Monday, August 1, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016, Kushoto ni mkewe Mary. 
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa katika gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea banda la Magereza katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo Agosti 1, 2016, kulia ni Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu wa Gereza la Mtego wa Simba, Oman Msekwa. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (Kulia kwake) wakatazama bwawa la samaki na banda la kufugia bata wakati alipotembelea banda la Magereza katika monyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na mtambo wa kukaushia mboga hizo katika katika maonyesho ya wakulima Nanene nane mjini Morogoro Agosti 1, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kushoto ni mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya Temeke kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali zinazotokana na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea meza ya Bibi Salome Kaiza (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016. Kulia kwake ni Mkewe Mary.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana tikiti maji wakiwa kwenye meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM KUTOA UAMUZI



Na Veronica Simba - GEITA

Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.

Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.

Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.

Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.

Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.

Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi.


Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Prof Abdulkarim Mruma akiwaeleza wawakilishi wa wananchi wa Geita (hawapo pichani) namna wataalam wa mitetemo kutoka Ofisi yake walivyofanya utafiti kuhusu chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wakazi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Mbunge wa Viti Maalum Geita (CHADEMA), Upendo Peneza, akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani husika kuhusu malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwamba shughuli zinazofanywa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) akitoa maagizo mbalimbali kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo kuwa shughuli zinazofanywa na Mgodi zinawaathiri kwa namna mbalimbali. Waliokaa Kulia ni viongozi kutoka GGM. Kushoto ni baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini. 
 
Akifafanua zaidi kuhusu masuala hayo yaliyosababisha Serikali kufikia hatua husika, Naibu Waziri alisema kuwa mwezi Februari alipotembelea Geita, wananchi walieleza kero kubwa walizokuwa nazo kuwa ni baadhi ya nyumba zao kupasuka kiasi cha kutoweza kukalika na nyingine kukalika lakini zimeharibika kutokana na ulipuaji wa baruti (blasting) wa Mgodi wa GGM.

Malalamiko mengine yalihusu wananchi ambao wanaendelea kuwa na makazi ndani ya eneo la leseni ya GGM, ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 196. 7 ambao walikuwa wanadai fidia ili waondoke katika eneo husika au waendelee kubaki na kufanya shughuli zao za maendeleo.

Pia, baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi na hasa maeneo ya chini ya Mgodi, walilalamikia maji machafu ambayo yalikuwa yanakingwa na tuta ambalo lilikuwa limebomoka na kuruhusu maji kutiririka kuelekea kwenye makazi yao na hivyo kuwepo uwezekano wa kuathiri afya zao. Walitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia mtiririko huo wa maji.

Alisema kuwa, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, kwa suala la mipasuko, aliunda timu ya wataalam wa Serikali kutoka GST na kuiagiza kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini chanzo cha mipasuko husika kwa kushirikiana na wawakilishi wa wananchi wa maeneo hayo.

Timu hiyo ilikamilisha kazi hiyo na kukabidhi taarifa yake kwa Serikali mwezi Julai mwaka huu ambapo ilibainisha vyanzo vikuu viwili vya mipasuko hiyo kuwa ni udhaifu wa majengo yaliyoathirika lakini pia milipuko inayofanywa na GGM hasa ya miaka ya nyuma hususan kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 ambayo ilikuwa na kipimo cha juu cha mitetemo kinachofikia 57.

Kuhusu wananchi wanaoishi kwenye eneo la leseni, Dkt Kalemani alisema kuwa alimwagiza Afisa Madini wa Geita kuwaandikia GGM ili wathibitishe kwa maandishi kati ya kuwaondoa wananchi wale kwa kuwafidia kama eneo hilo lilivyo kwenye leseni yao au kuwaruhusu waendelee kuishi na kufanya shughuli za maendeleo, jambo ambalo Mgodi haukutekeleza badala yake walisema wananchi hao ni wavamizi.

Aidha, kuhusu suala la Tuta, Naibu Waziri alieleza kuwa, aliagiza lizibwe mara moja ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama maji yangeendelea kutiririka kuelekea kwenye makazi ya wananchi, ambalo pia halijatekelezwa hadi sasa.

“Ni kutokana na hali hiyo, sasa Serikali tumeona tutoe maagizo ya mwisho ili yatekelezwe na yasipotekelezwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.” Naibu Waziri alisema kuwa Serikali haina nia mbaya kwa Mgodi husika isipokuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha pia sheria zinafuatwa ili pande zote zipate haki stahiki.

“Tunapenda sana wawekezaji muwekeze kwa sababu ndiyo mnatupa ajira, mnalipa mirabaha na kodi lakini lazima tuzingatie sheria.” Dkt Kalemani alizitaka Mamlaka zinazohusika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.

DC MTATURU ATENGA SIKU YA JUMAPILI KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi.
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikagua ujenzi wa matundu ya choo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipokea maelekezo ya namna ya kuitumia miche iliyooteshwa na muwekezaji Mr Choi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alipata nafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna

Na Mathias Canal, Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A ambapo inajengwa shule mpya ili kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao. 

Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua madarasa mawili na ofisi ya walimu.

Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi ambacho kina jumla ya matundu 12.

Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi wa darasa la kwanza.

Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani Mbeya.

Sawia na hayo Mtaturu pia amebaini Changamoto waliyonayo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuendesha Shuguli zao kibiashara na mtaji ambapo amewapa nafasi ya kupeleka wajumbe watatu kwa kila kikundi kwenye viwanja vya nane nane mjini Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo na mtaji wa shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwasaidia kuanza ununuzi wa vifaa vya kusaga chakula cha kuku na mayai ili waanze uzalishaji wa vifaranga.

Dc Mtaturu pia amemtembelea Mr Choi raia wa Korea aliyeamua kuanzisha kitalu cha miche ya miti na matunda kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Kimbwi na pia amewekeza katika elimu ambapo anajenga shule ya Awali hadi kidato cha Sita.

Aidha Dc Mtaturu amempongeza muwekezaji huyo na kuwaalika wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza wilayani Ikungi katika sekta mbalimbali kwani kuna ardhi ya kutosha ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri kuwaelekeza watendaji wa Kata kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na matunda kwa Mr Choi ambaye ameamua kuungana na serikali katika kampeni ya kutunza mazingira kwa kugawa miche bure.

"Naomba mfahamu kuwa Gharama za mashine ya kusagia chakula cha kuku ni shilingi milioni 9.1 zilizotolewa na Halmashauri na wananchi walichangia kujenga majengo" Alisema Mtaturu.

Mtaturu pia amekagua ujenzi wa maabara uliokwama katika Sekondari ya Mkiwa hadi umeanza kubomoka hivyo amemuagiza Diwani kukaa na Kamati ya maendeleo ya Kata yake kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi katika Kata wapatao 2009 ili serikali iwaunge mkono kupaua na hatimaye ifikapo Januari mwakani maabara ianze kazi.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu anatekeleza kauli ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ya Hapa Kazi Tu ambapo ametenga Siku ya Jumapili kuwa Maalumu kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo.


Katika kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo pia Mtaturu alipata nafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna ambayo kitaaluma matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ilishika nafasi ya 10 bora.

Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii

Mwashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akikata keki wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam yaliyoanza rasmi tangu April 26 mwaka huu. Katikati ni Mwashamu Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara Titus Mdoe,kutoka kulia ni Mhamasishaji Mkuu wa Redio Maria Tanzania Bi. Veronica Mwita na wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania (RMTZ) Padre John Maendeleo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Mtwara Mwashamu Askofu Titus Mdoe wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre. John Maendeleo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Saalam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na wadau na marafiki wa Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Mkurugenzi wa Redio Maria Tanzania Padre John Maendeleo akizungumza na wadau na marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira akizungumza na wadau na marafiki wa Radio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 20 tokea kuanzishwa kwa Redio hiyo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipokea risala kutoka kwa Rais wa Redio Maria Tanzania Humphrey Julius Kira(Kulia) wakati wa sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akipeana mkono na baadhi ya marafiki wa Redio Maria Tanzania waliofika kuchangia Redio hiyo katika harambee iliyofanyika ikiambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Redio Maria Tanzania Bw. Humphrey Julius Kira.
Baadhi ya waumini wa Roman Katoliki wakifurahi wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Redio Maria Tanzania (RMTZ). Picha zote na Frank Shija, MAELEZO.

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Rais wa Redio Maria Tanzania, Humphrey Kira ameiomba Serikali kurekebisha Sheria ya leseni ya redio za jamii ili ziweze kuwa na vituo vingi vya kurushia matangazo yake.

Hayo yamesemwa leo na Rais huyo wakati alipokuwa akisoma risala kwenye sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya redio hiyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Msimbazi Centre, Jijini Dar es Salaam.

Kira amefafanua kuwa redio za kijamii hasa zilizojikita katika nyanja za kiimani zinasaidia kufundisha maadili na kufanya wananchi wakomae kiimani, hivyo angefurahi sana kuona redio za aina hiyo zinapewa leseni za kurusha matangazo yake nchi nzima.

“Ndugu mgeni rasmi, redio yetu inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufinyu wa sehemu za usikivu (coverage areas) ambapo tatizo hili linatokana na sheria ya leseni za redio ambayo hairuhusu redio za aina hiyo kuwa na vituo zaidi ya kumi nchini nzima, tunaomba serikali itusaidie kuiboresha sheria hii ili tuongeze vituo vya matangazo ya dini”, alisema Kira.

Rais huyo ameongeza kuwa majimbo yote yanahitaji kufikiwa na huduma za maombi, hivyo anawashauri wasikilizaji wote kuendelea kuisikiliza redio hiyo kwa njia ya mitandao ikiwemo simu za mkononi kwani hivi sasa huduma hiyo inapatika nchi nzima.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa rai kwa uongozi wa redio hiyo kutobadilisha maudhui wala kuweka vipindi visivyokuwa vya dini ili iendelee kuunganisha familia na sio kuzigawa familia.

“Tunasema kuwa redio Maria ni sauti ya kikristu nyumbani mwako lakini mimi nasema ni sauti ya Mungu ndani ya familia kwa kuwa inafanya kazi ya kuunganisha familia, vyombo vingine vya habari vinafanya kazi kubwa ya kuigawa familia lakini Redio Maria ni tofauti”, alisema  Pengo.

Askofu Pengo amewashukuru wananchi wote waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo kwa kuwa kufanya hivyo ni njia moja wapo ya kumuenzi na kumpa heshima Mama Bikira Maria.

Nchini Tanzania, Redio Maria ilianzishwa Aprili 26 mwaka 1996 katika Jimbo Kuu Katoliki la Songea ikiwa na lengo la kumsaidia Mama Bikira Maria katika kazi yake ya kumtangaza Yesu Kristo kwa watu wote. Mpaka sasa ina vituo 10 Tanzania Bara na viwili Zanzibar.

ESRF YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA NA VIWANDA

TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF) imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Akifungua mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa wananchi.

Akiwasilisha mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema, ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na kuhudumia maeneo mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).

Profesa Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia 90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za kigeni hutumika.

Katika majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo endelevu.

Akizungumzia kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya wakati wa mdahalo huo.

“Bajeti ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.” Alifafanua.

Wakichangia mada hizo, wengi wa washiriki wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kufanikiwa kwa malengo ya serikali kwenye Sekta hizo kutokana na muonekano wa bajeti yenyewe na mahitaji halisi ya sasa ya utoaji huduma kwenye Sekta hizo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa nchi kumekuwepo kwa mtazamo kuwa biashara nchini zinaanguka kutokana na mkazo wa kukusanya mapato.

Akifunga mdahalo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, aliwashukuru washiriki kwa michango yao mbalimbali na kwamba mawazo yao yatawezesha utayarishaji wa mtazamo wa wadau kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye Sekta hizo mbili za Afya na Viwanda.
Edith Mackenzie, akichangia kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akishiriki kwenye mdahalo huo.
Mkurugenzi wa SIKIKA, Irinei Kiria, akichangia mawazo yake kwenye majadiliano hayo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi, akiwasilisha mada ya changamoto zinazoikabili bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Viwanda hapa nchini, wakati wa majadiliano yaliyowaleta pamoja wasomi na wawakilishi wa taasisi za Umma na Binafsi kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF).
Dkt. Kida akichangia baadhi ya hoja za washiriki na watoa mada. Kushoto ni Profesa Prosper Ngowi.
Baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, akitoa hotuba ya kufunga mdahalo huo.
Afisa Mpipango Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Alfred Matuntera, (kushoto0, akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, (kulia), Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Afya Shirikishi Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja, (wa pili kulia), na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi.

TAASISI ZATAKIWA KUANZISHA MFUMO WA KUPIMANA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia) akitoa maelezo ya hali ya miundombinu ya mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea ofisini kwake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa (Kulia) wakati alipotembelea ofisini kwake kupata taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa huo.
Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa (wa pili kushoto) akitoa maelezo kuhusu barabara ya Ikana-Makamba –Chitete kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua barabara hiyo kwenye mkoa wa Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa wakati alipokagua barabara ya Ikana-Makamba –Chitete iliyopo mkoa wa Songwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua kituo cha kukuza mawimbi ampilification station kilichopo miangalau mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Meneja wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Katavi na Rukwa Bw. Peter Kaguru.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelothe Stephen akitoa taarifa ya hali ya Miundombinu katika mkoa huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Meneja wa Wakala wa barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa pili kushoto) akisoma taarifa ya utendaji ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Waziri Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na viongozi wa taasisi hizo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa taasisi zilizo chini ya yake (hawapo pichani), wakati alipokutana nao Mkoani humo.
Viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkoani Rukwa, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati alipokutana nao Mkoani Rukwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kuanzisha mfumo maalumu wa makubaliano utakaotumika kupima utendaji kazi wa watumishi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na kutoa matokeo chanya.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo Mkoani Rukwa alipofanya mazungumzo na Viongozi na watendaji wa taasisi hizo wakati alipotembelea mkoa huo kwa lengo la kukagua hali ya miundombinu na kuwaeleza mtazamo mpya wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Amesema katika mfumo huo Waziri ataingia mkataba na wenyeviti wa bodi wakati Katibu Mkuu wa kila sekta kuingia mkataba na watendaji wakuu wa taasisi hizo na watendaji hao wataingia mikataba na wafanyakazi wao ili kuweza kuweka mazingira ya kila mfanyakazi kufikia malengo yaliyowekwa na wizara pamoja na taasisi husika.

“Mimi nitawekeana mkataba na wenyeviti wa bodi za taasisi zote, kwa Sumatra moja ya vipengele vitakavyokuwa kwenye mkataba huo ni pamoja na mkakati madhubuti wa kupunguza ajali za barabarani zinazosababisha vifo kwa Watanzania, TCRA Makusanyo kwenye makampuni ya simu na taaasisi nyingine hivyo hivyo”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa amehimiza taasisi hizo kufanya kazi kwa bidii ili kuwajengea miundombinu iliyo bora watanzania ili kuweza kuwafikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Aidha, Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa ubunifu, kasi na uadilifu ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuwajibika kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kubadili maisha ya watanzania kwa ujumla.

“Ni wakati wa kutekeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu kwa vitendo, hivyo nawataka muwe wabunifu katika utendaji kazi za kila siku na muweze kutoa matokeo chanya ya haraka kwa wananchi”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Awali akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Lt. Mstaafu Chiku Galawa, Profesa Mbarawa amesema Serikali kupitia wizara yake itaendelea kupandisha hadhi baadhi ya barabara zilizo chini ya Halmashauri na kuwa chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), ili kuweza kuendelea kuboresha hali ya miundombinu na kuunganisha mkoa huo na Mikoa ya Mbeya, Rukwa pamoja na nchi zinazozunguka mikoa hiyo kwa barabara za lami.

Profesa Mbarawa amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa huyo kuwa Serikali itaendelea kufanya matengenezo kwa barabara zote nchini kupitia gawio kutoka Mfuko wa Barabara nchini (Road fund) ili kuinua uchumi wa Mkoa.

Waziri Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua utendaji kazi kwa wafanyakazi pamoja na hali ya Miundombinu katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Sunday, July 31, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Sia Pius ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka Miss Sinza na kufaikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadhamini wa shindano hilo.https://youtu.be/H3s12MVjf0k  

SIMU.TV: Timu ya Afrika media Group imefanikiwa kutoa sare ya goli moja kwa moja ilipocheza na timu ya umoja wa watuma salamu. https://youtu.be/1c9YuGRp1ek

SIMU.TV: Rais DR. John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa mikoa na wabunge kuwa wabunifu katika miradi mbalimbali ya Maendeleo. https://youtu.be/nAZ1a--vz5M

SIMU.TV: Waziri wa fedha na Mipango Dr Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa rais wa benki ya afrika AfDB. https://youtu.be/6DW4H7-_e8s

SIMU.TV: Chuo cha sayansi ya ardhi kikishirikiana na chuo kikuu cha Dodoma vimeanzisha mradi wa kuteteza taka ngumu ili kulinda mazingira. https://youtu.be/XURlWP2taDY

SIMU.TV: Idara ya uhamiaji Tanzania ikishirikiana na idara ya uhamiaji nchini Zambia wameanzisha utaratibu wa kuthibiti nyaraka bandia za kusafiria katika nchi hizi.https://youtu.be/linhLJKIr18

SIMU.TV: Naibu waziri wa kilimo ufugaji na uvuvi amewaagiza maafisa ardhi katenga maeneo kwa ajili ya wafugaji wa samaki. https://youtu.be/Mm9msIFIg68

SIMU.TV: Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Kinondoni limemkamata mkazi mmoja aliyekua kajiunganishia huduma ya umeme kwa njia za wizi.https://youtu.be/_Fca8AFRCyA

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zalote Steven, ameagiza kukamatwa kwa watumishi wa umma wanaoshirikiana na wananchi katika vitendo vya uvuvi haramu;https://youtu.be/6z8OpzBMxpo

SIMU.TV: Wakazi wa mkoa wa Geita wameombwa kujitokeza kwa wingi kuchangia katika hospitali ya mkoa huo ambapo mpaka sasa zimebakia chupa nne;https://youtu.be/bcrz2Uf4FKc

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli amewaagiza viongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga kinaanza kufanya kazi ifikapo Agosti 1 mwaka huu;https://youtu.be/B94FeFXDWOg

Rais Dr Magufuli amemtaka mkandarasi anayejenga barabara wilayani Manyoni, kuhakikisha anarudi kazini na kumaliza haraka ujenzi wa barabara hiyo;https://youtu.be/O_Ob6ltSyv8

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wanaoishi pembezoni mwa Barabara moja kuelekea wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameilalamikia serikali kwa kuchelewa kuwalipa fidia zao za kupisha ujenzi wa barabara; https://youtu.be/mSLzJhmYVt8

SIMU.TV: Serikali imesema itaifanyia ukarabati barabara ya Lusahunga kwenda Rusumo mkoani Kagera ambayo imeharibiwa sana kutokana na msongamano wa Malori;https://youtu.be/st5iKipEzkE

SIMU.TV: Zaidi ya wapangaji 1000 wamekosa makazi baada ya kulazimika kuondoka kwenye Nyumba zinazomilikiwa na CDA mkoani Dodoma kwa kushindwa kulipa kodi;https://youtu.be/8bb9uA3coH0

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango Dr Philip Mpango, amekutana na makamu wa rais wa benki ya maendeleo Afrika na kumshukuru kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali; https://youtu.be/MfXq-3-HTog

SIMU.TV: Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene amewasimamisha kazi afisa elimu pamoja na afisa elimu sekondari mkoani Mbeya baada ya wanafunzi wilayani Ileje kulala chini; https://youtu.be/BPKnpcpCA-M

SIMU.TV: Washiriki wa shindano la Klabu Raha Leo wametakiwa kuongeza bidii na kutokata tama kama wanataka kuibuka na ushindi katika shindano hilo;https://youtu.be/hTQJ2Mx993U

SIMU.TV: Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amelazimika kuhairisha kambi ya timu hiyo baada ya kuombwa kufanya hivyo na klabu mbalimbali nchini;https://youtu.be/LHxHulgh7sI

SIMU.TV: Wasanii wa Tanzania wameshauriwa kurekodi nyimbo zao kwa kutumia studio za hapa nchini baada ya kwenda kufanya hivyo nchi za nje; https://youtu.be/IaWjsJwufI0

SIMU.TV: Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, amewataka wachezaji wa timu ya KMC ambayo inamilikiwa na manispaa hiyo kuheshimu mikataba yao ya kazi;https://youtu.be/NTy5Ok8vvhQ

SIMU.TV: Tamasha la Tumaini Jipya lenye lengo la kuifundisha jamii kuwa na malezi bora kwa familia zao linatarajia kufanyika hii leo jijini Dar Es salaam katika uwanja wa Uhuru;https://youtu.be/pBsWgyH0unw

SIMU.TV: Mtunzi wa kitabu cha Historia ya soka la Tanzania Peter Ching’ole, amewataka watanzania kuwa na desturi ya kufanya utafiti ili waweze kuwa watunzi wazuri wa vitabu;https://youtu.be/DmISLH-WtK0

SIMU.TV: Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameanza kufungua akaunti ya magoli akiwa na klabu yake hiyo mpya baada ya hapo jana kufanikiwa kuisawazishia timu yake dhidi ya Galatasaray; https://youtu.be/sMtBAtwN7l0