Monday, February 26, 2018

SHAHIDI ADAI WEMA ANATUMIA BANGI KAMA STAREHE

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, msanii wa Filamu na Miss Tanzania mwaka 2006  Wema Sepetu  alimueleza askari polisi kuwa anatumia bangi kama starehe.

Shahidi wa tatu wa upande wa mashtaka, WP 6441 DC Mary (35) ameyaeleza hayo leo Februari 26 mwaka huu alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wafanyakazi wake wawili.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, WP Mary amedai, Februari 4, 2017 alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi OC CID Denis Mujumba kumtoa Wema mahabusu na kwenda nyumbani kwake kufanya upekezi.

Amedai waliondoka  yeye, OC CID Mujumba, Inspekta Wille, Koplo Robert na DC Hassan na kuwa wkiwaa njiani alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazo mkabili kama anahusika na uuzaji wa dawa za kulevya ama kutumia.

Shahidi huyo alieleza,  Wema alimjibu kuwa yeye hajishughulishi na uuzaji wa dawa za kulevya ila anatumia bangi kama starehe.Alidai kuwa alimuuliza Wema kuwa ni lini ilikuwa mara mwisho kutumia bangi  nakwamba siku hiyo ilikuwa Jumamosi ya Februari 4,mwaka 2017 na Wema alimwambia kuwa  Mara ya mwisho kutumia bangi ilikuwa siku ya Jumatatu.

Alieleza wakati akimuuliza hayo, walikuwa njiani kuelekea nyumbani kwa Wema na  walipofika waligonga geti na likafunguliwa na mfanyakazi wake mmoja, Amedai walipoingia ndani ndipo walimkuta mfanyakazi mwingine wa Wema,ambapo kabla ya upekuzi Wema aliomba dada yake Nuru Sepetu apigiwe simu ili awepo katika upekuzi, alifika pamoja na mjumbe Steven Ndoho.

Shahidi huyo alidai baada ya watu hao kufika dada yake Wema,Nuru aliomba kuwapekua kwa sababu wanawea kumuwekea Wema kitu chochote.
Alidai walianza upekuzi jikoni ambapo walikuta msokoto mmoja wa bangi na Rizla moja kwenye shelfu za kabati.

Walipekuwa sebuleni hawakukuta kitu chochote, katika chumba cha Wema cha kuvalia nguo na viatu walikuta kipisi kimoja cha bangi dirishani.Pia walipekuwa katika chumba cha wafanyakazi walikuta kipisi kimoja cha bangi ndani ya kiberiti katika droo ya kitanda.

Ushahidi huyo alieleza kuwa baada ya upekuzi huo wote walitoka nje na kuandika maelezo ambapo Afande Wille alijaza hati ya ukamataji mali na wakarejea polisi.Aliongeza kudai kuwa February 8,mwaka 2017 saa 4 asubuhi Inspekta Wille alimpatia maelekezo ya kumpeleka Wema kuchukuliwa sampuli ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Aliendelea kudai baada ya kifuata taratibu zote na kuchukua alama za sampuli ya mkojo, walirudi  Polisi.Wakili Albert Msando baada ya ushahidi huyo kutokaushahidi, alimuuliza kati ya mshtakiwa wa pili na wa tatu  ambapo ni wafanyakazi wa Wema alimkamata na bangi.

WP Mary alieleza kuwa hakuna aliyemkamata .Wakili Msando  unakiri ushahidi wao ni kuhusu upekuzi katika nyumbani ya Wema.

WP Mary ninakiri

Wakili Msando ulihusika mahali popote kuchukua maelezo ya washtakiwa namba mbili na tatu.

WP Mary sikuhusika

 Mbali na Wema washtakiwa wengine in Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Katika kesi hiyo inadaiwa  kuwa  Februari 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, mwaka 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.

No comments: