Sunday, February 18, 2018

WAZIRI JAFO ABAINI KUWEPO KWA WANAFUNZI 472 NA WALIMU WA SHULE SEKONDARI MAKULUNGE WILAYANI KISARAWE KUKABILIWA NA TATIZO LA VYOO

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Makulunge iliyopo kata ya kiluvuya katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea shule na kusikiliza changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Waziri wan chi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo akizungumza na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziaara yake ya kikazi aliyoifanya katika kaata ya Kiluvya kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Mmoja wa walimu wa shule ya sekondari Makuunge Ester Matemu akizungumza kuhusiana na changamoto ambayo ianwakabili ya ukosefu wa vyoo,(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

……………………………………………………………………….

VICTOR MASANGU, KISARAWE 

WANAFUNZI wapatao 472 na walimu zaidi ya 25 katika shule ya sekondari Makulunge iliyopo katika kata ya kiluvya Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa sasa wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo UTI,na kipindu pindu kutokana na vyoo ambavyo wanavitumia kwa sasa vipo katika mazingira hatarishi na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo wakati mwingine inawalazimu kwenda kujisaidia katika maeneo mengine.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ambayo imefanyika katika kata ya Kiluvya na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ambapo baada ya kutembelea shule hiyo ya sekondari ameweza kubaini kuwepo kwa mapungufu makubwa ya walimu wa shule hiyo kutokuwa na choo chao hivyo kuchangia na wanafunzi wao.

Wakizungumza kwa masikitiko wanafunzi hao akiwemo Waziri Mwinjuma na Zuwena Mohamed wamebainisha kwamba kwa sasa wanapata shida kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira magumu ya miundombinu ya vyoo na kwamba kunahatarisha usalama wa afya zao kutoka na kukithiri kwa uchafu pamoja na miundimbinu kuwa mibovu na baadhi ya vyoo hazina milango na sehemu za ukuta zimeanza kubomoka.

Walisema kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya wanafunzi wengine hususan wa kike wanapata ugonjwa wa UTI kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na matundu ya vyoo yaliyopo hivyo wakati mwingine wanafunzi kujisaidia sehemu ambayo sio salama kabisa.

“Kwa kweli shule yetu kwa sasa tunakabiliwa na chanagmoo ya vyoo kwani ukizingatia idadi ya wanafunzi tuliopo ni wengi sana, na matundu ya vyoo yaliyopo ni machache maana kwa upande wa wavulana matundu yapo manne tu, na kwa wasichana hivyo hivyo, kwa hiyo tunachangai vyoo vyetu pamaja na walimu na ukizingatia vipo katika mazingira machafu,havina milango na miundombinu yake ni mibovu, walisema wanafunzi hao.

Nao baadhi ya walimu hao hususan wakike wakitoa kero hiyo akiwemo Merry Godfrey na Ester Matemu wamesema kwamba kwa upande wao hawana vyoo kabisa kwani vilivyopo ni vyawaanafunzi na vipo katika hali mbaya hivyo inawalazimu kuchangia na wanafunzi wao na wakati mwingine wanaogopa kuingia kujisaidia kutokana na kuwepo kwa wadudu wakali kama vile nyoka.

Aidha walimu hao kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo wameiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha wanawajengea vyoo ili waweze kuwa katika mazingira ambayo ni rafiki kwa upande wao kuliko ilivyo kwa sasa kwani ni hatari kwa usalama wa afya zao. 

Kufuatia kuwepo kwa kilio hicho Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha wanaanza jitihada za ujenzi wa matundu ya vyoo mara moja kwa lengo la kuweza kuwaepusha wanafunzi na walimu wa shule hiyo wasiweze kupata magonjwa ya mlipuko na madhara mengine.

“Hii hali kwa kweli mimi kwa upande wangu siwezi kuivumilia hata kidogo maana haiwezekani watendaji mpo na mnashindwa kutekeleza majukumu yenu ipasavyo, haiwezekana shule kama hiii ya sekondari ya makulunge walimu kukosa vyoo, hii ni hatari sana na wanafunzi vyoo vyao navyo vipo katika mazingira hatarishi hivyo namuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kisarawe kulifanyia kazi suala hili haraka iwezekanavyo kwa kujenga vyoo,”alisema Jafo.

Pia Waziri Jafo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi wa ngazi zote hivyo asingependa kuona wanafunzi na walimu wanasoma katika mazingira magumu, na kuahidi kulivaia njuga sualaa hilo kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika suala zima la elimu.

SHULE ya sekondari ya Makuiunge iliyopo katika halmasauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambayo ina jumla ya wanafunzi wapatao 472 inakabiliwa na uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo, pamoja na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo kunahatarisha usalama wa walimu na wanafunzi wao katika suala zima la afya zao kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko.

No comments: