokea wakati Klabu ya Mbeya City imesainisha Juma Nyosso. Alipewa unahodha na kumfanya Hassan Mwasapili kuwa msaidizi wake. Sasa katika msimu huu ilikuwa ajabu Kwa Bocco ila Kwa Asante kwasi imeonekana kawaida.

 Hapo ndipo unapopata jawabu la kuteswa na ushabiki wa Simba na Yanga. Kila upande huona wafanyacho wenzao kina walakini. Mara baada ya kutambulishwa kama mchezaji wao,klabu ya Aston Villa ikamtangaza John Terry kuwa nahodha wao. Na hakuna aliyetilia shaka na maisha yameendelea. Ilikuwa pia Mara tu baada ya kusainishwa na klabu ya West Bromwich Albion,Darren Fletcher alipewa unahodha katika klabu hiyo.

 Wako wachezaji ambao ukiwa nao katika klabu wanakuwa na nyota pia wanakua na hali ya kiuongozi. Unapompa Unahodha Nyosso au Kwasi maanake unamfanya awaongoze wenzake kucheza kama yeye anavyocheza Kwa kujitoa. Hadi kufikia hatua mtu anapewa unahodha manake benchi la ufundi limepima mambo mengi ya faida toka Kwa mchezaji husika. 

Uongozi ni karama ili uongoze unahitaji kuwa na ari na mvuto wa kiuongozi Kwa wenzako. Nani anaweza kutia shaka juu ya Asante Kwasi. Ifike wakati tusijone kama sisi kila siku tunaosea kutokana na kutokufanya kama akina Fulani. 

Tunapaswa kuonyesha kile tunachokiamini na sio kuiga ili kuwafurahisha watu wengine. Kuwafurahisha watu ni kama kumchukua mchezaji kipenzi cha mashabiki na kumpa unahodha kitu ambacho pengine kikawa tofauti na matarajio ya wengi na kuonekana hajui kuongoza. 

Nafasi ya unahodha ni kubwa unahitaji watu wenye mvuto Kwa wachezaji wenzao na sio mashabiki. Unaweza kupendwa na mashabiki lakini ukawa huna ushawishi Kwa wenzako mkiwa vyumba vya kubadilishia nguo. Kiuongozi siku zote anakuwa mtu wa mfano katika kutenda na sio anasukumwa kutenda.

 Licha ya kuwa na kipaji kikubwa cha kucheza soka lakini Ronaldinho Gaucho hakuwahi kuwa nahodha Barcelona na hata Brazil. Akili ya kumchagua mchezaji kuwa kiuongozi hakumaanishi una kiwango bora kuliko wenzako hapana ila una muono mkubwa wa kiuongozi katika mpira Kwa wachezaji wenzako. Unahodha kwasi hautii shaka Kwa watu kwasababu ni lipuli au ilivyowahi kutotia shaka ule wa Nyosso na Mbeya city. 

Ukitaka kuona unahodha unajadiliwa na kuonekana ni kitengo nyeti Kwa watu maalumu usikie kuwa Yanga wamemteua Youthe Rostand kuwa nahodha. Mashabiki wao watakuja na hoja ya kutaka kujua kigezo kilichotumika kupewa unahodha. Wakati wale wapinzani wao watakuwa wanaona kama ajabu sana jambo hilo kutokea. Hivyo usishangae kusikia ikasemekana kuwa ni rekodi ya dunia. 

Hii ni kwasababu tu ya fikra za wengi kuishia katika kufuatilia soka na wachezaji wa Simba na Yanga. Kocha wa Lipuli Seleman Matola alitazama mengi toka Kwa mtangulizi wa Asante. Wakati wakiwa daraja la kwanza walikuwa na nahodha Ramadhani Kudunda na baadae Salumu Machaku ambaye hadi timu inapanda ligi kuu yeye ndo alikuwa nahodha. 

Lakini unapokuwa na mtu wa aina ya Asante Kwasi lazima umtumie vyema Kwa manufa ya klabu. Binafsi sikuona maajabu kama wakivyosema baadhi ya wadau kwasababu ya rejea zilizokuwepo juu ya nafasi ya Nahodha Kwa vilabu vingi duniani.

 Hivyo suala la Bocco haikuwa 'story' kama ilivyochukuliwa. Hii ni kama ilivyotokea Kwa Ndikumana,Terry,Nyosso,Fletcher na wengine ambao waliwasili katika klabu na kupata unahodha kama ilivyo Kwa Kwasi. Ifike wakati tuache weledi utumike vyema katika kujadili au kutolea ufafanuzi mambo yanayohusu utaalamu Fulani.

Tusizidiwe na maarifa kwasababu ya mapenzi na tukashindwa kung'amua Yale yanayohitaji akili.

WASANII NGULI NCHINI KUPIMANA MABAVU DIMBA CONCERT TRAVELNTINE MAGOMENI

 Meneja Tukio wa Tamasha la Dimba Concert , Mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamasha litakalo wakutanisha Wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini na bendi ya Msondo Ngoma katika ukumbi wa Traventine September 2 mwaka huu kwa kiingilio cha shilingi 10,000 na 20,000 kwa VIP.
 Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Tamasha la Dimba Concert , Jimmy Chika akifafnua namna bendi hizo zitkavyotoa burudani kwa mashabiki na wadau wa Muziki wa dansi watakaofika katika ukumbi wa traventine siku ya Jumamosi
 Msanii wa Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Husein Jumbe akiwatoa hofu Mashabiki wake kuwa muziki wao bado upo juu
 Mwanamuziki wa Mkongwe wa Double M Sound ,  Mwinyjuma Muumini akijigamba kwa tambo kuwa siku hiyo patachimbika kwa hiyo mashabiki wote wasikose kuhudhuria Tamasha hilo
 Mpiga gitaa la solo wa siku nyingi , Adolf Mbinga akionesha namna atakavyocharaza nyuzi siku ya Tamasha la Dimba Concert siku ya jumamosi
 Mwanamuziki Juma Kakere akieleza namna watakavyoweza kukonga nyoyo za Mashabiki kupitia nyimbo zake kadhaa ambazo ziliweza kutamba
 Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akieleza namna atakavyoweza kutoa burudani kwa wadau wa muziki wa Dansi na Mashabiki watakaofika siku hiyo
 Wanamuziki wakongwe wakiwa katika mazoezi yao wakionyesha namna watakavyoimba siku ya Dimba Concert  siku ya Jumamosi
 Rais wa Vijana wa Muziki wa Dansi nchini , Nyoshi Elsadat akiimba mbele ya waandishi wa habari namna atakavyofanya siku ya Dimba Concert itakayofanyika Sept 2 mwka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni

Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

Wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini wametambiana kuoneshana uwezo wa kuimba siku ya Tamasha la Dimba Concert litakalofanyika katika ukumbi wa Traventine Magomeni Septemba 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja tukio tamasha la  Dimba Concert,Mwani Nyangasa amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa  Taifa muziki bendi kupambana na wanamuziki nguli wa Bendi ya Msondo ngoma.

“ Dhumuni la tamasha hili ni  kuendeleza muziki wa dansi hapa  nchini  kwa kutumia wasanii hawa wakongwe ili waweze kuonesha vijana,wapenzi na wadau kuwa muziki huu bado upo hai.” Amesema  Nyangasa.

 Nae msanii nguli nchini Hussen Jumbe ametanabaisha kuwa wadau na mashabiki wa muziki huo wafike kwa wingi siku hiyo pale Traveltine  septemba 2 mwaka huu ili kupata radha halisi ya muziki wa dansi.

Kwa upande wake  raisi wa vijana  sauti ya simba Nyoshi El Saadat, amewaomba mashabiki wa muziki huo kufika  kwenye tamasha hilo  na kuwaahidi kutowaangusha na kuwapa burudani ya kukata na shoka.

SERIKALI YATUMIA BILIONI 85 KUPELEKA MAWASILIANO VIJIJINI

Serikali imesema kuwa imetumia shilingi Bilioni 85 kupeleka mawasiliano vijijini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuzipatia ruzuku kampuni za simu za mkononi ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenye Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu mjini Dodoma.

“Mfuko huu unaendelea kuhakikisha kuwa mawasiliano bora yanafika katika maeneo mengi nchini hususan vijijini na kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara ambapo Takwimu zinabainisha kuwa, tayari mawasiliano   yamefikishwa kwenye kata 443, vijiji 1,939  kuanzia mwezi Machi 2013 hadi Julai mwaka huu”, amefafanua Naibu Waziri Ngonyani.

Ameongeza kuwa tayari Mfuko umetiliana saini mkataba na kampuni za simu za mkononi mwezi Agosti mwaka huu kuhakikisha kuwa zinapeleka mawasiliano kwenye kata nyingine 75 na vijiji 154.

Aidha, ametanabaisha kuwa hadi hivi sasa asilimia 94 ya wananchi wanapata huduma ya mawasiliano nchini na kuongeza kuwa, Serikali kupitia mkataba wake na Kampuni ya Simu ya Halotel imefikisha mawasiliano kwenye jumla ya vijiji 3,069 kati ya vijiji 4,000 tangu walipoanza utekelezaji wa jukumu hilo mwezi Novemba, 2015 na wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso, amezitaka kampuni za simu za mkononi zinazopeleka mawasiliano vijijini na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ambazo zinapatiwa ruzuku na Serikali kuhakikisha kuwa zinatoa taarifa sahihi kwa Mfuko huo ikiwemo hatua zilizofikiwa za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji husika.

 Amewataka UCSAF kujitangaza na kuweka mabango yao kwenye minara yote nchini iliyojengwa kupitia ruzuku ya Serikali ili kuwawezesha wananchi kutambua uwajibikaji wa Serikali katika kufikisha mawasiliano kwa wananchi wake.

Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete, amesema kuwa Wizara kupitia UCSAF itahakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na mawasiliano kuendana na jukumu la msingi la Mfuko huo la kufikisha mawasiliano kwa wote.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Eng. Peter Ulanga, amewahakakikishia wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuwa Taasisi yake itashirikiana na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakiki kazi zilizofanywa na kampuni za simu za mkononi za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji mbalimbali nchini.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo katika kikao na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Kakoso na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo Eng. Angelina Madete. 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu miradi ya maendeleo ya mawasiliano vijijini katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kasoso, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao kilichowakutanisha na uongozi wa Wizara ya  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu maeneo ya vijijini yaliyofikiwa na mawasiliano katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Dua Nkurua na kushoto ni Mhe. Rita Kabati wajumbe wa Kamati hiyo.


MAGAZETI YA ALHAMIS LEO AGOSTI 31,2017