Friday, August 31, 2012

WA5 WATINGA FAINALI YA SHINDANO LA REDD'S MISS KANDA YA MASHARIKI TALENT, KUUMANA KESHO MORO

 Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Redd's Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.
 Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
 Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall........
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini wengine ni pamoja na mtandano huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd'd, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.....
 Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
 Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea..........
 Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo...
 Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
 Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora ...............
Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone......

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WANAHISA WA TBL

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana.
 Mwanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mchiwa Chedego akiuliza swali wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana.
Mwanahisa Arphaxar Masambu akichangia hoja wakati wa mkutano huo.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria, Steve Kilindo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche.
 Wanahisa wakiperuzi taarifa ya hesabu za kampuni hiyo kwamaka 2012/13
                              
    Sehemu ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo wa mwaka
                         Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wake, Robin Goetzsche
                                           Baadhi ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo
                          Mwanahisa Adrian Makelele akichangia hoja wakati wa mkutano huo
 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche akijibu maswali ya wanahisa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Cleopa Msuya.

                            Mwanahisa Zainab Ramadhan akiuliza swali kuhusu masuala ya kununua hisa
                          Mwenyekiti wa Bodi. Msuya (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari
                                                   Wanahisa  wakipata kifungua kinywa
                                                      Ni msosi kwa kwenda mbele


 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ambayepia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche.wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana.

 Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin O'Flaherty akijadiliana jambo na Katibu wa kiwanda hicho, pamoja na Mkurugenzi wA Uhuiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (katikati).
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBL,  Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (katikati waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wanahisa baada ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa kampuni hiyo kumalizika jana jijini Dar es Salaam.

taarifa kutoka shirikisho la soka nchini (TFF) leo

MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI SEPT 27
Mtihani kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 27 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF. Ada ya mtihani ni dola 50 za Marekani.

Pia Damas Ndumbaro na Ally Mleh wa Manyara Sports Management ambao tayari ni mawakala wanaotambuliwa na FIFA wanatakiwa kufanya mtihani huo kama wanataka kuendelea na uwakala kwa vile muda wa leseni zao za awali umemalizika.

Mawakala wengine ambao ni John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully leseni zao bado ziko hai.

WACHEZAJI 17 WAPINGWA KWENYE USAJILI
Klabu mbalimbali zimewasilisha pingamizi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupinga usajili wa wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu.

Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.

Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.

Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23.

Azam inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani. Nayo Simba inapinga Kelvin Yondani kusajiliwa Yanga kwa maelezo kuwa ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23 mwaka jana.

Vilevile Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga kwa maelezo alisaini mkataba na klabu yao Agosti Mosi mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) na APR ambapo alilipwa dola 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.

Nayo Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.

Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa inatarajia kukutana Jumapili (Septemba 2 mwaka huu) kupitia pingamizi hizo pamoja na usajili wa wachezaji kwa ujumla kwa 2012/2013.

LIGI KUU TANZANIA BARA 2012/2013
Michuano ya Ligi Kuu kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kwa msimu wa 2012/2013 itaanza Septemba 15 mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.

Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).

Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.

MECHI YA UFUNGUZI WA MSIMU WA LIGI 2012/2013
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SERENGETI BOYS KUJIPIMA KWA ASHANTI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyokuwa kambini kujiandaa kwa mechi dhidi ya Kenya itavunja rasmi kambi yake kesho (Jumamosi) kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ashanti United.

Mechi hiyo dhidi ya Ashanti United iliyoko daraja la kwanza itachezwa kuanzia saa 10 jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kwa kiingilio cha sh. 2,000.

Serengeti Boys ilikuwa Septemba 9 mwaka huu icheze na Kenya kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17, lakini Kenya ikajitoa ambapo sasa itacheza na Misri katika raundi ya pili. Mechi ya kwanza itachezwa Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwishoni mwa Septemba, Serengeti Boys itarejea tena kambini kujiandaa kuikabili Misri ambapo kabla inatarajia kupata mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu itakayotangazwa baadaye.

MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR NAYE APATA ITC
Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull FC ya nchini humo.

ITC hiyo ilitumwa jana (Agosti 30 mwaka huu), hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu. Dirisha la usajili wa wachezaji litafungwa rasmi Septemba 4 mwaka huu.

Wachezaji ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba. ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani tayari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshaziomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa kupatikana.

Thursday, August 30, 2012

A NEW ERA FOR MOVIES AS M-NET EXPANDS MOVIE OFFERING ON DStv

DStv audiences across Africa are set to get more movie magic as entertainment powerhouse M-Net embarks on an exciting new chapter! From Monday 1 October 2012, the M-Net movie offering on DStv will be expanding to include eight genre-themed movie channels.  

The 8 movie channels are themed according to movie type and will include M-Net Movies Premiere,
M-Net Movies Comedy, M-Net Movies Family, M-Net Movies Action Plus, M-Net Movies Drama & Romance and M-Net Movies Showcase. Rounding off the M-Net movie line-up are M-Net Movies Action (previously M-Net Action) and M-Net Movies Stars (previously M-Net Stars).   

With the tagline A Movie for Every Mood, audiences can now be assured of a wider choice of the best possible selection of available movies anytime of the day.  

This marks a significant evolution in M-Net’s movie line-up that currently encompasses only 2 generic movie channels. The new range of movie channels, which debuts in October, is specifically designed to ensure easy navigation for audiences so they know just where to find their favourite type of movie. 
To find out more on each channel, please read on… 
  • M-Net Movies Premiere (DStv Channel 103): This where you can find the freshest movies appearing on television for the first time. 5 new movies will be screened every weekend on M-Net Movies Premiere and kicking off every weekend on a Friday is 4 of the 5 blockbusters. 
  • If you like your comedies with a little romance, drama or with slapstick humour, M-Net Movies Comedy (DStv Channel 104) will have you laughing out loud.
  • M-Net Movies Family (DStv Channel 105) is the destination for wholesome entertainment for all ages, featuring animation, musicals, fantasy and feel-good family movies will keep both kids and the young at heart engrossed all day.
  • Viewers can expect a host of blockbuster movies from Action to Westerns, Horror and Sci-Fi on M-Net Movies Action Plus (DStv Channel 106).
  • There is also M-Net Movies Drama & Romance (DStv Channel 107) for those who prefer biographies, thrillers, documentaries and war movies.
  • M-Net Movies Showcase (DStv Channel 108) shines the spotlight on specific movies and directors with exciting festivals, themes and box sets. In addition, viewers get to take control and recommend movies with a special viewer’s choice.
              (MM1 and MM2 will be replaced with the 6 themed movie channels above) 
  • All things action will be available on M-Net Movies Action (DStv Channel 110, previously M-Net Action).
  • And M-Net Movies Stars (DStv Channel 111, previously M-Net Stars) is the channel for young and old alike. It features modern greats and movie favourites from past and present across a variety of genres from comedy to drama and romance.
PLUS: From the month of October, viewers can look forward to festivals, themed evenings and a viewer’s choice on selected nights across all the channels. 

For more information on these exciting new channels, log on to www.dstv.com!  
DStv subscribers can also get information on the upcoming DStv channel re-numbering initiative on the DStv website. With DStv launching several new channels in the recent past, the channel re-numbering initiative is focused on ensuring that all channels are grouped as relevant by genres. 

This will mean that viewers can find the channels that they are looking for easily and quickly. This update of the channel numbers will also allow for future channel growth on DStv.  

And to help viewers navigate the channel number changes, DStv is also launching a dedicated channel (DStv channel 198), hosted by Big Brother star IK Osakioduwa.  Alternatively simply press OK on your DStv remote and click on the Renumbering section for info. 

So sit back, relax and get ready for a world of great movie entertainment…courtesy of M-Net and only on DStv!

Wednesday, August 29, 2012

Shoo ya Evans Bukuku ilivyokuwa jana

 Mchekeshaji Maarufu Nchini kutoka Vuvuzela Entertainment,Evans Bukuku akikafanya vitu vyake usiku wa kuamkia leo katika kiota cha maraha cha Nyumbani Lounge,Namanga jiji Dar wakati wa Shoo yake ya kuvunja mbavu za watu (kuchekesha katika stand up comedy).
 Evans Bukuku akiendelea kuchana mbavu za watu kwa vituko vyake wakati wa Shoo yake ya kuvunja mbavu za watu (kuchekesha katika stand up comedy) iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cha maraha cha Nyumbani Lounge,jijini Dar.
 Evans Bukuku akimuuliza mmoja wa wadau wake swali la kizushi kuhusiana na mambo ya kuchimba dawa safarini.
 Dogo Pepe wa Vuvuzela akionyesha umahiri wake wa kuvunja watu mbavu kwa kucheka wakati wa shoo yao iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cha maraha cha Nyumbani Lounge,jijini Dar.
 MC wa Shoo hiyo alikuwa ni Taji Liundi nae haachi kuchekesha awapo stejini.
 Enika akiimba nyimbo za vichekesho.
Mmoja wa Wadau wakubwa wa Stand up Comedy za Evans Bukuku,aitwaye Ester Ulaya nae hakuwa nyuma kuotoa kituko chake wakati shoo hiyo ikiendelea.
 Kila aliefika ukumbini hapo hakuacha kucheka kwani vichekesho vilinoga ile mbaya.

Tuesday, August 28, 2012

Notting Hill Carnival London

Salam,

Urban Pulse Creative na Freddy Macha wanakuletea taswira ya Notting Hill Carnival iliyofanyika jana tarehe 27.8.12.

Kihistoria sherehe hii ilifanywa siku 40 kabla ya Pasaka kipindi kinachoitwa LENT ( “Kwaresima“ )ambapo waumini wa Kikristo hujinyima, husali, hutoa sadaka, huomba msamaha, huungama makosa , kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa kufunga (kama wafanyavyo Wayahudi na pia Waislamu kabla ya Idd El Fitri). Carnival hushereherekewa kidesturi mwezi wa pili na watatu (Brazil, Ujerumani, nk) lakini nchi mbalimbali ( mathalan Uingereza, Japan, Cape Verde nk) zimegeuza tarehe kufuatana na tamaduni au matakwa yao. London ni Jumapili na Jumatatu ya mwisho wa mwezi Agosti ambapo hamna kazi (huitwa Bank Holiday).

Carnival ni neno lenye asili ya Kilatini "Carne Vale" –maana yake “Kwaheri” (Vale) “Nyama” (Carne)

Baadhi ya nchi maarufu kwa Carnival

1. Brazil – Rio ni Samba na Bahia ni siku tano za muziki juu ya malori makubwa- Feb na March

2. Trinidad na Tobago- Mwezi Feb na March kabla ya Pasaka, athiri sana Carnival ya London kwa muziki wake wa Soca na ngoma za chuma („steel pans“

3. Nchi za Kiafrika zenye asilia ya Kireno- husheherekea Carnival, Maputo, Luanda na visiwa vya Cape Verde- ambapo Carnival inaitwa “Mindelo“....(mji mkuu wa Cape Verde). Carnival ya Mindelo ni maarufu na kubwa kuliko zote Afrika.


4. Asakusa, Japan. Carnival la Japan lenye mahadhi ya Samba na Brazil kila mwaka mwisho wa mwezi wa Agosti. Vutia watu laki moja.


Muasisi mkuu wa Carnival ya London ni Claudia Jones- mwanamke mwenye asilia ya Trinidad aliyehamia Uingereza mwaka 1955. Alikuwa mwanahabari aliyepigania haki za watu weusi. Mwaka 1959 alianzisha Carnival ya kwanza katika kitongoji cha St Pacrais. Sherehe hii ilivutia sana Habari na ilitangazwa katika BBC. Claudia Jones alifariki mwaka 1964 kutokana na maradhi ya moyo na kifua kikuu. Amezikwa kando ya kaburi la Karl Marx, High Gate, London kaskazini.

Asanteni,

Urban Pulse wakishirikiana na Freddy macha

Freddy Macha akipiga Filimbi.
Freddy Macha na Frank Katika Notting Hill Carnival.
Freddy Macha na Wadau wakisherekea Carnival.
Furaha kila sehemu.
Mh Balozi Kallaghe na Frank kwenye Notting Hill Carnival.
Ni furaha na shangwe tu kwa kila mtu.
Hata watu wazima walikuwepo ndani ya Carnival huku wakipata mambo ya Mbwa Moto (Hot Dog).
Polisi katika pozi.
watu wakumwaga.