Friday, April 6, 2018

WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI WATAKIWA KUJITATHIMINI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lililofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), akizungumza na wajumbe wa baraza hilo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya sekta hiyo katika kikao cha baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora akiwasilisha rasimu ya bajeti na mpango wa utekelezaji wa sekta hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika mkoani Morogoro.
Katibu wa baraza la wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Vendeline Massawe, akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa baraza kwa kumchagua kushika nafasi hiyo mara baada ya katibu wa zamani kupata uhamisho, Mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), pamoja na viongozi wengine wakishiriki kuimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha baraza la wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi mara baada ya kufungua kikao cha baraza hilo kilichofanyika Mkoani Morogoro.

…………………

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi kujitathimini yale waliyoazimia kutekeleza kwa mwaka wa Fedha 2017/18 kama yamefikia lengo ili kuweza kusaidia kuboresha utendaji na kutafutia ufumbuzi masuala ambayo yanakwamisha ufanisi wa kazi na kuwezesha mazingira wezeshi kwa wafanyakazi.



Prof. Mbarawa amesema hayo mkoani Morogoro, wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi ambapo pamoja na mambo mengime amesisitiza umuhimu wa baraza hilo katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi wenye tija, staha na upendo.



“Ni matarajio yangu kuwa kila mjumbe kwa nafasi aliyonayo katika baraza hili atatumia fursa hii kutoa michango ya mawazo ili iweze kuwa mwongozo mzuri wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi”, amesema Prof. Mbarawa. 



Aidha, ametoa wito kwa wajumbe hao kuhakikisha kuwa Wizara inashiriki kikamilifu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwajengea watanzania miundombinu bora na imara ili kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda na hivyo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya kuifanya nchi yetu iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.



Profesa Mbarawa, amewataka wajumbe hao kujadili kwa kina Rasimu ya Bajeti na Mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2018/19 ili kuweza kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.



Awali akimkaribisha mgeni rasmi Waziri Prof. Mbarawa, Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi ya Wizara, Idara na Taasisi za Umma kuhusu usimamizi wa rasilimali watu, utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi na weledi kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya utumishi wa umma. 



Ameongeza majukumu mengine kuwa ni kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi; kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi; maslahi ya Wanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi.

FEDHA ZA UPANUZI WA VITUO VYA AFYA ZIFANYE ZAIDI YA KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.


Grace Gwamagobe-Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.

Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.

Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.

Gallawa amesema kukamilika upanuzi wa vituo hivyo vya afya kutavifanya vituo hivyo vivutie na hata mgonjwa akifika apate matumaini ya kupona na sio kukatishwa tamaa na hali mbovu ya mazingira.

“Tiba ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya akute mazingira yanavutia na sio majengo mabovu na uchafu hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata matibabu sahihi, tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutahakikisha tunapaka rangi paa za majengo yote zifanane ili vituo vyetu vya afya vivutie”, amefafanua Gallawa.

Aidha Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo kwa ajili ya matumizi.

Naye Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya kero walizokuwa wakizipata awali.

“Tunaishukuru sana serikali ya Magufuli kwakweli wametusaidia, tulikuwa tunapata shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu yakiwa hayatoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.

Kwa upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa awasaidie upatikanaji wa taa ili waweze kufanya kazi mchana na usiku naye Mkuu wa Mkoa amekubaliana na mapendekezo hayo.

Thursday, April 5, 2018

MAHAKAMA YA TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA POSTA KUSAMBAZA NAKALA ZA HUKUMU

Na Mary Gwera

MAHAKAMA ya Tanzania imeingia Mkataba na Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma za usafirishaji wa nakala za hukumu, barua na nyaraka muhimu za Mahakama.

Mkataba huo ulisainiwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta mapema Aprili 05 katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam.

Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni, utalipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na mahali walipo (Anwani za makazi).

Akizungumza kabla ya utiani saini wa mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga amesema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi.Aidha; Mtendaji Mkuu amelitaka Shirika hilo kutekeleza makubaliano hayo kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kusambaza nakala za hukumu na nyaraka nbyingine kwa wahusika na kwa wakati.

“Sitarajii kuona wananchi wanapanga foleni Mahakamani kutafuta hukumu zao na nyaraka nyingine, nina imani kuwa Posta mtafanya kazi ya kukusanya na kusambaza nyaraka hizo kwa wananchi ipasavyo,” alisema Mtendaji Mkuu.Naye  Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati ameeleza kufurahishwa kwake na utiaji saini wa Mkataba huo kwani utasaidia kufikia ndoto ya Mahakama ya muda mrefu ya kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.

“Naomba kusema kuwa, nimefurahishwa sana na hatua hii , kwani ni ndoto ya Mahakama ya muda mrefu, vilevile hatua hii itarahisisha utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Jaji Mkuu ya kutoa nakala za hukumu bure kwa zitawafikia wananchi popote watakapokuwa,” alisema Mhe. Revocati.Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe alisema alimuhakikishia Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa watafanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.

“Kusainiwa kwa Mkataba huu kutawezesha pia kuongeza kasi ya usambazaji wa barua za kawaida za Mahakama kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitachukuliwa  Mahakamani na Maofisa wa Posta na kupelekwa moja kwa moja kwa wahusika/mhusika,” alisema Bw. Mwang’ombe.

Vilevile Mkuu huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Posta hususani kwa kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.
Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Tanzania pamoja na Shirika la Posta Tanzania.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango (kulia), akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. 
Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Zuhura Pinde, akisaini akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, jijini leo.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla hiyo.

MAANDALIZI YA UZINDUZI WA UKUTA KUZUNGUKA MIGODI YA TANZANITE MEREARNI YAKAMILIKA

Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akipokelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo kabla ya kikao cha majumuisho kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Florence Turuka wakati wakikagua maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (wapili kutoka kushoto) akikagua hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 Aprili 2018.
Sehemu ya ukuta unaozunguka mgodi wa Tanzanite kama unavyoonekana kabla ya uzinduzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 Aprili 2018 katika eneo la Mirerani Mkoani Manyara.
Sehemu ya Majukwaa yatakayotumika wakati wa uzinduzi wa ukuta unaouzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa tarehe 6 Aprili 2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
PIX7.Mafundi wakiwa katika hatua za mwisho kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Mmoja wa mafundi akiendelea na kazi ya kuandaa eneo litakapowekwa jiwe la msingi wakati wa uzinduzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.
Sehemu ya geti la kuingia katika eneo la mgodi wa Tanzanite kama inavyoonekana katika picha.
Kanali Mtaula akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa ukuta wa kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani Mkoani Manyara kwa viongozi mbalimbali akiwemo Katibu mkuu Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Florence Turuka na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Saimon Msanjila, unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 6 Aprili 2018.

MAHAKAMA YAINGIA MKATABA POSTA MLANGONI NA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi. 
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango (kulia), akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. 
Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Zuhura Pinde, akisaini akisaini mkataba huo, huku akiangaliwa kwa makini na Mwanasheria wa Mahakama ya Tanzania, Peace Mpango.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, jijini leo.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla hiyo.

AIRTEL MONEY YAGAWA BILIONI 14 KWA WATEJA WAKE HADI SASA, YATANGAZA GAWIO JIPWA

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money. katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akitangaza gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money wakati kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kulia ni Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.

Airtel Tanzania imetoa gawio linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi nzima ikiwa ni  sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015.

Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8.

“Tangu tuanze kugawa sehemu ya faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha hizi wanavyotaka,” alisema.

Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza.

Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa huduma ya  Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi na rahisi kupatikana.

“Maduka haya ya Airtel Money huhakikisha mawakala wana salio la kutosha muda wote ili wateja wasipate usumbufu wanapohitaji huduma hiyo,” alisema. 

Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money, alisema kuanzia leo, wateja wa Airtel Money na mawakala watapata gawio linalofikia shilingi bilioni 1.8 kupitia akaunti zao za Airtel Money na wanaweza kutumia gedha hizo wanavyotaka ikiwemo kulipia huduma mbalimbali kama vifurushi vya mtandao, muda wa maongezi na LUKU.

Alitoa wito kwa mawakala wa Airtel Money kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kampuni hiyo iendelee kutoa gawio kwa wateja wake kila robo ya mwaka.

“Airtel Money imejizatiti kuendelea kutoa huduma bora na nafuu ambayo ni suluhisho kwa biashara za aina yoyote,” alisema na kuongeza kuwa Airtel inashirikiana na biashara zaidi ya 400 na ziadi na benki 30 katika kutoa huduma za kifedha.

Airtel ina zaidi ya mawakala 50,000 nchi nzima na inaendelea kutanua wigowake ili kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana katika miji na vijijini. 

URAFIKI WA TANZANIA,CHINA NI WA DAMU,LAZIMA UDUMISHWE NA KULINDWA-BALOZI MAHIGA




*Balozi wa Wang Ke aongoza Jumuiya ya marafiki wa China ,Tanzania kuwakumbuka waliopoteza maisha wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


 SERIKALI ya Tanzania imeungana na Jamhuri ya Watu wa China katika kumbukumbu ya vifo vya Wachina 70 waliofarika wakati wa ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Watanzania waliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustino Mahiga huku ikiwakilishwa na Balozi wao nchini, Wang Ke. Kumbukumbu hiyo, imeandaliwa na Jumuia ya Marafiki wa Tanzania na China ambayo Mwenyekiti wake Dk.Salim Salim na Katibu wake ni Joseph Kahama.

Kabla ya kuweka mashada kwenye makaburi kwenye makaburi ya wachina hao ambao wengi wao ni wataalamu na wahandisi katika ujenzi wa reli, ilitolewa historia fupi ya vifo vyao.

Akizungumza baada ya kuweka mashada, Balozi Mahiga alisema ujenzi wa reli hiyo ulithibitisha urafiki wa kutoka moyoni kati ya nchi hizo mbili na kufafanua ujenzi wake ulifungua milango kwa China kujenga viwanda vingine kama UFI na Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.

"Wakati wa ujenzi huu damu zilimwagika, wachina wamepoteza maisha na wengine wamebaki na ulemavu wa kudumu...hivyo urafiki wetu sisi na China ni wa damu," amesema.


Naye, Balozi Wang amesema nusu ya karne iliyopita, kupitia ombi la Rais wa Tanzania, Julius Nyerere na Rais wa Zambia, Kenneth Kaunda, viongozi wa kizazi cha China, Mwenyekiti Mao Zedong na Waziri Mkuu, Zhou Enlai walifanya maamuzi ya kimkakati na kihistoria kusaidia ujenzi wa TAZARA.

"Wafanyakazi na mafundi Wachina 50,000 waliitikia wito wa taifa na waliungwa mkono na wenzao kutoka Tanzania na Zambia, walishinda vigumu na vikwazo vingine kumalizia ujenzi wa TAZARA yenye urefu wa kilomita 1,860 ndani ya miaka sita na kuufanya kuwa  mradi wa kihistoria wenye umaarufu duniani,"alisema.

Amesema wafanyakazi na mafundi 65  Wakichina walipoteza maisha na walizikwa katika ardhi ya Afrika mbali na nyumbani kwao.

"TAZARA imekuwa ikifahamika kwa dunia kama reli ya ukombozi iliyowasaidia watu wa Afrika kupata Uhuru na Ukombozi...na pia reli ya urafiki ikiwakilisha urafiki wa ndani kati ya Wachina na Waafrika,"amesema.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema ipo haja kwa Tanzania na China kuendelea kudumisha urafiki wao.

"Wakati ule Mwalimu Nyerere kabla ya kwenda kuomba China watujengee reli alianza kuomba kwa nchi moja ya Magharibi sihitaji, anaetaka kuijua aje nitamnong'oneza. Nchi hiyo ilimjibu Nyerere hivi; ujenzi wa reli ya Tanzania na Zambia upitie Zanzibar. Nyerere akaondoka tukaenda China na baada ya kufika huko Mwalimu ikabidi aongee na waziri mkuu wa nchi hiyo, Zhou Enlai.

"Tena wakati anaomba hakwenda moja kwa moja alizunguka lakini hakujibiwa chochote ila wakati tunataka kuondoka tulienda kuaga kwa Rais wa China ambaye alikubali ombi letu. Kwa hiyo huu ni urafiki wa damu,"amesema.
 Mnara wa Makaburi ya Wachina waliokuwa wakijenga Reli ya Tazara  ambao walifariki wakati wa ujenzi wa reli hiyo miaka zaidi ya 40 iliyopita.
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga akitoa heshima  na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, kwenye Mnara wa makaburi ya Wachina waliofkuja kutengeneza Reli ya Tazara
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakiweka mashada kwenye moja ya kaburi la wakandarasi waliofika nchini kujenga reli ya Tazara
 Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga  akihutubia Viongozi na wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofikakatika sherehe ya kitamaduni ya watu wa china ya kuwakumbuka mafundi waliojenga reli ya Tazara.
  Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, akihutubia na kutoa historia fupi ya ushirikiano wa Tanzania na China ulivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.
 Waziri wa Katiba na Sheria , Profesa Paramagamba Kabudi akiweka maua kwenye kaburi la wataalamu wa kichina waliokuwa wanajenga reli ya Tazara.
 Kibao kinacho elezea utambulisho wa Makaburi ya Wataalam wa Kichina Gongolamboto
 Katibu  wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akieleza namana Mwalimuj Nyerere alivyoweza kuomba reli kwa kiongozi wa China Mau Sentum
  Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi  Agustine Mahiga  na  Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, pamoja na Viongozi wengine wakiwa wamesimama nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zilivyokuwa zikiimbwa.
 watu waliofika katika Sherehe za utamaduni za kuwakumbuka Wataalamu na Wakandarasi walikuwa wanjenga reli ya Tazara  kutoka china  wakitoa heshima zao kwenye mnara wa kaburi hilo
Baadhi ya Wazee walioshiriki kujenga Reli ya Tazara kwa kushirikiana na Wachina miaka 40 iliyopita.
-- 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yazindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu

Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe Hamad Rashid leo amezindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa jamii hapa Zanzibar. 

‘Leo kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tunayo furaha kubwa kutangaza ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila mama mjamzito ambaye ataudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na watoto wanaopata chanjo ya surua. Vile vile kila Mzanzibari ataweza kupokea chandarua kutoka kituo cha afya kwa kutumia koponi ambayo ataipata kutoka kwa mjumbe wa sheha,’ alisema Hamad Rashid.

Kampeni Endelevu ya ugawaji vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu una lengo la kufanya upatikanaji kwa rahisi vyandarua kupitia vituo vya afya. Ugawaji endelevu wa vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la Johns Hopkins Center for Communication kupitia mradi wa VectorWorks kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID .
,
kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP . ‘Serikali inatoa shukrani kwa washirika wa Maendeleo ya afya, Watu wa Marekani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO, Global Fund na wengine wote, aliongeza Mh Rashid.

‘Zanzibar imedhamiria kumaliza ugonjwa wa malaria kwa kusambaza vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu jambo ambalo litafanya upatikanaji wake kuwa rahisi. Upatikanaji kwa urahisi wa vyandarua ni hatua moja muhimu kwenye kupambana na ugonjwa wa malaria’, alisema Mhe Rashid akiongeza kuwa kupitia mradi huu unaozinduliwa leo, kila mama mjamzito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja watapata vyandarua bila Malipo yoyote. Vile vile alitoa wito kwa kila Mzanzibari kubadailisha chandarua chake cha zamani kwa kupata kopuni kutoka kwa Shehia kisha kutembelea kituo chochote cha Afya kupata chandarua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks Waziri Nyoni alisema ‘Tunayo furaha kufanya kazi pamoja na Kitengo cha kumaliza Malaria Zanzibar - ZAMEP kuendesha programu hii yenye lengo la kumaliza malaria Zanzibar. Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu pamoja na koponi unaendeshwa na kitengo cha Serikali cha kusambaza vifaa tiba pamoja, Zanzibar Central Medical Store (CMS). 

Kupitia mfumo huo, vyandarua na koponi zitakuwa zikipelekwa kwenye vituo vya afya na CMS, huku Mfumo wa Taarifa ukihusisha vitengo vingine vya afya kupitia HMIS, alisema Nyoni. Nyoni aliongeza kuwa VectorWorks pamoja na ZAMEP, HMIS, CMS wameandaa utaratibu ambao unahakikisha kila chandarua na kuponi inahesabiwa.

Leo tunasherekea hatua nyingine muhimu kwenye historia ya kumaliza malaria Zanzibar kwa kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila mama mjamzito na mtoto wenye umri wa mwaka mmoja wa kupata bure chandarua pamoja na kila Mzanzibari. Vyandarua hivi vitawapa usingizi mzuri lakini pia muhimu ni kinga dhidi ya malaria, aliongeza Nyoni.

Haya ni mafanikio makubwa kwa Zanzibar, alisema Mhe Rashid. ‘Tumepiga hatua kubwa dhidi ya mapambano na malaria kwa miaka mitano iliyopita. Tumeweza kupunguza ugonjwa wa malaria kuwa chini ya Asilimia moja. Lengo letu kama serikali kuendeleza juhudi hizi, na kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na washiriki wetu kwenye Maendeleo ya afya, malaria inaweza kuwa sio tishio kabisa kwa Zanzibar’, alisema Mhe Rashid.

Ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda unaongozwa na Wizara ya Afya Zanzibar kupitia Central Medical Stores, Kitengo cha kumaliza malaria Zanzibar (ZAMEP), Sekta ya afya ya uzazi na kitengo cha usimamizi wa taarifa. Kampeini imefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria. Uratibu wa kitaalam wa programu hii unafanywa na mradi wa VectorWorks. 

VectorWorks ni mradi wa miaka mitano (2014-2019) wenye lengo kuongeza upatikanaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu na vidhiti vingine vya malaria. VectorWorks inaongwa na Johns Hopkins Center for Communication Programs –CCP. Washirika wa mradi ni pamoja na PSI Tanzania, Tropical Health na chuo kikuu cha Tulane.

Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid akiongea na waandishi wa habari jana Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria. 
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid akiongea na waandishi wa habari jana Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria. 
Naibu Meneja wa Kitengo cha Kupambana na Malaria Zanzibar Faiza Bwanaheri akiongea na waandishi wa habari leo Zanzibar baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu ikiwa ni juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kupambana na ugonjwa wa Malaria chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria. Kushoto ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks Waziri Nyoni.