Monday, September 1, 2014

RAIS KIKWETE ATEMBELEA WILAYA YA CHAMWINO KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA DODOMA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Fatma S. Ally alipowasili wilayani humo kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi
 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo
  Rais Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wilayani humo
 Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde "Kibajaji"
 Ujumbe toka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Msanga
 Kikundi cha utamaduni cha Shule ya Msingi ya Msanga kikitumbuiza
 Rais Kikwete akiangalia ngoma ya Kigogo ikichezwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Msanga
 Rais Kiwkete akiwapongeza wacheza ngoma wa Shule ya Msingi ya Msanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akishauriana jambo na Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally
 Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally akitoa taarifa ya Wilaya
 Watendaji wa Wilaya ya Chamwino wakiwa katika kikao na Rais Kikwete
 Rais Kikwete akitoa ushauri na maagizo kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali
 Watendaji wa Wilaya wakisikiliza kwa makini
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Chamwino akifafanua jambo
 Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri ambaye ni mwalimu mwenye ulemavu wa macho akitoa maoni yake
 Mwakilishi wa shirika la kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) akifafanua juu ya mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni
 Rais Kikwete akitoa ushauri wa njia bora za kuendeleza mradi wa chakula kwa wanafunzi mashuleni
 Vijana waliomaliza elimu ya juu na kuamua kujishuhghulisha na mradi wa kilimo wilayani Chamwino wakitambulishwa. Rais Kikwete ameahidi kuwapatia trekta ili kuongeza tija
 Mmoja wa wataalamu wa miradi akitambulishwa 
 Rais Kikwete akisalimiana na Mwalimu Silvanus Hosea wa shule ya Bwigiri
 Rais Kikwete akisalimiana na wahandisi wa mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
 Sehemu ya mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashuari ya wilaya ya Chwamwino
 Wananchi wakifurahia katika sherehe za uwekaji wa jiwwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
 Kikundi cha utamaduni cha kinamama kikitumbuiza katika sherehe za uwekaji wa jiwwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
 Mkuu wa wilaya ya Chamwino Mhe Fatma S. Ally akimkaribisha Rais Kikwete na ujumbe wake
 Katibu tawala wa Wilaya ya Chamwino akitoa muhtasari wa mradi wa ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya hiyo
 Mbunge wa jimbo la Chamwino Mh. Chibulunje akizungumza katika sherehe hizo ambapo alitangaza nia ya kutogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao mwakani
 Rais Kikwete akimpongeza Mbunge wa Chamwino Mhe Chibuluje kwa kutangaza hadharani nia yake ya kutogombea tena nafasi hiyo 
 Rais Kikwete akizungumza na wananchi
 Rais Kikwete na Mbunge wa jimbo la Chamwino Mhe Chibuluje wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
 Vifijo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
 Rais Kikwete akipata maelezo ya  mradi wa ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Chamwino
 Bango la mradi
 Rais Kikwete akilakiwa na walimu wa Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela alipowasili ili kuzindua  maabara ya masomo ya sayansi
 Rais Kikwete akikaribishwa kwa ngoma  Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela alipowasili ili kuzindua  maabara ya masomo ya sayansi
 Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde Kibajaji akiongea machache wakati wa sherehe za uzinduzi wa maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela 
 Rais Kikwete akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akizindua maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akiangala wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akiangala wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Wanafunzi wakiwa mafunzoni baada ya Rais Kikwete  kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na walimu  baada ya kuzindua  maabara  ya Shule ya Sekondari ya Dkt Malecela
 Rais Kikwete akiwasili katika Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission
 Rais Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission
 Rais Kikwete akiwapa somo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission
 Rais Kikwete katika picha na walimu na viongozi wa wanafunzi  Shule ya Sekondari ya Mvumi Mission
 Rais Kikwete akiongea na wananchi baada ya kuwasili mvumi kuzindua mradi wa maji
 Rais Kikwete akiongea na Mbunge wa Mtera Mhe Livingtsone Lusinde
  Rais Kikwete  na Mbunge wa Mtera Mhe Livingtsone Lusinde wakizindua mradi wa maji wa Mvumi
 Rais Kikwete akimtwisha ndoo mmoja wa wakinama baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mvumi
 Rais akilakiwa na umati wa watu alipowasili uwanja wa Mvumi kwa mkutano wa hadhara
 Rais Kikwete akipokea zawadi ya mkuki na fimbo 
 Rais Kikwete akimshukuru Mzee Manyweke kwa zawadi
 Zawadi zaidi toka kwa wazee mashuhuri wa Mvumi
 Rais kikwete akipata picha ya pamoja na wazee mashuhuri wa Mvumi 
 Rais Kikwete akipewa zawadi ya mbuzi kutoka kwa vijana wa stendi ya basi ya Mvumi
 Ngoma ya utamaduni
 Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde akiongea na wananchi
 Rais Kikwete akimpongeza Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde 
 Rais Kikwete akihutubia wananchi
 Umati wa wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete
 Rais Kikwete akipeana mikono na Mbunge wa Mtera Mhe Livingstone Lusinde
 Rais Kikwete akipongezwa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino
 Rais Kikwete akipeana mikono na Mhe Chibuluje
Rais Kikwete akiagana na wananchi.
PICHA NA IKULU

Sunday, August 31, 2014

Wabunge Afrika Mashariki watembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)

 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa akipanda mti  katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akipanda mti  katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira.
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo. 
 Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha  Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
 Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa  Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo.
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) Bw. Michael Kadinde wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki. TaSuBa ni taasisi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki uliopewa dhamana ya kuwa Kituo cha Maarifa katika Nyanja za Sanaa na Utamaduni
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto)  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya  Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
 Baadhi ya wageni wakifurahia ngoma wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki jana mjini Bagamoyo walipotembelea Tasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Kutoka kulia mwenye skafu niNaibu Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt.Abdulla Juma Abdulla, Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (mwenye miwani), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere, Mwenyeki ti wa Bodi wa TaSuBa Bw. Abraham Bafadhili na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TaSuBa Bw. Michael Kadind wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha sanaa kutoka taasisi hiyo wakti wa ziara ya wabiunge wa Afrika Mashariki katika taasisi hiyo jana.