Saturday, October 31, 2015

SAID NA SALMA WALIVYOMEREMETA USIKU WA MAGUFULI

 Bwana Harusi Said akimnywesha Shampein mkewe Salma wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika kwenye Uukumbi wa Best Choice uliopo Tabata jijini Dar es Salaam, jana usiku ambapo wanandoa hao walijiwekea historia ya ndoa yao kwa kusherehekea siku maalum ya utambulisho wa Rais mpya wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli aliyekabidhiwa hati ya utambulisho wa ama cheti cha ushindi kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliomalizika wiki iliyopita.

Aidha wanandoa hao walifunga Ndoa Okt 27 huko Karatu mkoani Arusha.
 Bi Harusi Salma akimlisha Keki mumewe Said ikiwa ni ishara ya upendo.
 Bwana harusi na Bi Harusi,wakimkabidhi keki Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe yao, George John, ikiwa ni sehemu ya kumshukuru kwa kusheresha na kufanikisha sherehe hiyo.
 Mdogo wa Bi harusi akifanya yake ukumbini hapo...
 Bw na Bi Harusi wakiwa katika pozi.... KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

SIMBA YAIKAUSHA MAJIMAJI YA SONGEA 6-1

Mshambuliaji wa Simba, Peter, Mwalyanzi akiwatoba wachezaji wa Majimaji ya Songea katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 6-1. (Picha na Francis Dande)
Wachezaji wa Simba, Hamis Kiiza na Irahim Hajibu wakishangilia kwa pamoja moja ya bao lililofungwa na Hajibu.
Ibrahim Hajibu wa Simba akiifungia timu yake bao la kichwa.
Wachezji wa Majimaji ya Songea baada ya kufungwa.
Hamis Kiiza akimiliki mpira.
Wachezaji wa Majimaji wakilaumiana baada ya kufungwa.
Golikipa wa Majimaji, David Burhan akichuana na Peter Mwalyanzi.
Mwinyi Kazimoto akichuana na beki wa Majimaji.
Mashabiki wa Simba.
Wachezaji wa Simba wakishangilia.
Kocha wa Simba, Dyllan Kerr akishangilia na wachezaji wake.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na kocha wa timu hiyo, Dyllan Kerr.
Furaha ya ushindi..........

Thursday, October 29, 2015

NMB MOSHI WATOA POLE KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB katika matawi ya Nelson Mandela na Mawenzi wakiwasili katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela ,Emanuel Kashusho akizungumza jambo na afisa habari wa hospitali ya rufaa ya KCMC Gabriel Chiseo,(Kulia).
Afisa Uhusiano wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB,matawi ya Moshi mjini waliotembelea hosptalini hapo kutoa zawadi na kuwapa pole wagonjwa.
Wafanyakazi wa NMB Moshi wakimsikiliza afisa habari wa KCMC,Gabriel Chiseo (Hayupo pichani).
Wafanyakazi wa Benki ya NMB matawai ya Moshi wakishusha zawadi tayari kugawa kwa wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya KCMC.
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela,Emanuel Kashusho akizungumza lengo la kufika katika hosptali hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB,wakiwa wamebeba zawadi tayari kugawa kwa wagonjwa waliolazwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Wafanyakazi wa NMB Moshi wakigawa zawadi kwa agonjwa.
Wodi zote katika hosptali hiyo zilifikiwa.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Moshi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya zoezi la kugawa zawadi kwa wagonjwa kumalizika.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.