Thursday, May 1, 2014

Wafanyakazi Ruvuma watakiwa kutimiza wajibu na kisha kudai haki

Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
SERIKALI ya mkoa wa Ruvuma imeendelea kuwasihi wafanyakazi wa sekta zote nchini wasijenge zaidi utamaduni wa kudai haki bila kutimiza wajibuwao kwanza kwa sababu kauli mbiu za vyama vingi vya wqafanyakazi kikiwemo chama cha walimu nchini ambacho kauli mbiu yake  ni wajibu na haki.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh. Abdula Lutavi
 -----------------
Kauili hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdula Lutavi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo amesema baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wamekuwa hawatimizi wajibu wao ipasavyo lakini ndiyo wanakuwa msitari wa mbele kulaumu na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wao kwanza kwa mwajiri.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA Songea wakipita mbele ya jukwaa kuu huku wakionyesha mavazi wanayoshona chuoni hapo ikiwemo mavazi la maharusi na ya ulimbwende.
-----------------------------------
Amesema sekta ya elimu ndiyo yenye watumishi wengi ambao wapo katika kila kijiji nchini na ndiyo wataalamu wanaotumiwa na wananchi wa maeneo hayo lakini baadhi yao wamekuwa ni watoro na wazembe katika maeneo yao ya kazi na kutotimiza wajibu wao kwa makusudi na kwa visingizio mbali mbali na wakiendelea kulindwa na walimu wakuu pamoja na wakuu wa idara za kielimu hali ambayo inazidi kudumaza kiwango cha elimu mkoani Ruvuma na kuufanya mkoa kuendelea kutofanya vizuri katika sekta hiyo muhimu.
Mtangazaji wa TBC mkoani Ruvuma Noela Njawa akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
---------------------
Aidha amesema walimu watoro na wazembe ndiyo wanakuwa wa kwanza kulaumu na kulalamikia masilahi duni na kuhamasisha migomo ambayo imekuwa ikiwaathiri wanafunzi pasipo sababu huku serikali ikionenesha nia kuongeza na kuboresha maslahi yao ikiwa ni pqamoja na kulipa malimbikizo mbali mbali wanayoidai serikali ambayo taratibu za malipo zinaendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika.

Nao wafanyakazi wa sekta mbali mbali mkoani Ruvuma katika risala yao kwa mgeni rasmi wameelezea kusikitishwa kwao na kitendo cha taifa kuadhimidsha miaka hamsini ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku taifa likiwa salama kutokana na dhana iliyojengeka ya kuzingatia  utawala bora katika kila Nyanja lakini bado kumeendelea kuwepo kwa matatizo ya madeni ya watumishi,mishahara duni na waajiri kutokujali sheria za kazi vitu ambavyo vimekuwa vikiendelea kugonga vichwa vya wafanyakazi walio wengi na kupunguza morali ya kazi.
Mfanyakazi wa Idara ya wakala wa majengo Mkoa wa Ruvuma Wizara ya Ujenzi Bw. Charles Buhili akipokea zawadi ya mfanyakazi bora.
----------------------
Wamesema imekuwa ni kawaida kwa watumishi wa umma kupewa ahadi kila mara za kupunguziwa matatizoi yao katika maeneo yao ya kazi yakiwemon madeni ya muda mrefu ya watumishi hao lakini utekelezaji wa ahadi hizo umekuwa ni wa kusuasua pamoja hali ya haslisi ya kiuchumi wa taifa ikijulikana hali imekuwa ikiwavunja moyo watumishi walio wengi wa umma kutimiza wajibu wao.
Mlinzi wa CCM mkoa wa Ruvuma Bw. Mika Nchimbi akipokea zawadi ya mfanyakazi bora
------------------------
Aidha wafanyakazi katika risala hiyo wametoa maoni kuwa utekelezaji wa ahadi hizo ungekuwa unapewa uzito kama vile zinavyotolewa kwa msisitizo na viongozi mbali mbali wa serikali na waajiri kikiwmo kilio cha muda mrefu cha kodi kubwa kwa wafanyakazi walioko kwenye mfumo rasimi ambao wamekuwa wakikatwa kodi hiyo moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao ambayo haikidhi mahitaji ikilinganishwa na gharama za maisha ya kila siku.

MRADI WA HAKUNA WASICHOWEZA WATOA ELIMU NA MISAADA YA VIFAA VYA KUJISITIRI WAKATI WA HEDHI KWA WASICHANA 6000 MKOANI MTWARA

Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salum Masalanga (katikati) akikabidhi msaada wa pedi kwa Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo, Neema Mohamed chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto)na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga (katikati) akipokea msaada wa pedi kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Wakishuhudia tukio hilo, ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia), mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii Vodacom, Yesaya Mwakifulefule (kushoto) na Mratibu wa Mradi kutoka T-MARC Tanzania, Bi. Dorice Chalambo (wa pili kulia) kwa pamoja wakikabidhi msaada wa pedi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maendeleo chini ya programu ya Hakuna Wasichoweza iliyofadhiliwa na Vodacom na T-MARC. Akishuhudia tukio hilo (katikati) ni Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw. Salumu Masalanga, mradi huo umeanza kufanya kazi mkoa wa Mtwara na Lindi na kusambaa nchi nzima.

Wasichana wa mkoani Mtwara wamefaidika na elimu ya afya pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kujisitiri wakati wa hedhi. Elimu hii na msaada vimetolewa kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza unaotekelezwa na asasi ya T-MARC Tanzania. 

Mradi wa Hakuna Wasichoweza unaendeshwa na asasi ya T-MARC Tanzania kwa ufadhili wa watu wa Marekani kupitia Shirika la Maendeleo la Kimarekani USAID kwa ushirikiano na Vodacom Foundation.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo kwa wasichana walengwa wa mradi huu, Meneja wa Mradi wa Hakuna Wasichoweza, Bi. Doris Chalambo alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wasichana kama njia ya uhakika ya kufanikisha maendeleo ya  jamii na Taifa. ‘’Awamu ya kwanza ya mradi huu imewafikiwa jumla ya wasichana 5000 katika shule za msingi za Mtwara na jumla ya wasichana 1000 walioko nje ya shule katika kata 17. Walengwa wa mradi huu ni wasichana wenye umri wa miaka 9 – 15. Jumla ya shule 24 zimefikiwa na mradi huu ambao pia umetoa mafunzo kwa walimu 40 wa shule na Wakunga wa jadi, makungwi/Nyakanga 34 wanaotoa elimu kwa wasichana wanaobalehe’’.

Aliongeza kuwa lengo kuu la mradi wa Hakuna Wasichoweza ni kukuza viwango vya elimu kwa wasichana Tanzania kwa kuongeza mahudhurio yao shuleni. Lengo hili linafikiwa kwa kutoa msaada wa vifaa vya  kujisitiri katika kipindi cha hedhi kwa wasichana wa shule na walio nje ya shule wanaobalehe, pamoja na kutoa elimu ya afya na kujitambua itakayowasaidia wasichana kuepuka vishawishi vinavyosababisha utoro shuleni na mimba za utotoni.

Pia alisisitiza kwamba elimu hii juu ya masuala ya hedhi itawezesha kuongeza uelewa wa jamii kwa ujumla juu ya umuhimu wa kuwasaidia wasichana ili waweze kuhudhuria masomo yao kwa ufanisi zaidi na kufikia malengo yao kimaisha.

“Asilimia kubwa ya wasichana hutumia njia za asili ili kujisitiri wakati wa hedhi. Mara nyingi njia hizi si salama kiafya na ni chanzo cha magonjwa mbalimbali. Ningependa kutoa wito kwa jamii kwa ujumla kuvunja ukimya juu ya masuala ya hedhi kwani ni kwa uda mrefu kumekuwepo na imani potofu juu ya utumiaji wa vifaa vya kisasa vya kujisitiri wakati wa hedhi” Alimalizia Bi. Doris

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Yessaya Mwakifulefule alisema kuwa elimu inayotolewa na mradi wa Hakuna Wasichoweza italiwezesha Taifa kupunguza kasi ya maambukizi ya mgonjwa ya ngono ikiwemo VVU/UKIMWI miongoni mwa vijana. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mwakifulefule amesema kuwa kila msichana atakuwa akipatiwa pakiti mbili za vifaa hivyo kwa mwezi na zoezi hili litafanyika kwa muda wa miezi mitano mfululizo.

“Tunajivunia kuwa sehemu ya chachu ya maendeleo katika sekta ya elimu hususani mradi huu wa Hakuna Wasichoweza ambao umelenga kunufaisha jumla ya wasichana 6000 waliopo na wasiopo shuleni”.

Naye Mtaalamu wa Masuala ya Misaada kwa jamii kutoka Vodafone, Bi Laura Turkington alisema kuwa mradi unakuza ushiriki wa wadau mbali mbali katika kukuza viwango vya elimu pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa jamii kuhusu changamoto zinazowakabili wasichana katika kipindi cha balehe.

T-MARC inatoa shukurani zake kwa shirika la USAID ambalo limetoa msaada wa dola za Kimarekani laki mbili (200,000)  kufadhili uanzishwaji wa mradi huu pamoja na Vodacom Foundation ambayo imechangia shilingi (TZS) 160 milioni kufanikisha awamu hii ya kwanza ya mradi.  

UBALOZI WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE) WASHEREHEKEA SHEREHE ZA MIAKA 50 MUUNGANO WA TANZANIA

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu,Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) akimpokea mgeni rasmi wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano Tanzania, Mheshimiwa Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa UAE,katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika Hoteli ya Intercontinental,Abu Dhabi..
Balozi Mbarouk akiwa na Chief of Protocol wa UAE Mhe. Shihab Al Faheem.
Balozi Mbarouk akimuongoza Mgeni rasmi Mhe. Dr. Hadef Jawa’n Al Dhaheri, Waziri wa Sheria wa Umoja wa Falme za Kiarabu, pamoja na Mabalozi wanao wakilisha nchi zao hapa UAE kuingia katika ukumbi wa Sherehe.
Balozi Mbarouk na Mama Balozi wakipokea wageni waalikwa
Mhe. Balozi, Mgeni Rasmi na baadhi ya Mabalozi wanao wakilisha nchi zao nchini UAE, wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za UAE na Tanzania

Balozi Mbarouk akitoa hotuba katika sherehe hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa, akiwepo Mhe. Mallallah Mubarak (mwenye kilemba cheupe), aliyewahi kuwa Balozi wa UAE nchini Tanzania.
Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai Bw. Omary Mjenga akiwa na familia yake na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi.
Wageni waalikwa wakipata chakula.
Balozi Mbarouk akiwa na wachezaji mashuhuri wa zamani wa timu za Yanga, simba na Timu ya Taifa, Alluu Ally, Omar Hussein na Yanga Bwanga wanaoishi nchini UAE.
Watanzania wanaoishi nchini UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk akiwa na viongozi wa Chama cha Watanzania wanaoishi UAE.
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi Mdogo Bw. Omary Mjenga akiwa pamoja Mwenyekiti wa Watanzania nchini UAE Bw. Mohammed Sharif na wageni waalikwa.

Hafla ya kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga yafana sana

Mamia ya wakotiliki wamejitokeza kumuaga Askofu wa jimbo la katoliki Dodoma,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga ambaye anahamia Mpanda kwa ajili ya kuendelea na kazi Dini.Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Ibada ilifanyika katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mkoani Dodoma.

Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ambayo alikuwepo Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pina,alikuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki hapa nchini,Mwadhama Polcarp Kardinal Pengo. Pia sherere hiyo ilihudhuriwa na Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.

Katika sherehe hiyo ,Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga. alizawadiwa vitu mbali mbali zikiwemo fedha taslimu. Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga anaondoka rasmi Dodoma kuelekea Mpanda Ijumaa tarehe 2 akipitia Tabora. Amehamishiwa kwa kazi za Kichungaji Jimbo la Mpanda.

Pamoja na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mama Rehema Nchimbi,Papadri na watawa wote wa jimbo la Dodoma kulikuwepo vikundi vya kwaya kutoka makanisa mbalimbali ikiwemo kwaya ya Kanisa analosali Mhe.Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Kwaya ya Shirikisho Hananasifu Dar es Salaam.
Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo (kulia) akipeana mkono na Askofu Gervas John Nyaisonga.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akibusu Pete ya Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisalimiana na Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo.
Askofu mstaafu wa jimbo la Domama Mhashamu Baba Askofu Mathias Isuja.
Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga.
Kiongozi wa kanisa Katoliki hapa nchini Mwadhama Polcarp Kardinali Pengo akiwa na Mhashamu Baba Askofu Gervas John Nyaisonga wakifuatilia vikundi vya kwaya vikitoa burudani.
Waumini na watawa wakiwa katika foeni ya kwenda kumpa mkono wa kila la kheri aliyekuwa Askofu wa jimbo lao ambaye amehamishiwa kitume jimbo la Mpanda Mkoani Rukwa. Kinamama wakatoliki wakiwa wamebeba zawadi ya mashine ya kufulia nguo na Mashine ya kupoozea maji ya kunywa wakati wakielekea kumuaga Mhashamu babab Askofu Gervas Nyaisonga.
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Dodoma wakifuatilia sherehe za kumuaga Askofu Gervas John Nyaisonga Katika viwanja vya kanisa la Mkatifu Paul wa Msalaba.

Vijana wa Skauti wa Kanisa Katoliki Mkoani Dodoma wakitoa salamu kwa Askofu Gervas John Nyaisonga.
Askofu Gervas John Nyaisonga akikagua gwaride la Skauti.

 Picha zote na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati Dodoma.

Mkutano wa 12 wa siku moja wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya afrika mashariki jijini Arusha

Na Othman Khamis Ame
Mataifa wanachama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanapaswa kuzingatia umuhimu wa ulinzi wa pamoja wa eneo lote la Afrika ya Mashariki kwa lengo la kujaribu kudhibiti vitendo vya ugaidi vinavyoonekana kujitokeza katika baadhi ya Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyata wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya alieleza hayo wakati akiuhutubia Mkutano wa 12 wa siku moja wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Arusha (AICC). 
Rais Uhuru Kenyata alisema Mataifa ya Afrika Mashariki hasa pembe ya Bara hilo imekumbwa na wimbi la vitendo vya kigaidi kiasi kwamba huleta hali ya wasi wasi kwa wakaazi wa eneo hilo. Alisema ukosefu wa utulivu katika baadhi ya maeneo ndani ya ukanda wa Bara la Afrika umekuwa ukiipa wakati mgumu jumuiya hiyo kiasi kwamba Mataifa wanachama yanalazimika kufanya kazi kwa pamoja ili kukabiliana na tatizo hilo. 
“ Ukanda wa Afrika Mashariki umekuwa ukikumbwa na vitendo vya kiharamia pamoja na ugaidi jambo ambalo halileti sura nzuri kiasi kwamba huchangia hali ya wasi wasi kwa wana Jumuiya wote “. Alifafanua Rais Uhuru Kenyata.
Akizungumzia suala la kuwa na Ushuru wa Forodha na Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya hiyo Rais Kenyata alisema upo muelekeo mzuri wa suala hilo ambalo linaonekana kupewa Baraka na Viongozi wa Mataifa wanachama. 
Rais Uhuru Kenyata alifahamisha kwamba taratibu na mikakati ya kisheria imekuwa ikiendelea kuchukuliwa na watendaji pamoja na Wataalamu wa Jumuiya hiyo ili kuona suala hilo linafikia muwafaka. 
Alieleza kuwa juhudi za kuwa na ushuru wa forodha na soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizoanza harakati zake kati ya mwaka 2005, 2010 na 2013 zimelenga kustawisha hali ya uchumi ya wananchi wa mataifa shirika wa Jumuiya. 
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki { EAC } aliipongeza Tanzania kwa kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ulioasisiwa na Mataifa mawili huru ya Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. 
Rais Kenyata alisema kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa kielelezo cha kihistoria ndani ya Bara la Afrika pamoja na Mabara mengine Duniani. Alieleza kwamba Afrika Mashariki na Bara zima la Afrika limepata heshima kubwa katika Nyanja za kisiasa kutokana na Muungano wa Tanzania uliofikia nusu karne sasa tofauti na ile miungano mengine iliyoshindwa kumudu hata kwa miezi michache. 
Mapema Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera ameishukuru Tanzania chini ya Rais wake Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa ukarimu wa Wananchi wake. Balozi Dr. Richard Sezibera ukarimu huo unaoendelea kuviwezesha vikao mbali mbali vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika kazi zake za kila siku Ndani ya ardhi ya Tanzania. 
Katika Mkutano huo wa 12 wa Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Majaji Watatu waliapishwa kushika nyadhifa mbali mbali katika baraza la Majaji la Jumuiya hiyo.
Majaji hao ni pamoja na Mh. Edward Mtakangwa, Dr. Aron Regerwa, Jaji Fakih Jundu akiwemo pia Dr. Enos Bukuku aliyeongezewa muda wa kuendelea kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki. 
Halkadhalika Viongozi hao Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa pamoja pia walizindua Mnara wa kumbumbuku ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea karibu miaka ishirini iliyopita. 
Mkutano huo wa 12 wa Viongozi wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umehudhuriwa na Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. 
Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
 Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha { AICC }.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Uhuru Kenyeta wa Kenya akihutubia Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha.
 Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini baadhi ya hati za makubaliano ya Jumuiya hiyo. Kutoka kulia ni Rais Wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiimba wimbo Maalum wa Jumuiya hiyo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya  hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha { AICC }.
 Majaji wapya walioapishwa kushika nyadhifa mbali mbali kwenye Mkutano wa 12 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha. Kutoka Kushoto ni Jaji Edward Mtakangwa, Dr. Anon Regerwa  na Jaji Fakih Jundu.

  Viongozi wa Mtaifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakilizindua Mnara wa kumbumbuku ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea karibu miaka ishirini iliyopita hapo Makao Makuu ya Jumuiya hiyo Arusha Tanzania.vKutoka kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya mabae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rais Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana PierreDamieni Habumuryemi.
 Wakuu waJumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Jumuiya hiyo Mkoani Arusha Tanzania.Kutoka Kushoto waliokaa vitini ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombaza, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza Majaji wapya wa Mahkama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki waliokula kiapo kwenye Mkutano wa 12  wa kuitumikia Jumuiya hiyo Mkoani Arusha. Nyuma yake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.