Thursday, April 2, 2015

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AONGOZA UPANDAJI MITI MABWEPANDE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA KUPANDA MITI

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akipanda mti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye kilelele cha maadhimisho ya upandaji miti yaliyofanyika kimkoa wilayani Kinondoni leo. Wa tatu kulia anayeshuhudia upandaji miti huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa Manispaa Kinondoni jinsi ya upandaji wa mimea mbalimbali pamoja na miti kwa kutumia matairi ya magari yaliyotumika.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamebeba miche ya miti wakielekea kuipanda katika maeneo mbalimbali shuleni hapo.
 Wananchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya upandaji miti.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Msanii akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akipanda mti.
 Diwani wa Kata ya Mabwepande, Clement Bocco  akipanda mti katika eneo la shule ya Mji Mpya.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki kikapu kilichotengenezwa kwa matairi yaliyotumika baada ya maadhimisho hayo.
 Wasanii wakitoa burudani.
 Maofisa wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye 
maadhimisho hayo.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakiserebuka pamoja na wananchi katika maadhimisho hayo ya upandaji miti mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande.
Wananchi wakicheza segere baada ya kumalizika kwa zoezi 
hilo la upandaji miti.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema waathirika wa mafuriko ya mto Msimbazi walioondoka baada ya kupewa viwanja maeneo ya Mabwepande na kurudi eneo la Msimbazi watanyang'anywa viwanja hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki ya upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofikia tamati leo kwa upandaji miti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mji Mpya iliyopo Mabwepande ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa mwenyeji.

"Natoa maagizo kuwa wale wote waliopewa viwanja na serikali hapa Mabwepande ambao wameondoka viwanja vyao wanyang'anywe kwani ni wasariti na wale waliouziwa imekula kwao kwani serikali haiwatambui" alisema Sadiki.

Sadiki alitoa mwito kwa wananchi kubadilika kwa kuacha kutumia nishati ya miti na mkaa badala yake watumie gesi ambayo inapatikana kwa wingi kutokana na jitihada za serikali ili kulinda mazingira.

Aliongeza kuwa suala la upandaji miti ni endelevu hivyo kila mtu mahali alipo apande mti walau mmoja na kuitunza kwani miti ni uhai.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda alisema Manispaa hiyo inabustani kubwa  maeneo ya Kilongawima hivyo wanajipanga kuanzisha mashindano ya ukuzaji na upandaji wa miti kwa kata zake 34 na mshindi atapatiwa zawadi.

Katika hatua nyingine amesema halmshauri hiyo itawakopesha fedha wananchi waishio Mabwepande ambao waliathiriwa na mafuriko kwa ajili ya kukamilisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja vyao kabla ya mwezi wa sita badala ya kusubiri fedha kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema changamoto ya kukamilika kwa nyumba za askari polisi na kituo cha polisi katika eneo hilo itakwisha katika kipindi kifupi kijacho.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Wednesday, April 1, 2015

SSRA HOSTED DELEGATES FROM PUBLIC SERVICE COMMISSION OF ZIMBABWE & TANZANIA, POPSM OFFICE

Head of Public Relations & Promotions of Social Security Regulatory Authority (SSRA), Mrs. Sarah Kibonde Msika (left) inviting delegates from Public Service Commissions of Zimbabwe & Tanzania
Head of Public Relations & Promotions of Social Security Regulatory Authority (SSRA), Mrs. Sarah Kibonde Msika making presentation regarding Social Security Sector in Tanzania
SSRA Staff first left Dr. Carina Wangwe, first right Mr. Sabato Kosuri & Teophory Mbilinyi listening to presentation.
On Behalf of SSRA Director General, Head of Public Relations & Promotions of Social Security Regulatory Authority (SSRA), Mrs. Sarah Kibonde Msika handles a small present to Mrs. M. Michada Chairperson of Zimbabwe Public Service Commission.
A group pictures of Delegates from Public Service commission of Zimbabwe & Tanzania Seating first from left Chairperson of Public Service commission (PSC) of Tanzania Dr. Steven Bwana, second Chairperson of PSC- Zimbabwe Mrs. M. Michada,third Commisioner of PSC- Zimbabwe Mr. Stephen Ngwenya & Head of PR &Promotion SSRA Mrs. Sarah Kibonde Msika
Delegates in a jovial mood after hearing a thank you Note from SSRA.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI CHARLES KITWANGA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (hayupo pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akisoma hotuba ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa kwanza kushoto). Katikati ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.
Sekretarieti inayoratibu mkutano wa baraza la wafanyakazi la Wizara ya Nishati na Madini wakisikiliza kwa makini na kunukuu mada zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa kuonyesha mshikamano ujulikanao kwa jina la “solidarity forever”.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mhasibu Mkuu Mfawidhi wa Wizara ya Nishati na Madini, Michael Marandu (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano ili kufungua mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga (katikati, waliokaa mbele) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi, Wizara ya Nishati na Madini.

TASWIRAZZ KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Pangani, Saleh Pamba bungeni mjini Dodoma Aprili 1,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Wizara Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana akijibu swali la msingi la Mhe.Kidawa Salehe (Mb) Viti Maalum CCM lililohoji juu ya Serikali imefanya utafiti gani juu ya sababu za ukatili kwa watoto,bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.
Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mhe.Stephen Kebwe akijibu swali la Mhe.Maryam Msabaha (Mb) Viti Maalum CHADEMA lililohusu serikali inamikakati gani kuboresha Hospitali zetu wananchi wa vijijini waweze kupata huduma hiyo kiurasi,Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe.Stephen Masele akijibu swali la Msingi la Mhe.Amina Makilagi (Mb) Viti Maalum CCM lililohoji kuhusu serikali itatumia lini tafiti zilizofanyika zakutumia nishati Mbadala, Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015 .
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Mhe.Charles Mwijage akijibu swali la Msingi la Mhe.Moses Machali (Kasulu Mjini) lililohoji kuhusu utekelezaji wa mradi wa umeme kutoka Mto Malagarasi ambao ulipaswa kutekelezwa kwa kutumia fedha za MCC Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015. 
Mbunge wa Kisarawe (CCM) Mhe.Seleman Jafo akiwasilisha hoja binafsi kuomba tarehe ya kura ya maoni isogezwe mbele na kupendekeza Serikali ipeleke Muswada Bungeni wa hati ya dharura kupitisha Katiba ya mpito,Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma mara baada ya kuhairisha bunge kutokana na fujo zilizozuka ndani ya bunge kutoka na kuwepo kwa mwingiliano wa hoja binafsi kati ya Mhe.Seleman Jafo (Mb) CCM Kisarawe na Mhe.John Mnyika (Mb)Ubungo CHADEMA Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.
Baadhi ya wabunge wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya Spika kuhairisha bunge kutokana na kuzuka kwa fujo Bungeni Mjini Dodoma 1 Aprili,2015.

Bunge la Pitisha Sheria ya Kuanzishwa Baraza La Vijana

Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.

Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Vijana litakalo kuwa chombo cha vijana kitakacho waunganisha Kitaifa bila kujali itikadi zao za Kisiasa,Imani zao za Kidini wala tofauti zao za Rangi,hayo yamesemwa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Fenella Mukangara alipokuwa akisoma Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania Bungeni Mjini Dodoma.

Mheshimiwa Mukangara aliendelea kusema Baraza hilo litaisaidia Serikali kuweza kuwafikia vijana kwa urahisi na kusikiliza shida zao pamoja na kutoa ufumbuzi wa hoja mbalimbali za vijana.Hata hivyo chimbuko la Muswada huo ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya 2007,Ibara ya 3 Sehemu ndogo ya 11 inayosema kwa uwazi Serikali itawezesha kuundwa kwa Baraza Baraza la Vijana na kuanzisha mfumo wa kisheria ili kuliwezesha kufanya kazi.

“Madhumuni ya Muswada huu ni Kutunga Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania(The Youth Council of Tanzania 2015) ili kuwa na chombo cha Kitaifa cha kuwewezesha vijana kujadili masuala yao,kutambua majukumu yao,kukuza maadili mema,kukuza moyo wa umoja ,uzalendo,uwajibikaji na kujitolea kwa malengo chanya miongoni mwao katika nchi yetu,”alisema Mhe.Mukangara.

Mbali na hayo katika sehemu ya pili kifungu cha 4-15 cha Muswada huo unaeleza juu ya masharti mbalimbali kuhusu Uanzishwaji,Uanachama,Muundo na kazi za Baraza.Pia sehemu hii imefafanua Mamlaka ya Baraza na vyombo vya utendaji katika ngazi ya Taifa,Mkoa na Wilaya.

Aidha,kwa upande wa maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yaliyosomwa na Mwenyekiti wake Said Mtanda aliishauri Serikali katika kifungu cha 4(3)Kisomeke Uanachama utakuwa na uwazi na hiari kwa kijana yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 15 mpaka 35.Pia kifungu cha 4(4) imeeleza kuwa baraza halitakuwa kisiasa liongezwe neno halitakuwa na Itikadi za Kidini.

Katika kipindi cha majadiliao ya Muswada huo naye Mhe.Kuluthum Mchuchuri (Mb) Viti Maalum CUF aliipongeza Serikali kwa mchakato wake mzuri wa kuandaa Baraza la Vijana litakalo saidia vijana kujadili matatizo yao na kuyawasilisha Serikali kwa kupatiwa ufumbuzi kwa urahisi,pia ameishauri Serikali katika suala la wajumbe uwawakilishi waanze kuanzia ngazi ya Kata na Serikali pia iweke wazi ni kwa utaratibu gani wawakilishi hao watapatikana.

Naye Mhe.Magret Sitta Mbunge wa Viti Maalum CCM aliiomba Serikali kuandaa ziara kwenda kuangalia mabaraza ya Vijana katika nchi za wenzetu yanafanyaje kazi na kujifunza,pia aliendelea kuiomba Serikali itoe mafunzo mbalimbali ya ufundi kwa kushirikia na taasisi ya Veta na Vyuo vya Wananchi ilikuwapatia elimu itakayo wasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kupunguza idadi ya vijana wa vijiweni.

Pamoja na hayo naye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR) Mhe.Moses Machali alishauri Serikali Kuanzisha asasi moja ambayo vijana watakayo jiunga huko ili kudhibiti uanzishwaji wa asasi bandia kwa watu wenye nia ya kujinufaisha,pia aliipongeza Serikali kwa kuleta Muswada huo kwani unamanufaa Makubwa kwa vijana.

Aidha,mbali ya kuwepo na marekebisho mbalimbali ya Muswada huo Serikali iliyapokea maombi ya Suala la Baraza hilo kuanzia katika ngazi ya Kata ilikupata uwakilishi uliyowa uhakika na baraza likalete manufaa kwa kuanzia ngazi ya chini ambapo ndipo vijana wengi wanapatikana na jamii inawafahamu kwa usahihi zaidi.

Halikadhalika Serikali iliridhia kuanzishwa kwa uwakilishi wa vijana watano kutoka kundi maalum kwa maana ya wenye ulemavu na ili kuweka uwianao wa vijana hawa kuweza kuwasilisha maombi yao kwa Serikali kwa urahisi huku ikizingatia mahitaji yao maalum.

Waziri Lukuvi ahitimisha ziara ya siku mbili kushuhudia utendaji wa NHC

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Nyumba za gharama nafuu za NHC Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akisikiliza maelezo ya Injinia wa NHC, Elisante Ulomi anayesimamia Mradi wa Mwongozo Housing Estate mchana wa leo. Mojawapo ya Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam inavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za gharama nafuu za NHC Kibada, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri Lukuvi alipozitembelea. Nyumba za mradi mkubwa wa NHC Morocco Square, Dar es Salaam zikiwa zinajengwa katika hatua ya msingi, zinavyoonekana leo wakati Waziri alipozitembelea. Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya Nyumba ya mfano itakayojengwa katika kitalu nambari 300 kona ya kuelekea kwenye Hospitali ya Mikocheni jijini, Dar es Salaam leo. Waziri Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria zinazojengwa na NHC alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Waziri Lukuvi akipata maelezo ya mradi wa nyumba za NHC Victoria kutoka kwa Mkurugeni wa Ubunifu wa NHC, Issack Peter alipokuwa akikagua mradi huo mchana wa leo. Mmojawapo wa mafundi wajenzi wanaojenga nyumba hizo za Victoria akiwa kazini wakati wa ziara ya Waziri.

Kadiri muda wa kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa unavyowadia, wananchi hawajaamua “ndiyo” au “hapana”


Wakati kura ya maoni inakaribia, wananchi wamejigawa katikati. Zaidi ya nusu yao (asilimia 52) wanasema wataunga mkono Katiba Inayopendekezwa. Lakini mwananchi mmoja kati ya wanne (asilimia 26), sawa na nusu ya wanao tayarajia kuiunga mkono katiba, wanasema wataipinga. Mwananchi mmoja kati ya watano (asilimia 22) bado hajamua. 

Mnamo mwaka 2014, wakati rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC) inajadiliwa, wananchi wengi (asilimia 65) walisema wangepiga kura kuikubali rasimu hiyo, na wananchi wachache (asilimia 21) walisema wangeipinga. Ingawa takwimu zinaonyesha kuwa Katiba Inayopendekezwa ingepitishwa na wananchi wa Tanzania Bara, tofauti kati ya makundi haya imezidi kuwa finyu. 

Maoni ya wananchi yanaonyesha wazi mashaka yaliyopo katika mchakato mzima wa kuibadili katiba. Mwezi mmoja tu kabla ya siku ya kupiga kura, uandikishaji wa wapiga kura bado haujakamilika. Nusu ya wananchi (asilimia 47) wanafikiri kuwa uchaguzi mkuu ujao utafanyika chini ya katiba mpya, lakini idadi ndogo (asilimia 30) inafikiri kuwa uchaguzi huo utafanyika chini ya katiba ya sasa. 

Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika muhtasari wenye jina la: Kuelekea Kura ya Maoni | Maoni ya Watanzania kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Muhtasari huu umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi (www.twaweza.org/sauti). Muhtasari huu unajumuisha maoni ya wananchi wa Tanzania Bara (Zanzibar haikuhusishwa katika utafiti huu) juu ya Katiba Inayopendekezwa. Takwimu hizi zinatokana na duru la 29 ya Sauti za Wananchi. Jumla ya wahojiwa 1,399 walipigiwa simu kati ya Januari 27 na Februari 17, 2015. Matokeo mengine yanatokana na duru la 5 la Sauti za Wananchi, (iliyowahoji watu 1,708 kati ya Julai 16 na Julai 30, 2013) na duru la 14 la Sauti za Wananchi (iliyowahoji watu 1,550 kati ya Februari 12 na Machi 4, 2014). Takwimu hizi zimetumika kufuatilia mwenendo wa muda mrefu. Ni muhimu kukumbuka kuwa mahojiano haya yalihusisha makundi yote ya wananchi wa Tanzania Bara. 

Tofauti kati ya “ndiyo”’ na “hapana” ulipungua kati ya mwezi Machi 2014 na Februari 2015, kipindi kilichoainisha mabadiliko mengi katika mchakato mzima wa kubadili katiba. Mabadiliko haya yaliyotokea kati ya rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na rasimu ya Katiba Inayopendekezwa  yanaleta wasiwasi baina ya wananchi. Wananchi wanne kati ya kumi (asilimia 39) wameonesha kuipendelea Katiba Inayopendekezwa. Idadi iliyo ni sawa na ile (asilimi 41) ya wanaoipendelea rasimu ya pili ya katiba. 

Hata hivyo, kuna tofauti kubwa kati ya rasimu hizi mbili. Wananchi walipohojiwa kuhusu vifungu maalumu, majibu yao yalikuwa ya uwazi zaidi. Wananchi nane kati ya kumi (asilimia 80) hawakubaliani na kuondolewa kwa kifungu cha kuwawajibisha wabunge wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao. Idadi inayokaribia hiyo Asilimia 78 ya wananchi hawakubaliani na kuondolewa kwa kifungu cha uwazi na uwajibikaji kwenye orodha ya tunu za taifa. Wananchi saba kati ya kumi (asilimia 70) hawakubaliani na kufutwa kwa kifungu cha ukomo (miaka 15) wa mbunge kushika ofisi. Kwa upande mwingine, wananchi wachache (silimia 36) hawakubaliani na kubadili muundo wa Muungano kutoka serikali 3 kubakia kuwa wa serikali 2. 

Je, wananchi wanakubaliana na UKAWA kususia vikao vya Bunge la Katiba na ushawishi wake kwa wananchi kususia kura ya maoni? Kati ya wananchi waliosikia minong’ono juu ya UKAWA kususia vikao vya Bunge la Katiba, asilimia 66 wanapinga hatua hiyo. Asilimia 68 wanapinga ushawishi kwa wananchi kususia kura ya maoni na robo tatu (asilimia 75) ya wananchi wanasema hawatasusia kura ya maoni. 

Elvis Mushi, Mratibu wa Sauti za Wananchi alitoa maoni yake kuhusu matokeo haya nakusema “Mashaka yaliyopo juu ya kukamilika kwa mchakato wa mabadiliko ya katiba na kubadilika kwa mwenendo wa mchakato huo kumesababisha mashaka kwa wananchi. Hali hii ndio inayosababisha maoni ya wananchi kugawanyika katikati kuhusiana na maswala yote muhimu”

Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, akaongeza “Kuna mambo matatu yanayojitokeza kutokana na maoni haya ya wananchi. Jambo la kwanza ni kwamba kura ya “ndiyo” kwa Katiba Iliyopendekezwa haina uhakika. Tofauti iliyopo ni finyu na wananchi wameonesha kwamba kura hii inaweza kubadilika wakati wote katika mchakato huu. Pili, kuna kilio kilicho wazi kuhusu umuhimu wa katiba kusisitiza maswala ya uwazi na uwajibikaji. Wananchi wameunga mkono kwa nguvu zote vifungu vinavyoimarisha uwajibikaji. Changamoto kubwa zilizopo katika upatikanaji wa huduma za kijamii na kuwepo kwa tatizo kubwa la rushwa vyote vimekuwa na athari kubwa na wananchi wanatafuta njia za kuwawajibisha viongozi kwa matendo yao. 


Tatu, wananchi hawajashawishika kuchukua hatua za nguvu za kuleta mabadiliko. Wito wa UKAWA wa kususia kura ya maoni haujawavutia na wananchi wengi hawauungi mkono. Mambo haya matatu yatakuwa changamoto kubwa kwa viongozi wa ngazi zote kuamini  kwamba mawazo yao yanawakilisha maoni ya wananchi.”