Saturday, April 7, 2018

RAIA RWANDA WAADHIMISHA MIAKA 24 YA MAUAJI WA KIMBARI JIJINI DAR LEO

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia),  Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura (wa pili kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez (kulia) wakiwasha mishumaa wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

LEO April 7 raia wa Rwanda waishio nchini Tanzania wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yalipoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu. Raia hao wameeleza kuwa kilichotokea  hawatakisahau na hakitatokea tena.

Mgeni rasmi katika kumbukizi hizo Waziri wa Habari, sanaa vijana Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana hata Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipofanya ziara nchini Rwanda mwaka 2016 alitembelea kituo cha mauaji hayo huko Kigali na kueleza kuwa haya yalianza kwa kupandikiza chuki katika jamii na kusisitiza kuwa mauaji haya hayatatokea tena Rwanda na kwingineko Afrika.

Aidha Mwakyembe ameeleza kuwa lazima tusaidiane na kushirikiana ili kuhakikisha haya hayatokei tena barani Afrika.

Naye Balozi wa Rwanda nchini ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo liliathiri wananchi na taifa kwa ujumla lakini baada ya vita Rwanda iliungana tena na kuwa wamoja na kuleta maendeleo, ameeleza kuwa wanawakumbuka wenzao ambao walilengwa kuuawa na hawatasahaulika kamwe. Pia hadi sasa wananchi wameungana pamoja na wapo sambamba katika kuleta maendeleo nchini humo.

Naye Mwakilishi wa umoja wa mataifa (UN) Alvaro Rodriguez ameeleza kuwa waliouawa watakumbukwa Rwanda na kueleza kuwa kuokoa maisha ya watu  lazima kuwe na matendo na katika kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya haki za binadamu lazima kila nchi ijizatiti katika kutimiza malengo yake ya kulinda haki za binadamu.

Maadhimisho hayo yalianza kwa sala fupi na baadaye mishumaa kuwashwa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye mauaji hayo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakiwasha mishumaa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kimasila na Chang'ombe wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura akitoa hotuba iliyolenga kuzungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 24 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
























TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAKWIMU ZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAKWIMU ZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kutoa ufafanuzi wa takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi nchini. Ufafanuzi huu unatokana na taarifa iliyorushwa na kituo cha Televisioni cha ITV katika moja ya taarifa zake za habari siku ya tarehe 29 Machi 2018 na baadaye kuanza kuzunguka katika mitandao ya kijamii inayosema “Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu-UNFPA limesema idadi ya vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi hapa nchini imeongezeka hadi kufikia vifo 556 kwa kila vizazi hai elfu moja (1000) kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwamo uhaba wa wauguzi na wakunga”.

Nikiwa Waziri mwenye dhamana ya Afya, napenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizo sio sahihi.  Na ukweli wake ni kuwa takwimu za tathimini iliyofanywa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/2016 (Ikiwa ni miaka miwili na nusu iliyopita) ya Hali ya Afya za Watu Tanzania (TDHS - MIS) ni kuwa vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 (laki moja) na si vifo 556 kwa kila vizazi hai 1,000 (efu moja). Aidha nasisitiza kuwa Takwimu hizi ni za miaka miwili na nusu iliyopita.

Ni muhimu ikafahamika kuwa Serikali ya awamu ya Tano tangu imeingia madarakani Novemba 2015, imewekeza sana katika sekta ya afya hususani katika eneo la afya ya mama na mtoto. Tuna imani kuwa endapo itafanywa Tathmini kama hii iliyofanywa na kusimamiwa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) hakuna shaka kuwa itatuonesha hatua kubwa tuliyopiga katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo tumechukuwa hatua mbalimbali zenye lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzaziMikakati ambayo serikali ya Awamu ya Tano kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya Afya imewekeza na kuitekeleza  ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni pamoja na:-
1.    Kuandaa na kuanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 5 wa mwaka 2016 hadi 2020 unaolenga kuboresha afya ya uzazi, watoto na vijana pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kufikia 292 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2020. Mpango huu umezingatia maeneo makuu matatu: ambayo ni: huduma ya uzazi wa mpango, huduma wakati wa ujauzito na huduma wakati wa kujifungua. Utekelezaji wa mpango huu unaelekeza Sekta ya Afya katika kujikita kwenye afua muhimu za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

2.    Kuongeza uwajibikaji kwa ngazi zote ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kutaka kila kifo cha mama na mtoto kinachotokana na matatizo ya uzazi kitolewe taarifa ndani ya saa 24 katika kituo cha huduma au ngazi ya Jamii kifo kilipotokea na baadaye kujadiliwa kwa lengo la kubaini chimbuko la kifo hicho na kuchukua hatua stahiki hasa kwa kutatua changamoto zinazojitokeza. Hatua hii imeanza kutekelezwa toka Octoba 2016 na imekuwa chachu katika kuboresha huduma kwa akina mama wajawazito nchini.

3.    Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI na wadau mbalimbali, inaendelea na kazi ya kukarabati Vituo vya Afya (Health Centres)  zaidi ya 220 katika Halmashauri mbalimbali nchini kwa kujenga na kukarabati majengo ya upasuaji (Theatre),  Wodi za Wazazi na Watoto,  Maabara ya damu na nyumba za watumishi ili kusogeza karibu na wananchi huduma za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni. Hadi Desemba 2015, ni Vituo vya Afya vya Serikali  (Health Centres) 117 tu (sawa na asilimia 21) kati ya vituo vya Afya vya 473 vinavyoweza kutoa huduma ya upasuaji wa dharura kwa wajawazito. Hakuna shaka kuwa jitihada hizi za Serikali ya Awamu ya Tano za kupanua huduma za upasuaji wa dharura zitaokoa maisha ya kinamama wajawazito na vichanga vyao.

4.    Huduma za Rufaa kwa wajawazito zimeendelea kuboreshwa ambapo Serikali imegawa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) zaidi ya 100 katika kuimarisha juhudi za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi katika mikoa ambayo takwimu zimeonesha kuwa ina vifo vingi zaidi vitokanavyo na uzazi.

5.    Serikali imeimarisha upatikanaji wa dawa zote muhimu zikiwemo dawa za uzazi salama kama oxytocin (inayozuia kupoteza damu wakati wa kujifungua) na dawa ya sindano ya magnesium sulphate (inayokinga na kutibu kifafa cha mimba). Aidha bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015 hadi bilioni 268 mwaka 2018/19 na upatikanaji wa dawa muhimu kwa ujumla hapa nchini upo juu kwa zaidi ya asilimia 85 kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya hususani ngazi ya msingi ambako ndiko akina mama waliowengi wanajifungulia.

6.    Serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi wa afya zaidi ya 3500 ambao wamepelekwa kwenye mikoa na Halmashauri zenye changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi.

7.    Serikali imeendelea kuboresha utoaji wa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya vinavyomilikiwa na Serikali. Tathmini ya awali ya kuhakiki Ubora wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya (Star Rating) iliyofanywa mwaka 2016 na Wizara ya Afya kwa vituo vya kutolea huduma za afya msingi 2,724 (Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali katika Halmashauri) zote katika Mikoa ya  Dar es salaam, Geita, Katavi, Singida, Mwanza, Pwani, Kigoma, Iringa, Kagera na Tanga ilionyesha kuwa jumla ya vituo 857 (31%) vilipata nyota sifuri (0) ukilinganisha  na Tathmini ya mara ya pili iliyofanywa mwaka 2017 ambapo ni vituo 138 tu (asilimia 4.87%) vilivyopata nyota sifuri. Aidha vituo 55 (3%) vilipata nyota 3 na zaidi  mwaka 2016 kulinganisha na tathmini ya mara ya pili ya mwaka 2017 ambapo vituo 612 (22.46%) vimepata nyota tatu na zaidi. Hii inaonyesha kuimarika kwa ubora wa huduma za afya ngazi ya msingi ambako ndiko akina mama waliowengi wanajifungulia.

8.    Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaochangia Mfuko wa Pamoja wa Afya (Health Sector Basket Fund) imefungua akaunti kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo Zahanati na Vituo vya Afya na kuanzia Desemba 2017 imeanza kupeleka fedha moja kwa moja kwenye akaunti za vituo hivi badala ya kuzipeleke kwenye Halmashauri zao. Hatua hii imechangia kuboresha upatikanaji wa fedha kwa wakati katika ngazi zote za kutolea huduma na kusaidia Vituo kupanga mikakati ya utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kutatua changamoto zilizoko na hivyo kuleta ufanisi mkubwa. Pia tunazijengea uwezo kamati za usimamizi za vituo katika kuimarisha uwajibikaji na kuboresha huduma katika vituo husika.

9.    Aidha Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imeanzisha Mpango wa Malipo kwa Ufanisi (Result Based Financing-RBF) kwenye mikoa 8 ambayo ina kiwango kikubwa cha vifo vya kinamama wajawazito na watoto ambayo  ni Kigoma, Geita, Kagera, Shinyanga,  Mwanza, Tabora, Simiyu na Pwani. Matokeo ya utekelezaji wa mpango huu yanaonyesha kuongezeka kwa morale ya watumishi wetu wa afya  na kuimarika kwa ubora wa huduma za afya kwa wananchi hasa wanawake wajawazito na watoto.

Hitimisho
Suala ya kuboresha afya ya mama na mtoto ni mojawapo ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli. Ninaomba watanzania wenzangu tuendelee kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha afya ya mama na watoto. Ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa hakuna mwanamke mjamzito atakayepoteza maisha kutokana na uzazi. Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa mikakati mbalimbali tuliyoweka ikiwemo kufuatilia kila kifo cha mama mjamzito kinapotokea ili kutatua changamoto zinazojitokeza. Changamoto nyingi ambazo tumebaini zinapelekea vifo vya kina mama hutokana na ama kuchelewa nyumbani kwa mama na familia katika kufanya maamuzi ya kwenda kwenye Kituo cha kutolea huduma, au kukosa usafiri stahiki wa kwenda kituoni.
Kwa pamoja tunaweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.


Imetolewa na


Ummy A. Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto
6 Aprili, 2018



Friday, April 6, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA UKUTA UNAOZUNGUKA ENEO LA MIGODI YA TANZANITE MIRERANI LEO

 Sehemu ilipofanyika sherehe za uzinguzi wa ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo ya jinsi kazi ya kujenga ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiuelekeza msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine alipokagua sehemu ya ukuta wa kilomita 24. 5 uliojengwa kuzunguka migodi ya Tanzanite eneo la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Sehemu ya ukuta wa kilomita 24. 5 uliojengwa kuzunguka migodi ya Tanzanite eneo la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara
 Sehemu ya ukuta wa kilomita 24. 5 uliojengwa kuzunguka migodi ya Tanzanite eneo la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika sherehe za  kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Askari wa JKT walipkuwa kazini kujenga ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eneo la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eneo la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husssein Mwinyi wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na hati ya kukabidhiwa ukuta aliyopokea toka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husssein Mwinyi wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsaidia mgunduzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma kuketi kitini  wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi gari la wagonjwa kwa uongozi wa serikali ya Wilaya ya Simanjiro wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi gari la wagonjwa kwa uongozi wa serikali ya Wilaya ya Simanjiro wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kukabidhi gari la wagonjwa kwa uongozi wa serikali ya Wilaya ya Simanjiro wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wenginme wakimsikiliza Mzee Jumanne Ngoma akitoa shukurani zake kwa kutambuliwa na serikali na kupewa shilingi milioni 1000 na Rais kama ahsante yake  wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wenginme wakimsikiliza Mzee Jumanne Ngoma akitoa shukurani zake kwa kutambuliwa na serikali na kupewa shilingi milioni 1000 na Rais kama ahsante yake  wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018. Kushoto ni Hassan na Asha Ngoma, watoto wa mzee huyo
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipeana mikono na Asha Ngoma, binti wa Mzee Jumanne Ngoma, mgunduzi wa madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya shukrani Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya jeshi hilo kukamilishi mbele ya wakati ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho cha Taifa mmoja wa wamiliki wa migodi ya Tanzanite ili kuwawezesha kupata ruksa ya kuingia na kufanya kazi ndani ya eneo lililozungukwa na ukuta  eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Ulinzi na Usalama ya Bunge na Mbunge wa Morogoro Vijijini Mhe. Prosper Mbena wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara  leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea maonesho ya madini ya Tanzanite wakati wa sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na familia ya mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma na wanawe kwenye sherehe za kuzindua ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine katika picha ya pamoja na watendaji wa JWTZ na JKT  waliosimamia kazi za ujenzi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akiaga  watendaji wa JWTZ na JKT  waliosimamia kazi za ujenzi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga wananchi baada ya sherehe za kuzindua rasmi  ukuta kuzunguka migodi ya Tanzanite eno la Mirelani wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara leo Aprili 6, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli katika picha na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma  wakati wa uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
Picha na IKULU

Mwalimu Rufiji ashinda pasaka mzuka jackpot ya milioni 260.




Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza na wanahabari  mapema leo jijini Dar wakati wa kumtambulisha mshindi
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga (Kulia) na kumpongeza kwa ushindi mkubwa wa kujishindia kiasi cha Shiling Milion 260. Kushoto ni Mkaguzi kutoka michezo ya Bahati Nasibu  Bakari Maggid.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 260 kwa
mshindi wa Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msenga .

Mshindi wa
Pasaka Mzuka Jackpot Edward Msengi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutambulishwa na kushukuru kwa kupata fedha hizo na kuwataka watanzania waamini kuwa mchezo huo unatenda haki.


Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaoongoza nchini leo umetangaza na kumtambulisha kwa wana habari mtanzania aliyebahatika kushinda milioni 260 kwenye Pasaka Mzuka Jackpot ambayo ilionyeshwa mubashara kupitia ITV, Clouds TV na TV 1 jumapili ya Pasaka.

Edward Msengi (56), ambaye anatokea Rufiji, Pwani ndiye aliyebahatika kuondoka na kitita cha shilingi milioni 260 ambayo ni jackpot kubwa kuwahi kutolewa kwa mshindi mmoja katika nchi hii.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bwana Sebastian Maganga alimtambulisha mshindi na kumpongeza kwa ushindi huo mkubwa. “ Sisi Tatu Mzuka tunayo furaha kiasi kwamba tumeamua kumleta mshindi Dar es salaam ili kushiriki pamoja nanyi katika tukio hili kubwa” . Msengi ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Singida na baba wa watoto wanne alikuwepo kudhihirisha furaha yake na kuhadithia safari yake aliyopitia mpaka kushinda kitita kikubwa cha milioni 260.

“ Nimekuwa nikicheza Tatu Mzuka kwa muda sasa. Nina furaha kubwa sana. Sikuwahi hata kuota kama ningeweza kupata fursa kubwa kama hii. Ninategemea kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yangu na kuwekeza katika biashara pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wangu wote wapo katika shule nzuri” alisema Bwana Msengi
 



Mbali ya tukio hilo adhim,Maganga aliufahamisha umma juu ya ujio wa  kampeni ya mwezi April ijulikanayo kama Mzuka FULL CHARGE.

“Maisha ni kusaidiana ndio maana unaposhinda Tatu Mzuka na kuwa ‘FULLCHARGE’; tunakupa fursa ya kumbusti mtu mwingine ambaye utamchagua. Shinda milioni 6 kila saa na upate nafasi ya kuingia kwenye jackpot ya milioni 10 kila siku na milioni 60 jumapili hii ili umbusti yoyote unayemtaka”