Monday, May 1, 2017

DKT. SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI (MEI MOSI) MAHONDA, ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Mhe. Maudline Cyrus Castico alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar Maalim Khamis Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa Maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja akiwa na Viongozi mbali mbali.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Wafanyakazi wa Benki ya Tanzania BOT wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
​Wafanyakazi wa ​Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakimpungia Mkono ​Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),​alipokuwa akipokea ​​maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.Picha na Ikulu, Zanzibar.

SMZ YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA ZANUSO KATIKA SEKTA YA UJASIRIAMALI

Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Tahani Said akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mshiriki wa Mashindano ya ujasiriamali kwa Vyuo vikuu, Issah Eugenio ambaye mradi wake wa Handbags made in Jeans umechukua nafasi ya mwanzo, akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO).
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad akiutubia wakati wa kufunga mashindano yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Mhadhiri wa Chuo hicho Juma Rashid Khamis wakati akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Zanzibar yaliyofanyika katika kampasi ya chuo hicho huku Tunguu, Unguja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed Wario ambayo ni miongoni mwa wadhamini akitoa nasaha zake kwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo pamoja na Viongozi wa ZANUSO na ZU pamoja na mgeni rasmi.

Na Juma Farid, Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar  imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na baadhi ya Jumuiya za wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini zinazoonyesha nia ya kuthamini  fani ya Ujasiriamali kama chanzo mbadala cha kupunguza tatizo la Ajira nchini.

Ahadi hiyo imetolewa na  Mkurugenzi  wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad  kwa Niba ya  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko  Balozi Amina Salum Ali Wakati akifunga warsha ya Mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar ( ZU) huko Kampasi Kuu ya Chuo hicho Tunguu.

Amesema ubunifu ulionyeshwa na wanafunzi hao katika uandishi, mikakati na bidhaa  za miradi ya Ujasiriamali waliyoiwasilisha katika Mashindao hayo inajenga ushawishi kwa serikali na mashirika mengine ya kimataifa kuwaunga mkono ili wafikie malengo yao ya kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine wasiokuwa na ajira.

Amesema bado wanafunzi wengi wanaohitimu elimu ya ngazi ya vyuo vikuu nchini hawajatumia fursa zinazopatikana katika fani ya Ujasiriamali ambayo imekuwa ikitegemewa na mataifa mbali mbali duniani kupunguza  tatizo la ajira hasa kwa vijana.

“ Nasaha zangu kwenu kabla ya kuanzisha mradi wowote fanyeni tathimini na utafti wa kitaalamu kubaini aina ya ujasiriamali unaotaka kufanya una maslahi gani na wateja wako wahitaji bidhaa za aina gani sambamba na kuwa wabunifu wa kufanya miradi isiyofanana.”, alisema Katibu huyo.

Aidha alieleza kwamba kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali serikali itaendelea kudhamini miradi itakayoonyesha ustawi na maendeleo endelevu.

Pia  katika juhudi za kuwajengea uwezo wajasiriamali hao alieleza kwamba serikali itashawishi makampuni na mashirika ya kimaita ya kibiashara kufanya kazi kwa karibu na jumuiya hizo ili zipate soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao.

Hata  hivyo ametoa nasaha zake kwa wajasiriamali hao kutengeneza bidhaa bora zitakazokubalika katika soko la kimataifa pamoja na kujiongeza kitaaluma kupitia mafunzo mbali mbali ya fani hiyo.

Mapema  akizungumza  Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Bw. Juma Rashid Khamis  ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo hicho aliwasihi washiriki wa mashindao hayo kuendelea kujifunza zaidi kupitia kwa wajasiria mali wakongwe ili wapate ujuzi wa ziada wa kukabiliana na ushindani wa bidhaa na miradi ya ujasiriamali ndani na nje ya Zanzibar.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed  Wario  aliwataka Wasomi hao kutumia  vizuri  fursa hiyo ya ujasiria mali kwa kuangazia  sehemu tofauti  ambazo bado hazijatumiwa  vizuri  kibiashara  zikiwemo  Sekta ya Utalii, Uvuvi na Ufugaji ili kuzalisha bidhaa bora zinazotokana na rasilimali hizo na kuzishindanisha katika soko la ndani na nje ya nchi.

“ Kampuni  ipo tayari kushirikiana na nyinyi  wakati wowote  lakini lazima mjiongeze zaidi kufikia lengo la kufanya miradi bora na inayoendana na mahitaji ya sasa ili mpate mafanikio zaidi”, alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake mshiriki wa mashindano hayo aliyeshindanisha mradi wa usindikaji wa bidhaa aina ya Jam inayotumia kwa chakula cha mkate iliyotengenezwa kwa matunda ya Maembe, Ehlam Ali Khamis alisema wazo la kutengeza bidhaa hizo ni kutokana na kukosekana kwa matumizi mazuri ya matunda hayo hasa wakati wa msimu wake hali inayosababisha kuharibika kwa kukosekana kwa viwanda vya kusindika matunda hayo.

Akitoa ufafanuzi juu ya  Warsha hiyo,  Mwanzilishi na Msimamizi  wa Mashindano hayo  Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar  ZANUSO,  Mohamed Omar  alifafanua kwamba awali mchakato huo ulishirikisha jumla ya vyuo Sita na ulipopita mchujo vikabaki vitatu ambavyo ni Zanzibar University (ZU), State University  of Zanzibar(SUZA) na Summait University.

Mashindano hayo wamepatikana washindi saba ambao wamepewa Zawadi mbali mbali zikiwemo simu za Adroid, lakini nafasi ya kwanza ambayo imeshikiliwa na Issah Eugenio kwa mradi wa Handbags Made in Jeans, nafasi ya pili ni Ehlam Ali Khamis kwa mradi wa Mango Jam na Tatu Ibrahim ahmad abdalla na Sabrina  Khamis Machano wa mradi wa Teke knowlge solutions company  wote kutoka vyuo tofauti vilivyoshiriki kwa awatua hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MAY MOSI 2017