Wednesday, April 4, 2018

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA MEI 2018 WANAFUNZI 1003 KIDATO CHA SITA SIMIYU WAPIGA KAMBI YA KITAALUMA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunz wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya walimu mahiri 40 waliochaguliwa kufundisha na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha sita (kutoka shule 11 mkoani Simiyu) na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya  Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani humo. 
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.




Na Stella Kalinga, Simiyu

Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu, wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu.

Akifungua kambi hiyo Aprili 03 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.

“Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana  kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafundisha na kuwaelekeza na akawataka kujiamini wakati wa mtihani wao wa mwisho.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema Mkoa huo una mpango wa kuondoa daraja la nne na sifuri katika matokeo ya Mitihani ya Taifa, hivyo wanayo matumaini makubwa kuwa, kupitia makambi hayo ya kitaaluma Mkoa utaweza kufikia lengo hilo kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

“ Tumeamua kuwaleta pamoja wanafunzi ili waweze kunyanyuka kama kundi moja la mama mmoja (Simiyu) na kuweza kupandisha ufaulu, tumewaleta hapa ili kuweza kunyanyua morali wa kazi kuwaleta pamoja anayeweza na asiyeweza ili tuweze kunyanyuka pamoja kama kundi” alisema Mwl.Nestory.

Amesema katika siku 10 za kambi wanafunzi wa kidato cha sita watapitishwa katika miiko ya watahiniwa wakati wa mitihani kwa kuwa mkoa wa Simiyu unapinga suala la udanganyifu kwenye mitihani, watapitishwa katika maswali na mada ambazo baada ya tathmini ilionekana hawakufanya vizuri katika mtihani wa kanda na mtihani wa Mkoa.

Akizungumza kwa niaba ya walimu mahiri 40 ambao watakuwa wakiwafundisha na kuwasaidia wanafunzi hao, Mwl.Majaliwa Chibona wa Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu amesema, wamejipanga kuwasaidia wanafunzi katika kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kujiandaa na mitihani wao wa mwisho ili waweze kufaulu.

Nao baadhi ya wanafunzi wamesema kambi hiyo itawasaidia sana katika kuwajengea hali ya kujiamini kwa kuwa watasaidiwa na walimu katika maeneo yote yanayoonekana magumu kwao, watasaidiana wa kwa wao kupitia makundi na watapewa mbinu zitakazowasaidia kujiandaa vema na hatimaye kufanya vizuri.

Tuesday, April 3, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI WA KUZALISHA UMEME WA KINYEREZI ll JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Dkt. Alexander Kyaruzi    alipowasili kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na    Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dkt.Tito Mwinuka alipowasili kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018  
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwakilishi wa Balozi wa Japani nchini  Bw. Hiroyuki alipowasili kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Bonna Kaluwa alipowasili kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati Mhe. Dunstan Kitandula  alipowasili kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Waziri wa Nishati Dkt. Menard kalemani  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa    Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Dkt.Tito Mwinuka  kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018  
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati Dkt. Menard Kalemani  na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Stanlaus Nyongo akitembezwa kukagua  mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Steven Manda kabla ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibofya kitufe kuashiria kuzindua  rasmi mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 

 Bila kujali mvua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mamia ya wananchi waliojitokeza kushuhudia akizindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Viongozi  na wadau wengine wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Viongozi  na wadau wengine wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Viongozi  na wadau wengine wakiwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 

 Wananchi wakijumuika katika sherehe za  kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Wananchi wakijumuika katika sherehe za  kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Wananchi wakijumuika na wafanyakazi wa TANESCO katika sherehe za  kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Wananchi wakijumuika na wafanyakazi wa TANESCO katika sherehe za  kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Wananchi wakijumuika na wafanyakazi wa TANESCO katika sherehe za  kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Viongozi  na wadau wengine wakiwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Viongozi  na wadau wengine wakiwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Viongozi  na wadau wengine wakiwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Viongozi  na wadau wengine wakiwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
Burudani katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikaribisha wageni wake  katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Mama Kate kamba akisalimia katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Sehemu ya wanahabari katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Katibui Mkuu Wizara ya Nishati Dkt. hamisi Mwinyimvua akitambulisha wageni katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Mama Janeth Magufuli akitambulishwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Makatibu Wakuu wakitambulishwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kudumu ya  Nishati Mhe. Dunstan Kitandula akitambulishwa katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Wabunge wa mkoa wa Dar es salaam katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwakilishi wa Balozi wa Japan  Bw. Hiroyuki Kubota kwa hotuba yake kwa Kiswahili fasaha katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na meza kuu akipiga makofi katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifurahia wimbo katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifurahia wimbo katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akifurahia wimbo katika sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiaga baada ya sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba  baada ya sherehe za kuzindua mradi wa kuzalisha umeme MW 240 wa Kinyerezi ll eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam leo Aprili 3, 2018 

PWANI KUJENGA VIWANDA VITATU VYA MADAWA NA BAADHI YA VIFAA TIBA

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

SERIKALI mkoani Pwani, imeitikia wito wa serikali ya awamu ya tano ya kujenga viwanda vya madawa na baadhi ya vifaa tiba ambapo inatarajia kuwa na viwanda hivyo vitatu hali itakayoondoa adha ya kuagiza madawa nje ya nchi .

Aidha imekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wawekezaji ya kutoa ajira kwa watu kutoka nje ya nchi na kuwabania fursa hiyo wanaPwani ama watanzania.

Akielezea masuala ya uwekezaji na ajira ,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mjini Kibaha ,mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo alisema Viwanda vya madawa vitawezesha kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakitumika kununulia madawa nchi jirani na nje.

Alieleza viwanda vitatu vinajengwa Mkoani Pwani ikiwemo Kairuki Pharmaceuticals industry Ltd ,Zinga pharmaceuticals ambacho kitajengwa kwa ubia na waislael na kipo mbioni kuanza kujengwa na Bahari pharmaceuticals .

"Tunaikitia wito wa rais Dk.John Magufuli ,lakini pia tangu kipindi cha nyuma tumejipanga kujenga viwanda hivyo ,kupitia ziara hii tunawathibitishia wananchi tunaunga  mkono kauli ya serikali yetu"alifafanua Ndikilo.

Pamoja na hayo ,mkuu huyo wa mkoa alieleza ,zipo fursa mbalimbali  za uwekezaji  lakini vijana na wazawa wanashindwa kukimbilia fursa hizo.

Ndikilo alisema wazazi na vijana bado hawajatambua kujipanga kukuza elimu na ujuzi wao kwa ajili ya kujipatia ajira kirahisi.

Alitoa rai kwa wawekezaji ,kuacha kuwanyima ajira wazawa na watanzania ambao wanaujuzi na sifa za kufanya kazi .

" Haiwezekani tunajenga viwanda vingi lakini vijana ,waTanzania na wanaPwani hawanufaiki na ajira zinazopatikana,haikubaliki"alisisitiza Ndikilo.

"Sidhani kama Pwani ama Tanzania nzima haina wenye sifa na ujuzi,hivyo aliwataka wawekezaji hao watoe kipaombele kwa watanzania wenye uwezo .

Ndikilo alisema amepokea taarifa uwekezaji wa standard gauge eneo la Soga hawatoi ajira hata ya udereva jambo ambalo analichunguza na atakapopata uhakika watachukua hatua zinazostahili.

Aliwataka kununua vifaa vya ujenzi kama nondo ndani ya nchi ,kwani taarifa waliyompatia kwenye ujenzi wa Kairuki Pharmaceuticals industry Ltd kuwa wananunua nondo huko Uturuki .

Alisema kipo kiwanda cha Kiluwa ambacho kinatengeneza nondo zenye ubora hivyo wanunue katika viwanda vya ndani ya nchi.

Nae mkurugenzi  mtaalamu wa Kairuki Pharmaceuticals eng.Valency Assenga alisema ujenzi wa mradi huo ulianza machi 10 mwaka huu na mkandarasi ni Petra Construction Ltd Ltd na unatarajiwa kumalizika Novemba 2018.

Alielezea kazi zote zinaendelea kwani zipo hatua ya awali ya ujenzi na mpaka kukamilika ujenzi wa awamu ya kwanza kiwanda hicho kitagharimu bilioni 3.9 " #

Eng .Assenga alitaja changamoto kuwa ni miundombinu ya barabara,mradi kusuasua kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na ucheleweshwaji wa uunganishwaji wa umeme.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji huo ,Jennifer Omolo akizungumzia suala la mipango miji alisema wameanza zoezi la kupima mji muda mrefu  na wanaendelea na zoezi hilo .

Omolo aliwataka watu waache kujenga na kufanya biashara kiholela bila kupangwa ,na kuwashauri waone watalaamu wa mipango miji ofisi ya mkurugenzi ili  kupewa maelekezo ya kupata vibali .