Ukiwa unatoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Sir Seewoosagur Ramgoolam International Airport,Mauritius lazima utaona bango hili ambalo linakaribisha katika nchi hiyo.Endelea kuburudika na taswira mbali mbali za Mauritius.
Wednesday, July 2, 2014
MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WILLIAM ERIO AKAGUA BANDA LA PPF KUJIONEA UTENDAJI KAZI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mhe William Erio akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko huo wakati alipotembelea Banda laa PPF kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wake katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea Kufanyika katika Viwanja vya Mwl Nyerere.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Mhe William Erio akiteta jambo na wafanyakazi wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wake. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF, Bi Lulu Mengele na Katikati ni Mbaruku.
Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akimuhudumia mteja aliyefika katika Banda la PPF kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF.
Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel (kushoto) akirufahia jambo na mmoja wa wateja wa PPF aliyefika katika banda la PPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika katika Viwanja hivyo vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakimsikiliza kwa makini mmoja wa mteja aliyefika katika banda la PPF kwaajili ya kujiunga na Mfuko huo wa Pensheni wa PPF katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa PPF, Mohamed Siaga akitoa maelekezo kwa mteja aliyefika kwenye dawati lake kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali za mfuko wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam.Picha zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
DIAMOND PLATNUMZ BET RED CARPET AND BEHIND THE SCENE !
Diamond Platnumz akipita kwenye Red Carpet ya BET mbele ya Mapaparazi zaidi ya 200,Mwanamuziki huyu alionekana kuwavutia watu wengi na Suit yake iliyokuwa imemkaa kisawasawa ambayo waingereza wanasema "Well Tailored Suit" By Designer Sheria Ngowi .
Mapaparazi zaidi ya 200 walichukua every step and moments za Red Carpet wakati Diamond akipita
Mwanamuziki Nelly alitushangaza pale alipomvuta koti Diamond kwa nyuma na kumwita kwa Jina,Tulishangaa sana kuona kumbe wanamuziki wa Marekani nao wanafatilia habari za African Nominees.
Hapa Diamond aligeuka nakukuta aliye mvuta koti ni Nelly ambaye alimwambia congratulations.
Ndani kwenye Award show Diamond na USA Manager wake Bwana DMK wakipata Ukodaki
ULIPO TUPO NA BENKI YA CRDB HADI HADI VIWANJA VYA SABASABA
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kuweka fedha na kutoa katika Mobile Branch lililopo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Benki ya CRDB akiwahudumia wateja waliofika katika banda la Benki ya CRDB wakati wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwahudumia wateja wapya waliofika kufungua akaunti.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Julius Ritte akiwasikiliza kwa makini wateja waliotaka kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na Benki ya CRDB pamoja na kujua faida ya kujiunga na huduma ya Simbanking kabla ya kufungua akaunti.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Mose Wamala akiwahudumia wateja wa Benki hiyo kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Banda la benki ya CRDB linavyoonekana.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Moses Wamala akimpiga picha mteja aliyefungua akaunti ya Benki ya CRDB katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa.
Ofisa wa Benki ya CRDB (kulia), akiwasaidia wateja wa benki hiyo kujaza fomu.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki katika tawi la benki hiyo lililopo katika viwanja vya Sabasaba.
KAMISHNA WA POLISI JAMII NCHINI,MUSA ALI MUSA AFANYA ZIARA WILAYA YA MWANGA
| Kamishna wa Polisi Jamii nchini ,CP Musa Ali Musa akitia saini katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake wilayani Mwanga. |
| Baadhi ya askari Polisi wa kada mbalimbali pamoja na viongozi kijiji cha Kisiwani wakimsikiliza kamishna wa Polisi jamii,Musa Ali Musa alipofanya ziara wilayani Mwanga. |
| Kamishna wa Polisi jamii Nchini,Musa Ali Musa akizungumza na maofisa wa Polisi wa kada mbalimbali katika wilaya ya Mwanga (hawako pichani) |
| Kamishna wa Polisi nchini Musa Ali Musa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa jeshi hilo pamoja na baadhi ya wananchi katika wilaya ya Mwanga. |
| Kamishana atembelea kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Mwanga. |
| Kamishna wa Polisi Jamii nchini ,Musa Ali Musa akipokewa na gwaride maalumu lililoandaliwa na askari Polisi kituo cha Mwanga. |
| Kamishna wa Polisi Jamii nchini ,Musa Ali Musa akitizama eneo ambalo linatazamiwa kujengwa kituo kipya cha Polisi. |
| Kamishna Musa akiondoka eneo hilo mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya ya Mwanga. |
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
Subscribe to:
Posts (Atom)






































































