Monday, July 31, 2017

UZINDUZI WA BARAZA LA WAZALISHAJI WAFANYIKA ZANZIBAR.

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Wafanyabishara wa Zanzibar katika Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Katibu wa Baraza la Wazalishaji Zanzibar Madam Cheherezade Chukh akitoa hotuba ya makaribisho katika uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazalishaji Zanzibar Ahmed Yussuf Baalawy akizungumza machache katika uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara  Wenyeviwanda,Kilimo na Utalii (ZNCCIA)Taufiq Tourky akitoa hotuba na kumkaribisha Mgeni Rasmi katika  Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja .
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika  uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace Malindi mjini Unguja.
Mgeni Rasmi Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Baraza la Wazalishaji lililofanyika katika Hoteli ya Grand Palace  Malindi mjini Unguja.

PICHA NA-YUSSUF SIMAI ALI/MAELEZO ZANZIBAR.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AHIMIZA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI NA TARATIBU KATIKA UTENDAJI KAZI.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw. Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
  Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
 Watendaji kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(hayupo pichani) katika  ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.   
 Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017. Picha na Erasto Ching’oro WAMJW


Na Erasto Ching’oro WAMJW.

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika kuendesha vyuo wanavyovisimamia.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao  kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na  kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka hoja za ukaguzi wa fedha.

Amesisitiza kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika kutimiza majukumu yao.

“Niwatake Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.

Aidha, Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa katika uendeshaji wa vyuo.

Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha, Mabughai, Monduli na Mlale.

UNCDF YAWEZESHA UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA BWAWA LA KALEMAWE



SERIKALI ya Tanzania, imeshukuru Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kuwezesha watanzania kupambana na umaskini kupitia miradi wanayoidhamini au kuitafutia fedha. Kwa miongo miwili UNCDF imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) katika mpango wa kupeleka madaraka kwa umma na shughuli za maendeleo ya kiuchumi . 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Mussa Iyombe katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Aisha Amour kwenye ufunguzi wa kongamano la siku 2 la Wadau wa Ufugaji Samaki Kibiashara Bwawa la Kalemawe lililoko wilaya ya Same mwishoni mwa wiki.

“Tunafurahishwa kwa namna ya pekee na UNCDF kwa jitihada zake zinazoendeshwa kupitia katika Mpango wa Ufadhili Miradi ya kiuchumi (LFI),” alisema Iyombe na kuongeza: “Tunapokutana hapa tunapewa fursa na kufunuliwa uzoefu wa ushiriki wa UNCDF katika miradi mbalimbali, safari hii tukishuhudia hatua yake ya kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro.” Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ufugaji samaki katika shamba hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mh. Naghenjwa Kaboyoka na Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (wa pili kulia).

 Pamoja na kushukuru kwa hatua mbalimbali zilizofikiwa na taasisi hiyo katika kusaidia watanzania, aliwataka wakazi wa Same kuhakikisha kwamba mradi huo ulioundiwa kampuni ili kwenda kibiashara unafanikiwa na kuwa mfano kwa wengine. Halmashauri ya wilaya ya Same, na jamii inayozunguka bwawa la Kalemawe wanashirikiana na UNCDF kuboresha miundo mbinu ya bwawa hilo na kuwezesha uwapo wa uwekezaji kwa kuanzisha kampuni. 

Kampuni hiyo iliyosajiliwa ya Kalemawe Dam Investment Limited katika mpango maalum (SPV) inamilikiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Same, halmashauri ya vijiji sita, wakala wa serikali, watu binafsi pamoja na makundi ya kijamii. Kuwapo kwa kampuni hiyo ni juhudi zinazofanywa za kuwezesha uhusiano mahsusi wa kibiashara unaohusisha ubia wa Serikali, Binafsi na jamii (PPCP) kwa kutoa umiliki linganifu mpaka katika ngazi za chini za mamlaka za kijiji, ambazo kimsingi ndizo wamiliki wa maliasili muhimu ya ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya Mwaka 1999.  Viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) wakiwa kwenye ziara fupi ya mafunzo kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba la ufugaji samaki la Ruvu lililopo wilaya ya Bagamoyo.

Mradi huo wa Ufugaji wa Samaki Kibiashara wa Bwawa la Kalemawe ni zao la ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Same, Kata za Ndungu na Kalemawe, asasi zisizo za kiserikali na wadau wa maendeleo walioazimia kukarabati na kufufua bwawa hilo na mfumo wake wa kilimo cha umwagiliaji. UNCDF kwa kushirikiana na wabia wake waitwao Mikono Tayari (ambao ni kundi linaloundwa na washirika kutoka Tanzania na Norway) ni wataalamu katika mradi hu wa ufugaji samaki kwa pamoja na SPV ya Same na washirika wake. 

Katika kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Same Rosemary Staki amesema wilaya yake ipo tayari kutekeleza mradi huo ambao una manufaa makubwa si tu kwa watu wa Kalemawe na vijiji vinavyozunguka bali pia na halmashauri ya wilaya ya Same.  Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (kulia) akitoa maelezo kuhusu vyakula vinavyotumika kulisha samaki wanaofugwa kwenye shamba hilo kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliofanya ziara fupi ya mafunzo juu ya ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo.

Akishiriki katika mjadala aliwataka wanakalemawe kutambua umuhimu wa mradi huo na kwamba hicho ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa watu binafsi na jamii kwa ujumla. Mradi huo ambao ni sehemu ya programu kubwa ya kubadili watu wenye makazi kuzunguka bwawa hilo umelenga katika siku za usoni kuzalisha samaki na vifaranga vyake. 

Ili kuwa na uelewa mkubwa wa kufanya biashara hiyo ya samaki, madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa za vijiji vinavyotengeneza kampuni hiyo ya Kalemawe walitembelea shamba la samaki Ruvu ambapo waliona shughuli mbalimbali zinazoendelea katika shamba hilo ili iwe mfano kwao Pamoja na kuuza samaki shamba hilo ambalo lipo kilomita 20 kutoka Bagamoyo na kilomita 13 hivi kutoka Mlandizi linafuga samaki aina ya sato na hutotolesha vifaranga laki moja kila wiki kwa kulingana na oda zilizopo.  Ziara ya mafunzo ikiendelea katika shamba la kufuga samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo. Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (wa pili kushoto) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (katikati) pamoja na ujumbe ulioambatana nao kwenye mafunzo hayo ukitazama jambo katika shamba hilo.

Mmoja wa viongozi katika mradi huo Khumbo Kanthenga alisema kwamba mradi huo ambao bado unapanuliwa kufikia mabwawa sitini kwa sasa umelenga kutoa vifaranga kwa mujibu wa oda na pia kuuza samaki ambao wapo tayari kuingia sokoni samaki hao wanafikia gramu 350 na kuendelea. Naye Mbunge wa Same Mashariki, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alikuwapo katika kongamano hilo alielezea haja ya wananchi wengi kutambua mipaka yao na kuhakikisha kwamba dhamira safi iliyopo ya kufufua bwawa hilo na kubadilisha maisha ya wananchi inafikiwa. 

Wakifunga Kongamano hilo UNCDF ili shukuru ushirikiano mkubwa wa karibu ambao umeonyeshwa na washiriki wa warsha hii ya wadau kuanzia serikali kuu, mkoa, willaya na viongozi wa vijiji sita vinavyohusika na utekelezaji wa mradi na pia iliahidi kua mashirika mengine ya umoja wa mataifa watashirikishwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu na miradi mingine mbalimbali katika eneo hili la bwawa la samaki.  Eneo ambalo linaandaliwa kwa ajili ya bwawa la kufugia samaki katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamayo. Wafanyakazi wa shamba la kufugia samaki la Ruvu wakitega nyavu kwa ajili ya kuonyesha samaki katika moja ya mabwawa kwenye shamba hilo wakati wa ziara hiyo fupi ya mafunzo. Mmoja wa wafanyakazi wa shamba hilo akiwa ameshikilia samaki aina Sato wanaofugwa kwenye shamba hilo. Meneja wa Shamba la Samaki la Ruvu, Khambo Kanthenga (tisheti nyekundu) akitoa maelezo katika chumba maalum cha kutotolea vifaranga vya samaki kwa viongozi mbalimbali wa Serikali wa wilaya ya Same na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) waliokuwa kwenye ziara fupi ya kupata elimu juu ufugaji wa samaki kibiashara katika shamba hilo lililopo wilaya ya Bagamoyo. Mshauri wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede akitazama mabwawa ya samaki katika shamba la kufugia samaki la Ruvu lililopo wilayani Bagamoyo. Mkurugenzi wa Shamba la Samaki la Ruvu, Daudi Makobole (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki (kulia) pamoja na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF)-Tanzania, Peter Malika (kushoto), Mshauri wa Shamba la Samaki la Ruvu, Per Gjoede (wa pili kushoto) baada ya kuhitimisha ziara fupi ya mafunzo katika shamba hilo. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Peter Malika akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku mbilli ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Staki. Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Staki akitoa salamu kwa wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe wakati wa warsha hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Ofisa Mwandamizi anayeshughulikia uwekezaji katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Imanuel Muro akisimamia majadiliano kuhusu wa kampuni ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji samaki kibiashara katika bwawa hilo iliyoandaliwa na UNCDF na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mkiurugenzi Msaidizi Idara ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dr. Charles Mhina akitoa maoni kwenye warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kijiji cha Misufini kata ya Ngungu wilaya ya Same, Omari Mganga akiwasilisha maoni wakati wa warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kijiji cha Mgandu kata ya Bendera wilaya ya Same, Merina Mhando akichangia maoni katika warsha ya siku mbili ya wadau wa mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mtaalamu wa Mawasiliano na Ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF) nchini, Jacqueline Namfua-Mwombela na Mshirika wa Programu UNCDF, Andulile Mwabulambo wakifurahi jambo wakati wa warsha hiyo iliyofanyika wmishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni washirki wa warsha ya siku mbili ya mradi wa ufugaji wa samaki kibiashara katika bwawa la Kalemawe iliyoandaliwa na UNCDF na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.   Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.

MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA KUONA MAENDELEO YA UFUFUAJI WA KIWANDA CHA MANONGA GENERY

 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akioneshwa moja kamba na mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan zinatokana na zao la pamba katika kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo Wilayani Igunga kata ya Choma. Katikati ni katibu wa kiwanda cha Nyuzi Tabora. ( Picha zote na Raymond Urio ) 
 Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akizugumza na Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati), alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho leo Wilayani Igunga kata ya Choma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Igombensabo Lazaro Ngullo .
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akipewa moja ya maelezo ya mashine ya ya zao la pamba ndani ya kiwanda cha Manonga Genery, leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.
 Mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan akimpa maelekezo Mbunge wa Manonga Seif Khamis Gulamali ndani ya kiwanda hicho (katikati), leo alipotembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda kilichopo Wilaya ya Igunga kata ya Choma.
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Igombensabo.
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akiongozana na viongozi wa serikali pamoja na wahandisi alipotembelea kiwanda hicho leo kilichopo Wilayani Igunga kata ya Choma.
 Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali (katikati) akisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisaliamiana kwa furaha na mmiliki wa kiwanda cha Manonga Genery, Urvesh Rajan leo alipotembelea kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho kilichopo Wilayani Igunga kata Choma.

NA RAYMOND URIO
Mbunge wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulamali leo ametembelea kiwanda cha Manonga Ginery kinachohusika na kutengeneza pamba, kilichokuwa kimesimama kwa takribani miaka ishirini (20) bila ya kufanya.

Mapema leo hii Mbunge Gulamali aliwasili katika eneo la kiwanda hicho, iliyopo Jimbo la Igunga Kata ya Choma akiwa pamoja na Mmiliki wa kiwanda hicho, ndugu Urvesh Rajan pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, wahandisi na mafundi wa viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea na kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi upya, baada ya kukaa kwa miaka kadhaa bila ya kufanya kazi, Mbunge Gulamali alisema, leo nimekuja kuoana maendeleo ya kufufuliwa wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu ya kutaka kutimiza tena ahadi yangu niliyo itoa kwa wanachi wa Igunga na Manonga kwamba lazima kiwanda cha Manonga Ginery, kianze kazi ili wananchi waweze kunufaika katika zao biashara ya pamba na wengine kupata ajira kwa kuendesha maisha na kukuza uchumi wa viwanda nchini.

" Leo nimekuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hichi ikiwa ni sehemu yangu ya ahadi niliyo itoa kwa wananchi wangu wa jimbo la Manonga pamoja na Igunga kwamba lazima kiwanda hiki kifanye kazi tena, ili biashara ya zao la pamba lirudi tena na wananchi na waweze kupata ajira katika kiwanda hichi pia kukuza uchumi wa nchi ya Viwanda.

" Kufufuliwa kwa kiwanda hiki ni fursa kubwa ya maendeleo kwa jamii ya wana Igunga na Manonga na hasa wakulima wa zao la pamba hata kwa wananchi wanao lilia ajira, hivyo fursa kwa sasa iko wazi, alisema Gulamali.

Hata hivyo Mbunge Gulamali alisema kuwa bila kumpa ujumbe mmiliki wa kiwanda hiki na kutompa matakwa ya wananchi basi ingekuwa sicho kilichotokea leo, kwahiyo nimetumia uongozi wangu kwaajili ya wananchi wangu ili kuona maendeleo yakiendelea tena katika swala kiwanda na kuona zao la pamba likirudi tenaa kwa kasi katika Jimbo la Igunga na Manonga.

Lakini pia Mbunge Gulamali amewataka wakulima wa zao la pamba kuanza kulima kwa kasi kilimo cha hicho kwa kuwa sasa kiwanda hiki kitaanza kufanya kazi, hivyo juhudi na jitihada zenu ndio itakayoweza kufanya kiwanda hiki kiendelee kwa kuwa nao wanategemea pamba toka kwenu na wao waweze kuuza kwa wafanya biashara wakubwa wa nje ya mipaka na ndani ya nchi.

Hata hivyo Mmiliki wa kiwanda hicho, ndug, Urvesh Rajan amemshukuru Mbunge Gulamali sambamba na uongozi wa serikali wa kata ya Choma kwa kuweza kuvumilia kwa kipindi chote tangia kiwanda kilivyo simama na hata pale alitoa ombi lake la kukufua tena kiwanda waliweza kumsikilliza na hivyo ni jambo la kushukuru.

Lakini pia mmiliki wa kiwanda hicho ndug, Rajan ametoa ombi kwa wakulima wa zao la pamba kuweza kujitaidi kulima zao hili kwa kasi, kwa kuwa kiwanda kinategmea sana zao hili na si zao jingine, hivyo pesa watakayo ilipa toka kwawakulima wana imani nao itarudi pale watakapo wauzia wafanya biashara na ndio kiwanda kitazidi kuendelea.

" Ninafurahi Mbunge Gulamali ameitikia wito wangu kwa kuja na kuona maendeleo ya kutaka kufufua kiwanda hichi hivyo, ni jambo zuri kuona kiongozi akiwa sambamba na wewe na mwenye kutaka maendeleo,

" haitochukua muda tutaaenda kuanza kazi hivyo nina waomba wakulima wa zao hili kuchangamkia fursa kwenye ulimaji kwa kuwa fedha watapata za kuendesha maisha hata ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu, alisema. Rajan.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha Choma, Ndug, Emmanuel Methew alisema kuwa kitendo kilichofanyika leo cha mbunge kuja kuona maendeleo ya ufufuaji wa kiwanda hiki ni kitu kizuri kutokana ni mikaa mingi kutofanya kazi hivyo wakulima walikuwa wanapata tabu katika zao hili, hata mwishowe kukata tamaa katika kulima zao hili kutokana na kufa kwa kiwanda hiki.

"Kiwanda kufufuliwa tena ni jambo zuri hivyo nina imani kuwa wakulima watarudisha nguvu zao kwa kasi kwenye zao hili la pamba kwakuwa ndio moja ya zao kubwa katika mkoa wa Tabora, alisema Methew.

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JULAI 31,2017