Sunday, August 2, 2015

WIZI WA FEDHA KWA KUTUMIA MTANDAO TISHIO DUNIANI

Jitihada za serikali katika kupambana na uhalifu wa mitandao imeungwa mkono kutokana na baadhi ya vyuo kuanzisha mitaala yenye somo la ulinzi wa  mitandao .

Moja ya jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ni kupeleka muswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa mtandao ya mwaka 2015  katika mkutano wa 19 wa bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ulipitishwa na bunge hilo .

Taarifa ya waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknologia , Profesa Makame Mbarawa kuhusu sheria hiyo inasema kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habarina Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio ya kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi
katika jamii ikiwemo  kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia mbinu mpya za kutenda makosa ya zamani. 
Makosa hayo    yanajumuisha uhalifu wa mitandao ambapo
simu za mkononi, kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo.
Mifano ya makosa hayo ni pamoja na  Wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,  Ugaidi unaofanyika kupitia kwenye mitandao,   Maudhui potofu yanayosababisha mmomonyoko mkubwawa maadili,  uharibifu wamiundombinu muhimu ya Taifa ikiwemo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. 
 Akizungumza na gazeti hili , mtaalam wa ulinzi wa mitandao Ezekiel Mpanzo amesema tatizo la wizi wa mitandao limekuwa kubwa na benki pamoja na wananchi wamekuwa wakiingia hasara  kutokana na kutoligundua.
 Mpanzo ambaye pia ni mkuu wa chuo cha Teknologia na uongozi cha Kilimanjaro amesema  kwa upande wa vyuo vya ufundi vya NACTE  pamoja na vyuo vikuu wameliona tatizo hilo na wamejaribu kutengeneza mtaala ambao unasomo la kuzuiya wizi huo 
‘’ Tumetengeneza mtaala mzuri na kuingiza somo la ulinzi wa mtandao . Tumeuandaa sisi wenyewe na kuupeleka NACTE ambapo wameupitisha kwa hiyo tunaamini kwamba wanafunzi watakao maliza hapa watakuwa na ujuzi mkubwa na pia  utasaidia Taifa kwa ujumla kupunguza tatizo hilo ‘’ alisema Mpanzo . 
Amesema njia nyingine ya kuzuiya tatizo hilo ni wataalam wa hapa nchini ambao ni wachache kujiunga na vyama vya kuzuiya uhalifu wa mitandao duniani . 
‘’Wataalam wa hapa nchini wakijiunga na vyama hivyo vikiwamo Ethical hacking na  CISCO itasaidia kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu wanazotumia wahalifu duniani kote kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknologia ‘’ aliongeza Mpanzo. 
Alisema uhalifu huu hawakubaliani nao,  cha kufanya ni kuwa na wataalam ambao siku zote wanataarifa zaidi kuliko wahalifu na wataalam wa hapa nchini wafanye mitihani ya ulinzi wa mitandao na wanapofaulu wapewe vyeti na kusajiliwa katika vyama vya ulinzi wa mitandao duniani .
 Changamoto ya uhalifu wa mitandao imekuwa ikileta mijada ambapo katika mkutano wa kuzuiya wizi kwa kutumia mitandao ilibainishwa kuwa kati ya mwaka 2010 na robo ya mwaka 2013 Tanzania ilipoteza shilingi bilioni 9.8 kutokana na wizi huo ambao ulifanywa katika mashine za benki za kitolea fedha za ATM. 
Ripoti hiyo ya septemba mwaka jana , ilitolewa katika mkutano wa kuzuiya wizi kwa kutumia mitandao ya nchi za Afrika ya mashariki mjini Arusha .

Akifungua mkutano huo , Naibu waziri wa mambo ya ndani Pereira Silima anabainisha kuwa kuna kesi zaidi ya 300 za uhalifu wa mitandao ambazo zinachunguzwa hapa nchini na baadhi ya hizo ziko karibu kufikishwa mahakamani

‘’ Pia kutokuwepo kwa raslimali za kutosha , kukosekana kwa uelewa wa kutosha wa kushughulikia masuala hayo kwa baadhi ya polisi wetu na wengine wanaofanya sheria zitekelezwe kunasababisha mapambano ya uhalifu wa mitandao kurudi nyuma ‘’ alisema

Katika ripoti yao washiriki wa mkutano walishauri  kwamba serikali kama mdau mkuu lazima ashirikiane na sekta binafsi na taasisi za kimataifa katika kuwaelimisha wanafunzi wa vyuo vya teknologia ya habari na mawasiliano .

Mengine ni kutafuta fedha kwa ajili ya kugharamikia program za utafiti ili kuongeza uelewa uliopo sasa na kutafuta nyingine za kuzuiya uhalifu huo .

Kwa upande wa vyuo , Mpanzo anasema wao wanafundisha kozi ya usalama wa mitandao lakini kinachokosekana ni wataalam wa kutosha waliobobea katika fani ya ICT kutokana na somo hilo kufundishwa kwa nadharia zaidi .

‘’ Kukosekana kwa wataalam waliobobea kunachangiwa na fani hiyo kutolewa kwa nadharia zaidi kuliko vitendo kutokana na uhaba wa vifaa vya kufundishia pamoja na maabara za kisasa za ambazo zitamwezesha mwanafunzi kujifunza kwa ufanisi ‘’ anasema na kuongeza .

Ameshauri serikali kutilia mkazo mfumo wa NACTE wa  ngazi ya cheti na diploma  kwani uzoefu umeonyesha kuwa wanafunzi wakipitia mfumo huo hadi vyuo vikuu wanakuwa watendaji wazuri kutokana na kupata mafunzo zaidi kwa vitendo .

Kwa wanafunzi ambao hawakufaulu kidato cha nne na cha sita wanaweza kusaidiwa kwa kupitia mfumo huu kwa kusoma kozi zinazofundishwa moja kwa moja kwa vitendo  kama zinazotolewa na chuo cheti ikiwemo CISCO networking ambayo ni ya kimataifa na inafahamika duniani kote pamoja na Microsoft server, oracle data base .

‘’ Naiomba serikali kuangalia namna ya kuwasidia kwa kuwalipia ili waweze kusoma kupitia mfumo wa diploma . Faida za kupitia mfumo huu ni kwamba mwanafunzi anapomaliza na kufika chuo kikuu anakuwa mzuri zaidi kwasababu anajifunza zaidi kwa vitendo na atakuwa katika nafasi nzuri ya kupata ajira ‘’ alisema Mpanzo . 
Tatizo la wizi kupitia mitandao  ni kubwa duniani kwani ripoti iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky lab inasema genge la wahalifu wa mtandao limefanikiwa kuiba mamilioni ya dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa benki 1000 katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015 
Wizi huo ulianza mwaka 2013 na bado unaendelea mpaka leo kwani benki zote zilizoathirika hazina uwezo wa kuwazuiya . Genge la Carbanak , linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwamo kamera za CCTV ili kunakili kila kitu kinachoandikwa kwenye komputa .

Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba fedha.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, benki katika mataifa 30 yakiwamo , Russia , Marekani, Ujerumani , China , Ukraine na Kanada yameathirika kwa asilimia kubwa .

Hivi karibuni benki ya CRDB iliwaonya wateja wake kuwa makini na baadhi ya mitandao inayoibuka na kulaghai kwa kuwataka wananchi kutoa taarifa zao muhimu za kibenki jambo ambalo linahatarisha usalama wa fedha zao .


Mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo , Dk. Charles Kimei anasisitiza wananchi wanatakiwa kuwa makini na kundi hilo , wasikubali kudanganyika kwa kutoa taarifa zinazohusiana na nyaraka nyeti za benki zao na kusisitiza kuwa ni  marufuku kutoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa benki .

WATANZANIA CALIFORNIA WAMUAGA BALOZI LIBERATA MULAMULA

 Watanzania California wakiongozwa na Balozi wa Heshima Mhe. Ahmed Issa walijumuika pamoja siku ya Ijumaa na kumuaga Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na kurudi nyumbani kwenda kulitumikia taifa kama Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Watanzania wa California wakipiga picha ya pamoja na Mhe. Balozi Libarata Mulamula (wapili toka kushoto) siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomuaga rasmi.
 Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi zawadi yake Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme mara tu baada ya kukabidhiwa na Watanzania California siku ya Ijumaa July 31, 2015 walipomualika rasmi kwa ajili ya kumuaga.
 Balozi Liberata Mulamula akicheza na kuburudika kwenye moja ya nyimbo zilizopigwa kwenye tafrija hiyo.
 Balozi Liberata akipiga makofi
Moja wa kikundi maarufu cha ngomma ya asili kikitoa burudani

Mchezo wa Kirafiki Kati ya Simba na Polisi Usiku Huu Uwanja wa Amaan Simba Ikiwa mbele kwa bao 2--0

Mgeni wa rasmin katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba na Polisi Zanzibar Kamishna wa Polisi Zanzibar Ndg Hamdanmi kulia Mwenyekiti wa ZFA Wilaya ya Mjini Ndg Hassan Chura na kushoto Mjumbe wa Kamati Tendaji ya ZFA Taifa Hashim Salum na Kiongozi wa timu ya Polisi.wakisimama wakati ukipigwa wimbo wa Polisi na Usalama wa Raia kabla ya kuaza kwa mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan Simba imeshinda 2--0 
Wachezaji wa timu ya Polisi na Simba wakisimama wakati wa kupigwa kwa wimbo wa Usalama wa Raia kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuaza mwezi ujao.  
Makocha wa Simba wakifuatilia wimbo huo maalum uliopigwa wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 2--0.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Polisi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan.
Kikosi cha timu ya Polisi Zanzibar kilichokubali kipigo cha bao 2--0 kutoka kwa timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Simba kilichotowa kipigo cha mabao 2--0 dhidi ya timu ya Polisi Zanzibar wakati wa mchezo wao wa kujipima nguvu wa tatu kisiwani Zanzibar ikiwa imeshinda michezo yake yote
Mchezaji wa timu ya Simba akimiliki mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo huo
Kazi hiyo kuwania mpira kati ya wachezaji hawa wakiwa wameinua madaruga yao juu bila ya mafanikio kuupata mpira.
Mshambuliaji wa timu ya Simba na kipa wa timu ya Polisi wakiwania mpira wakati wa mchezo wao huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan Simba imeshinda 2--0.
      Kipa wa timu ya Polisi akiokoa mpira golini kwake huku mchezaji wa Simba akiwa nyuma yake
Mchezaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Polisi wakati wa mchezo wao wa kirafiki kujipima nguvu kujiandaa na Ligi Kuu zinazotarajiwa kuaza hivi karibuni Ligi ya Tanzania Bara na ya Zanzibar.
Mchezaji wa Simba akijiandaa kumpita beki wa timu ya Simba, wakati wa mchezo wao wa kirafiki katika mchezo huo timu ya Simba imeshinda 2--0
                       Wachezaji wa timu ya Simba na Polisi wakiwania mpira
Mshambuliaji wa timu ya Simba akiweka majaro golini kwa timu ya Polisi 
Picha na OthmanMapara.Blog Zanzinews.com

Saturday, August 1, 2015

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MHIMBILI 1988 WAIKUMBUKA SHULE YAO.

Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, akikata utepe ili kufungua Ofisi ya walimu wa shule ya msingi Mhimbili, iliyokarabatiwa na kuweka viti 29 na meza 8 na wanafuzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo Mwaka 1988, pamoja na kiti na meza ya kisasa katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo katika hafra fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao ikiwa imeudhuliwa na walimu wa shule hiyo wa tangu mwaka 1978.
 Walimu wa Shule ya Msingi Mhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi walihitimu katika shul;e hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo.Kutoka kulia ni Mhitimu wa shule ya msingi Mhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi mhimbili,Usia Mkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Mhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na  Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Mhimbili, George Ntevi.
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Mhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy akizungumza mara baada ya wanafunzi wa hitimu wa sarasa la saba mwaka 1988 katika shule hiyo kukabidhi viti vya walimu pamoja na meza, katika hafra fupi iliyoandaliwa na wanafunzi hao katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
Mwalimu wa shule ya msingi Mhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mhummbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafra fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dra es Salaam.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Mhimbili wakiimba wimbo kuwashukuru wanafunzi wa zamani katika shule hiyo kwa kuwakumbuka waalimu wao pamoja na shule yao.
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza katika shule ya Msingi Mhimbili wakiwa wamehudhuria hafra fupi pamoja na waalimu wao,katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo. 
 Kutoka kushoto ni Mhasibu wa wahitimu wa 1988 shule ya Msigi Mhimbili, Ernest Nyambo  katikati ni Makamu Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Mhimbili, Jacquline Kaluwa na Mwenyekiti wa wahitimu 1988  shule ya msingi mhimbili,Usia Mkoma wakiwa wameshiriki hafra iliyoandaliwa na wasnafunzi hao katika shule ya msingi Mhimbili jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akutana na ujumbe Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar michoro iliyotengenezwa na Wataalamu wa ECG ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kuwa katika mazingira ya Biashara ya Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wafanyabiashara pamoja na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri waliopo Tanzania kuangalia maeneo ambayo wanaweza kuwekeza miradi ya Kiuchumi.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana Mohammed Alef Sherief wa kwanza kutoka kushoto akimfahamisha Balozi Seif hayupo pichani fursa zinazotolewa na Taasisi yake katika kuwajengea Vijana uwezo wa kufanya Biashara.
Balozi Seif katika Picha ya pamoja na Wafanyabiashara na wataalamu wa ushauri wa Uhandisi kutoka Nchini Misri mara baada ya kufanya mazungumzo nao Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri Mhandisi Amri Alouba na Balozi wa Tanzania Nchini Misri Balozi Mohammed Hamza. Kulia ya Balozi Seif ni Mtaalamu wa Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji ya ECG Mhandisi Sherif Meurad pamoja na Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Kimataifa ya AIKAN ya Nchini Misri Bwana Mohammed Alef Sherief.
Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kufanya mazungumzo yao ya Ushirikiano wa kuimarisha uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu wa kidugu uliopo baina ya Oman na Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdullah Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

Taasisi ya Ushauri wa Uhandisi katika miundombinu ya ujenzi, usarifu wa Miji, Majengo ya Kisasa pamoja na Vituo vya Kimataifa vya Biashara { ECG } ya Nchini Misri imeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika azma yake ya kusaidia Uchumi wa Zanzibar na ustawi wa Wananchi wake.

Kiongozi wa Ujumbe wa Wafanyabiashara wa Misri wanaotembelea Tanzania kuangalia maeneo wanayoweza kushirikiana na Serikali katika uwekezaji Mhandisi Amr Allouba alisema hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Mhandisi Amri Allouba ambae pia ni Makamu  Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya  uhandisi ya { ECG } alisema Wataalamu wa Taasisi hizo wako tayari kuelekeza nguvu zao ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki, Zanzibar ikiwa miongoni mwake kutokana na mazingira mazuri ya rasilmali pamoja na uwekezaji.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Uhandisi ya ECG alisema Wataalamu wa Taasisi hiyo tayari wameshaandaa michoro ya jinsi linavyoweza kujengwa eneo la Darajani na kubadilishwa kuwa katika mazingira ya kisasa ya Biashara  ya Kimataifa.

Mhandisi Amr alifahamisha kwamba eneo hilo la Darajani upande wa iliyokuwa kituo cha Dala dala pamoja na Makontena linaweza kujengwa Vituo vya Biashara bila ya kuathiri mipango Miji iliyowekwa katika Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao umo katika urithi wa Kimataifa.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Balozi Seif kupitia Balozi Mdogo huyo wa Oman aliishukuru Serikali ya Nchi hiyo kwa jitihada inazochukuwa katika kusaidia harakati za Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar.

Mapema Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Ali Abdulla alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Nchi yake itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kuelekea kwenye maendeleo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/8/2015.

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA 4 LAANZA RASMI, WAFANYIWA SHEREHE YA UKARIBISHO KIJIJI CHA MAKUMBUSHO DAR

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri , Shindano hili litaruka katika  Runinga ya ITV Kila siku kuanzia 2.08.2015 -21.08.2015 saa 12 Jioni akicheza ngoma ya kwao wakati wakitambulishwa
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa hapo jana katika kijiji cha Makumbusho
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisalawe Bw. Ellioth Phillemon akiwakaribisha washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Wilayani Kisalawe.
 Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu. 
  Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
 Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura  ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni
  Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi.
 Wanao onekana Mbele ni Baadhi ya wenyeji ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa mama shujaa wa chakula pindi watakapokuwa kijijini.
 Baadhi ya wageni waalikwa katika Sherehe hizo
 za kuwakaribisha Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo endeshwa na Shirika la Oxfam katika Kampeni yao ya Grow.