Friday, September 7, 2018
Thursday, September 6, 2018
KATIBU MKUU UVCCM AWATAMBULISHA WAKUU WA IDARA WAPYA KWA WATUMISHI WA MAKAO MAKUU UVCCM LEO.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) pamoja na wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walipowalisi katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya Makao Makuu UVCCM Upanga Dar Es Salaam
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl.Raymond Mwangwala (MNEC) akizungumza na watumishi wa Makao makuu wakati akiwatambulisha wakuu wa Idara wapya wa Umoja wa Vijana walioteuliwa na Kuthibitishwa na baraza kuu la UVCCM Taifa lililoketi jijini Dodoma wiki iliyopita
Wakuu wa Idara za Makao makuu UVCCM wakifuatilia mazungumzo ya Katibu Mkuu UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha kwa watumishi wa UVCCM makao makuu.
Watumishi wa UVCCM makao makuu wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu wa UVCCM Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) alipokuwa akiwatambulisha wakuu wa idara za UVCCM makao makuu kwao
Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Siasa Ndg Peter Kasela akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg.Hassan Bomboko akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kamana Juma Simba akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu wa Idara ya Uchumi na Uwezeshaji Ndg.Nelson Lusekelo akizungumza na watumishi wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM leo wakati wa kutambulishwa Kwa watumishi wa Makao makuu ya UVCCM
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwakabidhi Mpangokazi wa Utekelezaji wa UVCCM Mwaka 2018/2019
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala (MNEC) akiwaongoza wakuu wa Idara za Makao makuu ya Umoja wa Vijana wakati akiwatembeza maeneo mbali mbali ya Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam
(Picha na FahadiSiraji wa UVCCM)
Wednesday, September 5, 2018
RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAMIA YA WANANCHI WA MUSOMA MKOANI MARA BAADA YA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI HUMO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa Musoma waliokusanyika katika viwanja vya Mukendo vilivyopo Musoma mjini kwa ajili ya kumsikiliza mara baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Musoma mjini katika viwanja vya Mukendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia dawati ambalo alikuwa akilitumia kujisomea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Stephanie Mouen wakanza kulia mwenye wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Musoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa wakisikiliza maelezo ya mradi wa wa maji safi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Musoma mjini Mkoani Mara kabla ya kuuzindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Stephanie Mouen mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD Agence Francaise De Development waliosaidia katika mradi huo wa maji Musoma mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe mara baada ya kufungua barabara ya kutoka Mpakani mwa Simiyu/Mara na Musoma km 85.5.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Musoma mjini (hawaonekani pichani) katika viwanja vya Mukendo Musoma mkoani Mara.
Picha namba 16. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika bweni alilokuwa akilala Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Shule ya Msingi Mwisenge Musoma. Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi kuanzia tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/193. PICHA NA IKULU
Subscribe to:
Posts (Atom)



























































