Tuesday, January 2, 2018

UVCCM YAPONGEZA MIRADI YA AFYA TABORA.


Na Mwandishi wetu,Tabora

Umoja wa Vijana wa CCM umesema umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotokana na ahadi katika ilani ya uchaguzi katika halmshauri za wilaya mji wa Nzega na Nzega vijijini mkoani Tabora. Pia Umoja huo umeeleza kikubwa kasi hiyo inatokana na kuwepo kwa mashirikiano makubwa kati ya viongozi wa chama,halmashauri za wilaya na serikali kuu.

Matamshi hayo yametamkwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM Kheri Denise james mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kazogolo katika halmashauri ya mji wa Nzege .

Kheri alisema kitendo cha serikali ya awamu ya tano kupeleka jumla ya shilingi milioni mia tano toka serikali kuu oktoba mwaka huu kwa ajali ya ujenzi wa kituo hicho ni kielelezo kuwa serikali inajali maisha ya wetu wake .

"UVCCM tumeridhishwa na ujenzi wa miradi ya afya katika halmashauri za mji wa Nzega na halmashauri ya nzega vijijini.Ilani ya uchaguzi ya chama imetekelezwa kwa vitendo. Hii ndiyo tafsiri halisi ya hapa kazi "Alisems Kheir .Aidha alisema kazi ya kuwatumikia wananchi haina mjadala badala yake inamhitaji kila kiongozi dhamana kuwa nafasi yake kuwajibika na kuwatumikia wananchi.

"Kuimarika kwa huduma za jamii na watu kupata huduma bora ndiyo malengo ya kisera yanayotakiwa kufanikishwa. Tuna wajibu kila mmoja kwa nafasi yake kumsaidia Rais na serikali yale "Alisisitiza  Kheri akiwa mkoani Tabora ametembelea mradi mkubwa wa usambazaji maji toka

ziwa Victoria mkoani mwanza kupitia shinyanga hadi Tabora,kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kazogolo na kuzumgumza na wananchi katika halmashsuri ya mji wa nzega na nzega vijiijini.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akipokelewa na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Nzega- mkoa wa Tabora akiwa anaelekea Mwanza kwa ajili ya mapokezi yake baada ya kuchaguliwa na mkutano mkuu wa 9 wa UVCCM kuwa mwenyekiti mpya wa UVCCM 2017-2022.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James wa tatu toka Kushoto akivikwa Skafu mara baada ya kuwasili katika Ofisi za CCM Wilayani Nzega.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akikagua kikundi cha ngoma mara baada ya kupokelewa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akisaini Kitabu cha Mauzulio ya Wageni.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Bi Tabia Maulid Mwita Akizungum,za na Wanachama wa Chaa cha Mapinduzi Wilayani Nzenga.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akizungumza na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wilayani nzega mkoa wa Tabora.
Wanachama Wilayani Nzega Wakimsikiliza
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice Jameswa tatu toka kushoto akizungumza jambo na M..mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shillingi billioni 600 utakaotokea Ziwa Victoria na kunufaisha wananchi wapatao milioni 1.1 wa mikoa ya Shinyanga (vijiji 39) na zaidi Tabora (vijiji 89).


Baadhi ya Vifaa vya Ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shillingi billioni 600 utakaotokea Ziwa Victoria na kunufaisha wananchi wapatao milioni 1.1 wa mikoa ya Shinyanga (vijiji 39) na zaidi Tabora (vijiji 89).
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akitunza fedha katika kikundi cha ngoma ya Asili alipowasili Wilaya ya Nzega Vijijini kuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama.
Viongozi wamsikiliza
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akipata maelezo toka kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nzega Ndugu Amos Kanuda na Mkuu wa wilaya ya Nzega Ndugu Godfrey William Ngupula,alipotembelea kituo cha afya cha Zogolo kilichopo Halmashauri ya mji wa Nzega kinachotegemewa zaidi kuhudumia wananchi wa mji wa Nzega yenye watu wasiopungua laki mmoja. Ujenzi unaolenga kuboresha utoaji wa huduma katika kituo hiki ulikadiriwa kugharimu shillingi milioni 500 ukiwa ni ufadhili wa mfuko wa World Bank.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Kheri Denice James akipokelewa na Wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Shinyanga akitokea Tabora kuelekea mwanza.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI) 

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JANUARY 2,2018

Monday, January 1, 2018

ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA MIFUGO LAONGEZEWA MUDA WA MWEZI MMOJA

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina(wa pili kushoto) akipiga chapa ng’ombe katika hitimisho la zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa katika Kijiji cha Migato, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.

Na Stella Kalinga, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina ameongeza muda wa mwezi mmoja kwa Halmashauri hapa nchini kukamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo na kuwataka watendaji wote wa Serikali wanaohusika kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, zoezi ambalo lilianza rasmi Kitaifa mwezi Desemba, 2016 na kupangwa kukamilika Desemba 31, 2017.

“Kwa kuwa hadi sasa zoezi hili limetekelezwa kwa asilimia 38.5 kutokana na sababu mbalimbali, Mimi Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa Mamlaka niliyopewa chini ya sheria ya Utambuzi, Usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na kanuni yake, ninaongeza muda wa kupiga chapa mifugo kutoka tarehe 01/01/ 2018 hadi 31/01/2018”alisititiza.

Mpina amesema miongoni mwa changamoto zilizopelekea Halmashauri nyingi kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa asilimia 100 ni baadhi ya halmashauri kutokutenga fedha kwa ajili ya zoezi hilo, kubaini mifugo kutoka nje ya nchi, baadhi ya wafugaji kushindwa kutaja idadi halisi ya mifugo yao na baadhi ya Halmashauri kuwatoza wafugaji zaidi ya shilingi 500 ambayo ndiyo bei elekezi, ambapo ameagiza wafugaji hao waliotozwa zaidi ya shilingi 500 warejeshewe fedha zao.

Ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2017 Halmashauri 30 hapa nchini hazijapiga kabisa chapa mifugo, halmashauri 23 zimeendesha zoezi hilo chini ya asilimia 10 na akaongeza kuwa orodha ya majina ya viongozi wa wilaya hizo walioshindwa kutekeleza agizo hilo la Serikali ameyawasilisha kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.

“Halmashauri 30 ambazo hazijapiga chapa kabisa hata ng’ombe mmoja na zile 23 ambazo zimepiga chini ya asilimia 10 majina ya viongozi wote na Halmashauri husika nimekabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, hatuwezi kuendekeza ukaidi wa maagizo ya Viongozi Wakuu wa Nchi” alisema Mpina. Akiwasilisha taarifa ya zoezi la Upigaji Chapa katika Mkoa wa Simiyu, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Elias Kasuka amesema zoezi hilo mkoani humo lilianza rasmi mwezi Aprili 2017 ambapo hadi sasa ng’ombe zaidi ya 764, 933 wameshapigwa chapa kati ya ng’ombe 1,500,000.

Akitoa maoni yake baada ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo, Paulo Mabula mfugaji kutoka Migato Itilima amesema wafugaji wamelipokea kwa furaha agizo la Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuongeza siku za kwa ajili ya kupiga chapa kwani litawasaidia wafugaji ambao bado hawajakamilisha ili kuondokana na changamoto ya wizi wa mifugo.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula amemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina kuwasaidia wafugaji wa Wilaya hiyo na maeneo mengine ya Mkoa huo kufanya vikao vya ujirani mwema na wale wa mikoa jirani ili kujadiliana namna ya kuondoa changamoto ya wizi wa mifugo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi amesema viongozi na wataalam wa wilaya hiyo wamekuwa wakiwahamasisha wafugaji kupanga matumizi bora ya ardhi ili waweze kutenga maeneo kwa ajili ya malisho na kuyawekea miundombinu muhimu kwa ajili ya mifugo ikiwemo maji, majosho pamoja malisho.
Vijana wa Skauti wilaya ya Itilima wakimvisha skafu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina alipowasili wilayani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa, mkoani Simiyu.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisalimiana na Afisa Mifugo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Ally Mzee mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (wa tatu kushoto) akipiga chapa ng’ombe katika hitimisho la zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa katika Kijiji cha Migato, Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu ambalo limehitimishwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Daudi Nyalamu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo leo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani mara baada ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Migato na vijiji jirani mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa lililofanyika kijijini hapo.
Ndg.Paulo Mabula akitoa mchango wake mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina kuhitimisha zoezi la upigaji chapa Kitaifa katika Kijiji cha Migato wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Elias Kasuka mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akipokelewa na Viongozi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo Kitaifa, lililofanyika katika kijiji cha Migato wilayani Itilima.