Wednesday, January 2, 2013

MWAKA MPYA DAR LIVE: WASANII WAANGUSHA MUZIKI WA KUFA MTU


 Juma Nature akiwapagawisha mashabiki.
 Mkongwe Profesa J akiwapelekesha puta mashabiki.
Stamina akionyesha anavyotawala jukwaa.
 Linex akiwapagawisha mashabiki.
 Mkongwe Luteni Kalama wa Gangwe Mob akifanya vitu vyake.
 Inspekta Haroun akikamua.
Wanamuziki wa Twanga pepeta wakiwajibika jukwaani.
 KR ‘Mulla’ akifanya vitu vyake.
 Inspekta Haroun akiwa na mkewe jukwaani.
 Umati wa mashabiki ukiserebuka.
 Stamina akikamua.
 Juma Nature akiserebuka.
 Linex akiwapa hi mashabiki wake.
 Profesa J akiwa na Linex katika picha ya pamoja.
 Prefesa J akizidi kuwapa raha mashabiki.
 Luteni Kalama akiwa na shemeji yake.
 Kundi zima la Gangwe Mob likiwapagawisha mashabiki.
 Juma Nature akiwaimbisha mashabiki.
---
USIKU wa kuadhimisha kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2013 ulishuhudia burudani ya kukata na shoka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala, ambapo wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya walitoa burudani ya kufa mtu. Wasanii ambao waliwafanya mashabiki wasitulie katika viti vyao ni wakongwe Profesa J, Inspekta, Juma Nature, pamoja na wasanii wanaokuja juu katika fani hiyo ambao ni Linex na Stamina, huku bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’ wakiwapindisha migongo mashabiki.
(PICHA ZOTE: ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

Tuesday, January 1, 2013

MeTL GROUP YADHAMINI MBIO ZA MARATHON ZA KILOMETA 10 USIKU WA MKESHA WA MWAKA MPYA JIJINI DAR

Mwandaaji wa Mashindano ya Marathon ya Kilomita 10 ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 ambapo amewashukuru Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Kwa kudhamini mashindano kama haya kwa sababu miaka ya nyuma yalikuwa yakikosa udhamini wa kuaminika na kwa mshangao wa wengi walikua wakijua Mohammed anadhamini Soka tu lakini hawajui kwamba hachagui na anadhamini michezo yote.
Kutokana na udhamini wake sasa tumepata mahali pakujenga uwanja wa Riadha kwa sababu Uwanja wa Taifa sasa umekuwa kama uwanja wa maonyesho wa soka lakini riadha tunakusudia kujenga Pwani.
Mwandaaji huyo amemshukuru mdhamini wa michezo hiyo na kusema kwamba wao kama chama watatimiza malengo ya chama hicho kuitangaza Tanzania Kimataifa katika riadha.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameshukuru ubunifu huu wa kuazimisha mkesha wa mwaka mpya kwa aina tofauti ambapo watu wengi wamezoea kuadhimisha katika kumbi mbalimbali za burudani lakini sisi tumeadhimisha mwaka mpya kimichezo zaidi kwa kufanya Marathon ya Kilometa 10 yaliyojulikana kama MeTL New Years Eve Midnight Race.
Sisi kama wanamichezo tumekubaliana na wazo hili la kufanya Marathon kama hii na tumashukuru MeTL GROUP kwa kudhamini kitu kama hichi cha kipekee n kuwataka washiriki wajitokeze kwa wingi mara nyingine na pia huu usiwe mwisho bali uwe ni mwanzo wa kuendeleza michezo Tanzania na tunakiomba chama cha Riadha RT kushirikiana na wadau wa michezo kukuza mchezo wa riadha Tanzania.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiambatana na viongozi wa chama cha riadha Tanzania RT kuelekea kuzindua rasmi mashindano ya riadha ya Kilomita 10 yaliyofanya maeneo ya Masaki jijini Dar na kumalizika katika Polisi Officers Mess.
Washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamejipanga tayari kuanza mbio za Marathon 2012 katika mkesha wa mwaka Mpya jijini Dar es Salaam.
On your Mark...........Get Ready.......Paaaa..... Mgeni rasmi Bw. Anthony Mtaka aliyenyanyua mkono juu kufyatua baruti kuashiria kuanza rasmi kwa mbio hizo huku washiriki nyuma yake wakijipanga kushindana vilivyo.
Mshindi wa kwanza katika mbio hizo kwa upande wa Wanaume Bw. Dickson Marwa akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa 29:14:45.
Baadhi ya washiriki wengine wakimaliza ngwe ya mashindano hayo ya Kilometa 10 yaliyomalizika katika bwalo la polisi Masaki Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania L.t.d (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akichezea ngoma za asili ya kabila la Wagogo sambamba na Watumbuizaji hao wakati wa mashindano ya riadha ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' usiku wa mkesha wa Mwaka mpya 2013 yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo Masaki jijini Dar.
Pichani juu na chini washiriki walifanikiwa kumaliza mbio hizo wakijiandikisha.
Joggers wakiingia katika viwanja vya Police Officers Mess baada ya kumaliza ngwe yao katika mashindano hayo ya mbio za kilomita 10 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL GROUP) katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2013 usiku wa kuamkia leo.
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo Bw. Said Abrahman kutoka Zanzibar akiwa amezinduka baada kuzimia alipo maliza ngwe hiyo katika viwanja vya Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu...Mwakilishi kutoka kampuni ya MeTL GROUP Bw. Cosmas Mtesigwa akiteta jambo na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka kabla ya kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi kwa washindi.
Pichani juu na Chini ni Baadhi ya washiriki wa Marathon wakicheza kwaito na kufurahia baada ya kutimia saa 6 kamili na kuuona mwaka Mpya 2013.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwa na waratibu wengine wa shindano hilo wakiratimisha shindano hilo ili kujua kuweza nani amepata pointi zipi na kuweza kumtangaza mshindi halali.
Pichani Juu na Chini ni Mgeni rasmi Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiongoza washiriki mashindano ya riadha na wageni waalikwa kupata chakula cha jioni kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Rais Mstaafu wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bw. Francis John akitoa nasaha kwa washirki ambapo amewataka kuongeza juhudi zaidi na kutokata tamaa kwa kuwa michezo ni Afya na kuwaasa wananchi wengine zaidi kujitokeza pamoja na wadhamini wengine katika tukio kama hili ili kuupa kipaumbele mchezo wa Riadha kama ilivyoonyesha mfano na kampuni ya MeTL GROUP.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwatolea uvuvi viongozi wa vyama vya michezo vya sasa kuwacha kula kwenye michezo ya wanamichezo na kujikita katika kuvumbua vipaji vipya kwa sababu tumekuwa tukiwaona walewale kila siku kwa kufanya hivyo mtakuwa hamkuzi mchezo huu.
Mwakilishi wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akizungumza kwa niaba ya Kampuni ambapo imeahidi kuendelea kushirikiana na wabunifu wa michezo hii na pia kuendelea kushirikiana nao bega kwa bega mpaka kufikia michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Brazil na kuhakikisha wanapata medali na kuipatia sifa nchi yetu kwa kuwa na wanamichezo bora.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akiwaasa washiriki na kutoa shukrani za pekee kwa Kampuni ya MeTL GROUP kwa kuelekeza macho nguvu zao kusapoti mchezo wa riadha ambao umekuwa haupewi kipaumbele na wadhamini wengine ambao wamekuwa wakitazama mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingineyo.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bw. Dickson Marwa aliyemaliza katika muda wa dakika 29:14:45 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bi. Sara Ramadhani aliyemaliza katika muda wa dakika 33:02:31 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 100,000/= kwa Mshindi wa tatu kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Mathia Jolo aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 43:16:07 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es Salaam
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 500,000/= kwa Mshindi wa pili kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Shukuru Khalfan aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 38:51:10 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikata keki ya kuukaribisha na mwaka 2013 baada ya kukabidhi zawadi kwa washiriki wa Marathon za Mbio za Kilometa 10 usiku wa kuamkia leo jijini Dar.
MgeniRais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akifungua rasmi muziki kwa wote baada ya zoezi la kukabidhi zawadi.

VODACOM GROWN AND SEXY PARTY YABAMBA VILIVYO NDANI YA UKUMBI WA MLIMANI CITY USIKU WA KUAMKIA LEO


Mmoja wa Wahudhuriaji wa Sherehe ya Vodacom Grown and Sexy Party akifanyiwa mahojiano juu ya Sherehe hiyo Kubwa ya Kuaga Mwaka na Kukaribisha Mwaka 2013 ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika Usiku wa leo Katika Ukumbi wa Mlimani City
 
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Udhamini Kutoka kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom,Kelvin Twisa akiwa katika Zuria jekundu Wakati wa Sherehe ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
 
 
 
Baadhi ya Wahudhuriaji wa Party ya Vodacom Grown and Sexy Party Wakiwa kwenye Zuria jekundu la Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika Usiku wa Mwaka Mpya Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City 
 Wadau 
 
Neema Swai akiwa katika picha ya pamoja na rafiki yake wakati wakiingia kwenye ukumbi wa sherehe ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia Leo
Warembo wakipata ukodaki mbele ya kamera yetu Wakati wa Sherehe ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo
Warembo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani city huku wakipata vinywaji baridi wakati walipohudhuria Sherehe ya Kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha Mwaka 2013 ijulikanayo Kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
Hii ndio Panel ya Ma Dj waliowarusha vilivyo wahudhuriaji wa Sherehe ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika Usiku wa Kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City
 ilipotimia Saa Sita na Dakika Moja Usiku wa leo Ukumbi wulifanana hivyi ikiwa ni shamra shamra ya kuuaga mwaka 2012 na kuupokea mwaka mpya wa 2013 katika sherehe ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia leo
Baadhi ya wadau waliohudhuria wakibadilishana mawazo huku wakijipatia vinywaji vyao wakati wa sherehe ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy party iliyofanyika Usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City
Wadau wakiserebuka Wakati wa Sherehe ya Kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 katika shehere ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
Baadhi ya wadau wakibadilishana mawazo huku wakipata vinywaji katika sherehe ya Kuaga mwaka 2012 na kuupokea Mwaka 2013 ijulikanayo kam Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo. Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Sunday, December 30, 2012

Balozi Sefue ahimiza ushiriki wa Smart Partnership Dialogue


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akijadiliana jambo kuhusiana na mkutano mkubwa wa kimataifa wa ushirikiano kwa manufaa ya wote, Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013’, unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi Mei mwaka 2013 alipokua akiongea na wanahabari jijini la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Kaimu katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Samson Chemponda na kushoto ni Meneja Mradi wa Smart Partnership Dialogue ‘Global 2013,’ Rosemary Jairo.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Viongozi katika ngazi mbalimbali Tanzania wamepewa changamoto kutoa umuhimu mkubwa na kushiriki kikamilifu katika majadiliano ya ushirikiano kwa manufaa ya wote (Smart Partnership Dialogue) ili kuchochea haraka maendeleo katika nchi.

Wito huu umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipokua akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho ya mikutano ya kitaifa na ule wa kimataifa kuhusiana na majadiliano hayo hapa nchini.

“Ningewataka viongozi nao watoe umuhimu mkubwa kwenye jambo hili kwa sababu watanufaika sana kupata mawazo mbalimbali ya wananchi,” alisema Balozi Sefue mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa viongozi washiriki katika majadiliano katika ngazi zote kitaifa na pia wajiandae na majadiliano ya kimataifa.

Haya ni majadiliano yanayolenga kutoa fursa kwa jamii kukaa pamoja na kuzungumzia maswala mbalimbali ya maendeleo.

Kwa hapa Tanzania, chombo kitakachosimamia na kuratibu majadiliano haya kitaifa ni Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) wakati Wizara ya Mambo ya Nje ina jukumu la kuratibu mkutano wa kimataifa kuhusu majadiliano hayo hapa nchini mwezi Mei, 2013.

Mchakato wa majadiliano haya ulishazinduliwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Mei, 2012.

Balozi Sefue ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya TNBC alisema kwamba kila mtanzania ajitahidi kuelewa dhana hii kwa kusoma na kusikiliza vyombo vya habari kwa sababu ni fursa nzuri kwa kila mwananchi kushiriki katika maendeleo ya nchi na namna tunavyoweza kufikia maendeleo ya haraka.

“Hakuna mwenye ukiritimba wa mawazo kwa hiyo tunahitaji mawazo ya kila mwananchi na hivyo kila mtu ajione kuwa ana wajibu wa kuchangia maana faida itakua kwa kila mmoja na nchi kwa ujumla,” alisema.

Alisema dhana hii ya majadiliano kwa manufaa ya wote ni muhimu sana hasa kwa viongozi kwa kuwa kadiri kiongozi anavyopata maoni ya watu wengi zaidi, ndio maamuzi yake yatakavyokua sahihi zaidi na yatazingatia mahitaji ya makundi mbalimbali katika jamii.

“Kwa mfano, maamuzi ya serikali yatakubalika kwa urahisi zaidi na wananchi kwa sababu watakua wameshiriki katika kuyaandaa,” alisema.

Akielezea zaidi alisema kujenga nchi kunahitaji makundi yote kwa hiyo ni vyema watu wakipata fursa nyingine kukakaa pamoja na kujadili mambo ya msingi ya maendeleo.

Alisema majadiliano kama haya ni fursa nyingine ya kushirikisha wananchi na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa mipango katika kutekeleza Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inazingatia maoni na inakua na faida kwa kila kundi katika jamii.

Mkutano wa mwezi Mei, 2013 ni mwendelezo wa mikutano kama hii ambayo imeanza kiasi cha miaka kumi na tano iliyopita na ikianzishwa na Jumuia ya Madola kupitia taasisi yake inayoitwa Commonwealth Partnership for Technology Management na kwa ushiriki mkubwa wa aliyekuwa waziri Mkuu wa Malaysia, Dkt. Mahathir Mohammed.

Tayari TNBC imeshaanza kuendesha semina za uhamasishaji zenye lengo la kutoa ufahamu kuhusu majadliliano ya kitaifa kabla ya yale ya kimataifa.

Kitaifa, majadiliano haya yatahusisha makundi mbalimbali yakihusisha serikali, wanasiasa, wafanyabiashara, wasomi,wafanyakazi, vijana, wasanii na wakulima ambao watakaa pamoja na kujadili maswala mbalimbali yanayohusu biashara na maendeleo.

Makundi haya yatapata fursa hiyo kupitia mabaraza ya mikoa na yale ya wilaya ya TNBC ambako madajiliano hayo yatafanyika kuanzia huko hadi ngazi za kitaifa kabla ya majadiliano ya kimataifa mwezi Mei.

Makundi yote yatapata fursa ya kujadili na kutoa mapendekezo yao.