Friday, February 27, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye sherehe za kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammograph) kwa akinamama katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwenye kitengo cha Uzazi na mtoto kilichopo eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhmu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo tarehe 27.5.2015.

Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki. PICHA NA JOHN LUKUWI

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOA WA MBEYE,LEO YUPO WILAYANI KYELA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkuu wa Zamani wa Mkoa wa Mbeya Mzee John Mwakipesile baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela kwa ziara ya siku moja wilayani humo Februari 26, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee wa Kyela baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya kuaza ziara ya siku moja wilayani humo Februari 26, 2015.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, MizengoPinda wakati aliozungumza baada ya kufungua mashine ya kukoboa nakuchambua mpunga mjini Kyela Februari 26, 2015.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu wa CHADEMA wa kata ya Mwaya, Ageni Pamesa kabla ya kufungau maabra ya shule ya sekondari ya Mwaya akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mbeya Februari 26, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kufungua maabara ya shule ya sekondari Mwaya wilayani Kyela akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 26, 2015. Kushoto ni Mkewe Tunu na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kyela anayeondoka Margareth Malenga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) akitazama mafunzo kwa vitendo wakati alipokagua maabara ya Kemia katika shule ya sekondari ya Mwaya wilayani Kyela Februari 26, 2015.
Daraja la Mwaya wilayani Kyela ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 26, 2015.


Daraja la Mwaya wilaya ni Kyela ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na watalaamu wa kampuni ya kichina ya CHICCO kabla ya kufungua daraja la Mwaya lililojengwa na kampuni hiyo wilayani Kyela Februari 26, 2015.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 26, 2015. Wapili kulia ni mkewe Tunu na wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kyela anayeoondoka, Margareth Malanga.

Hatua za mwisho za Maandalizi Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2015

Maandalizi ya mwisho ya kukarabati maeneo mbalimbali ya uwanja wa Chuo kikuu kutakapofanyika mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathoni.
Mabango mbalimbali yakiwa yamewekwa maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi kuashiria kuanza kwa shamrashamra za mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Baadhi ya wageni wakijiandikisha kukimbia mbio ndefu za kilometa 42 ambapo zoezi la uandikishaji linafanyika katika hotel ya Keys mjini Moshi.
Washiriki wa mbio za Kilometa 21 zinazodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakijiandikisha kwa ajili ya kupata namba maalumu wakati wa kukimbia mbio hizo. 
Baadhi ya wakimbiaji wakijaza fomu kwa ajili ya kukimbia mbio ndefu za km 42.
Wale wa mbio za Km 5 fun run pia walihakikisha wanafanya usajili wa ndugu zao pia.
Katika eneo la kujiadikishia unapata kiburudisho cha Grand Malt mara baada ya kupatiwa namba kwa ajili ya kushiriki mbio hizo.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Embrace e-commerce: Kaymu advises

Today technology is changing Tanzania - the way we work, communicate with each other, educate ourselves, buy goods and services and transfer money are done increasingly through the Internet, bringing convenience to our day-to-day routine How do we ensure Tanzania keeps pace with the global shifts toward e-commerce? What do we need to do to avoid being left far behind in this development? 

First, we should not only accept that technology is changing our way of life, but embrace that an increasing amount of our time in the near future will be spent conducting more business online. E-commerce commonly refers to any business conducted online, using any of a variety of websites and applications that rely on the Internet (such as e-mail, instant web messaging, social media, websites etc. This kind of trading can be between two businesses transmitting funds, goods, services or between a business and a customer.

For example, the online shopping space has become a source for buyers to do product comparisons and find out all the information they would ever want without setting foot in a store – offering buyers the complete satisfaction of a shopping experience without the hassle of visiting a market and window browsing store-by-store. People can now browse virtual marketplaces and online adverts on their favorite websites or even social media pages. 

Kaymu has set an example on how Tanzanians can use e-commerce to improve their businesses. Tanzania’s number 1 online platform offers anyone who joins Kaymu (registration is free) the chance to buy or sell items. For a business – especially local SMEs – this means a very affordable, risk-free opportunity to generate additional revenues and grow a company’s operations.

Mobile networks have introduced mobile wallets where you can pay, save and withdraw money using your mobile phone through different recognized agents. Anyone with a mobile wallet can also transfer money to his/her bank account, buy groceries from elected shops and so forth. This reduces our reliance on carrying sufficient cash everywhere we go (a restriction on some and a safety risk for others), and allows to conduct business or simply lending a friend money over great distances.

On the other hand you can even see event tickets being sold online. Using these same mobile wallets, people can pre-order discounted tickets to their favorite events (like the Nyama Choma Festival) online, from [Kaymu.com] or tiketi.co.tz. This rewards those who plan ahead by helping them save money and avoid long queues at the event. 

The way we sharing and listen to music has also rapidly moved online. In the most recent news, Tigo announce the launch of Tigo Music through a partnership with Deezer, an international music streaming service that will provide Tanzanians with unlimited music experience. A part from giving Tigo customers unlimited access to local and international music local artists are getting an opportunity to earn extra payment from their songs listened to through the service.

This demonstrates how technology can help us improve lives, by saving time and making business much easier and successful, this is a step closer to Tanzania becoming one of the developed countries even though we still has long strides to take.

NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA LEO

Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 


Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.