Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa
kwenye maduka ya watu binafsi kwani serikali haitaki kuingia kwenye
matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu zake za kutolewa huduma ya
afya.
Dk.
Ndugulile amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye
maduka ya watu binafsi wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya ya
Shinyanga, Februari 21,2018 akikagua shughuli za huduma za afya
zinavyotolewa kwa wananchi pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na
Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa.
Dk.
Ndugulile alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2017-18) serikali
kwenye bajeti ya wizara hiyo ya afya imetenga jumla ya shilingi bilioni
270, tofauti na mwaka wa fedha (2015-16) ambapo zilikuwa milioni 30
hivyo hawatarajii kusikia sehemu za kutolewa huduma zake za kiafya kuwa
zina upungufu wa dawa.
Akiwa
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha Afya cha
Kambarage manispaa ya Shinyanga na kukagua bohari za dawa, Dk. Ndugulile
alitoa tahadhari kwa wauguzi kuwa ni marufuku dawa hizo za serikali
kukutwa zinauzwa kwenye maduka ya watu binafsi na ikibainika
watachukuliwa hatua kali.“Serikali ya awamu hii ya tano imedhamiria
kuboresha huduma za afya hapa nchini, na ndio maana hata bajeti yake
imetolewa ni ya fedha nyingi hivyo sisi kama wizara husika hatutarajii
kuwepo kwa upungufu wa dawa kwenye sehemu za huduma za afya”,alieleza.
Pia
aliwataka wananchi kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa,
ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu hasa pale watakapougua na
kukutwa hawana pesa ambapo wataweza kutibiwa kwa shilingi hiyo 10,000/=
ili kuokoa maisha yao.
Naye
kiongozi wa Mradi wa Maendeleo ya Tuimarishe Afya (HPSS) kutoka makao
makuu Dodoma Profesa Manoris Meshack, alisema mradi huo wa Bima ya afya
ya jamii CHF ulianza mwaka 2011 mkoani Dodoma, na baada ya kufanya
vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga na
Morogoro.
Alitaja
takwimu za kaya katika mikoa hiyo mitatu zilizojiunga na CHF
iliyoboreshwa hadi sasa kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya kaya
1,220,413, na hadi kufikia Disemba 2017 kupitia uandikishaji wa
wanachma wamekusanya shilingi bilioni 7,027,605,547. ambapo shilingi
bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Nao
baadhi ya wazee kati ya kumi wasiojiweza ambao walikatiwa Bima hiyo ya
Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa na Naibu Waziri huyo wakati wa ziara
hiyo,Mohamed Mkumbola na Regina Kulwa waliipongeza serikali kwa kujali
makundi hayo maalumu, na kuomba wazee wote wakatiwe Bima hiyo pamoja na
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wajiunge.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa katika bohari ya dawa kwenye kituo cha afya
kata ya Kambarage mjini Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu na Steve
Kanyefu
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa ameshika kopo la dawa katika bohari ya dawa
kwenye kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga na kusisitiza kuwa dawa
zenye nembo ya dawa za serikali MSD hazitakiwi kutoka nje ya hospitali
za serikali.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akimsalimia mgonjwa katika kituo cha Afya Kambarage
mjini Shinyanga huku akiangalia dawa alizopewa mgonjwa na kupiga
marufuku wagonjwa kuambiwa dawa hakuna na kwenda kununua kwenye maduka
ya dawa ya watu binafsi.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulileakikagua chumba cha upasuaji katika kituo cha afya
Kambarage mjini Shinyanga, na kuagiza jengo hilo lifanyiwe marekebisho
ili kuendana na hadhi ya chumba cha upasuaji, sababu haliridhishi
kuendana na huduma ambayo itakuwa ikitolewa.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akitoka kwenye jengo la chumba cha upasuaji katika
kituo cha afya kata ya Kambarage mjini Shinyanga na kuacha maagizo
lifanywe marekebisho.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akihamasisha wananchi wa kata ya Kambarage mjini
Shinyanga kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwa
na uhakika wa kupata matibabu pale watakapo patwa na ugonjwa gafla
harafu hawana pesa ambapo bima hiyo itasaidia kupata tiba na kuokoa
maisha yao.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akitoa hamasa kwa wananchi kwa vitendo juu ya ukataji
wa Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kukata Bima hiyo papo
hapo, na hapo akipigwa picha na Ofisa uandikishaji CHF Kata hiyo ya
Kambarage Marry Budigila.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akijaza taarifa zake wakati akiendelea na zoezi la
ukataji Bima hiyo ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, na kutoa hamasa
kwa wanachi kujiunga nayo huku akikatia watu 10 bima hiyo ambao
hawajiwezi wakiwamo wazee.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa hamasa ya wananchi
kujiunga na bima hiyo ya Afya CHF iliyoboreshwa, pamoja na kusaidia
kuwaunga watu watano wasiojiweza kwenye Bima hiyo.Matiro alimuunga mkono
Naibu waziri kwa kutoa elimu kwa vitendo huku akiwataka wadau
kujitokeza kusaidia kukatia Bima hiyo watu waliokatika makundi maalumu.
Ofisa
uandikishaji wa Bima ya afya CHF iliyoboreshwa Jackson Njau, akiendelea
na zoezi la kuingiza taarifa kwa wananchi ambao wamejitokeza kujiunga
na Bima hiyo ya afya ya jamii.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akimkabidhi Kadi ya CHF Mzee Mohamed Mkumbola ambaye
ni miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akimkabidhi kadi ya CHF bi Regina Kulwa ambaye ni
miongoni mwa watu 10 wasiojiweza aliowakatia Bima hiyo.
Mzee
Mohamed Mkumbola akitoa shukrani kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakatia
kadi ya bima ya afya wazee wasiojiweza, huku akimuomba kumsaidia kupata
madai yake katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga anayodai mara
baada ya kuacha kufanya kazi, ombi ambalo liliahidiwa kushughulikiwa na
kukabidhiwa majukumu hayo katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert
Msovela.
Baadhi
ya wananchi wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga, wakisikiliza nasaha
kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile juu ya kujiunga na Bima hiyo ya afya CHF,
ambayo itakuwa msaada mkubwa katika kuokoa maisha yao pale
watakapopatwa na magonjwa na kukutwa hawana pesa.
Baadhi
ya wananchi wa kata ya Kambarage mjini Shinyanga wakiwa kwenye mkutano
wa hamasa ya kujiunga na Bima ya CHF iliyoboreshwa, ambapo mtu akikata
shilingi 10,000 yeye na familia yake watu watano watatibiwa bure kwa
mwaka mzima.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga
kuangalia namna huduma za afya zinavyotolewa dhidi ya wananchi, huku
upande wa mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro, na mkono wa kulia ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk.
Geogre Masigati.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia huduma ya mfumo wa malipo ya kielekroniki
kwenye hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, na kukuta mfumo huo
haufanyi kazi ambapo hapo awali aliambiwa unafanya kazi na kusababisha
kuwepo na upotevu wa fedha.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia majalada ya wagonjwa na namna
wanavyopatiwa huduma za matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Shinyanga.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akimsalimia mzazi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa
wa Shinyanga, na kumuliza maswali juu ya huduma anazopewa ikiwemo kama
aliagizwa kwenda kununua dawa yoyote ama vifaa kwa ajili ya kujifunguli
na kupewa majibu kuwa kahudumiwa vizuri na vitu vyote kapewa hapo
hospitalini.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akipitia taarifa ya hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa
wa Shinyanga na kubaini kuna upotevu mkubwa wa pesa kutokana na
kutofanya kazi mfumo wa ukusanyaji pesa kwa njia ya kielektroniki na
kuagiza ufanye kazi haraka sana.
Baadhi
ya wauguzi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakisikiliza
ujumbe kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na kusisitizwa watoe tiba vizuri kwa
wananchi pamoja na kutoa kauli nzuri kwa wagonjwa.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro, akimkaribisha Naibu Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile
kusikiliza taarifa za huduma ya afya kutoka kwa wakurugenzi wa
halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na Shinyanga vijijini
Mkurugenzi
wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akisoma
taarifa ya huduma ya afya ya manispaa hiyo. Alisema katika manispaa hiyo
kuna vituo Viwili vya afya, zahanati 28 na hakuna tatizo la uhaba wa
dawa,na kutaja takwimu za Kaya zilizojiunga na bima ya afya ya jimii CHF
kuwa ni Kaya 7,136 sawa na asilimia 21.2 ya kaya zote, na kaya zilizo
hai hadi sasa ni 3,781na zinaendelea kupata huduma ya matibabu sawa na
asilimia 11.2, ambapo lengo la kitaifa ni kufikia asilimia 30 na
kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na bima hiyo
ya CHF.
Mkurugenzi
wa halmashuari ya Shinyanga vijijini Bakari Kasinyo, akisoma taarifa ya
huduma za afya kwenye halmshauri hiyo ambapo alisema kuna vituo vya
afya vitano na zahanati 35 na hakuna tatizo la dawa na kutaja idadi ya
kaya zilizojiunga na bima ya CHF iliyoboreshwa,kuwa ni 10,615 kati ya
kaya 59,321 sawa na asilimia 11.3 ,na kubainisha mkakati ulipo ni
kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na Bima hiyo ya CHF.
Kiongozi
wa mradi wa maendeleo ya tuimarishe afya (HPSS) kutoka makao mkuu
Dodoma Prof Manoris Meshack, akisoma taarifa ya mradi huo wa Bima ya
afya ya jamii CHF kuwa ulianza mwaka 2011 mkoani Dodoma, na baada ya
kufanya vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili ya Shinyanga na
Morogoro.
Alitaja
takwimu za kaya katika mikoa hiyo mitatu zilizojiunga na CHF
iliyoboreshwa hadi sasa kuwa ni 318,334 sawa na asilimia 26 kati ya Kaya
1,220,413 na hadi kufikia Dicemba 2017 kupitia uandikishaji wa wanachma
wamekusanya shilingi bilioni 7,027,605,547. ambapo shilingi bilioni
2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Naibu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
wakikagua Jengo la Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga ambayo
inajengwa katika kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa nje wa jengo jipya la hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Marco Maduhu na Steve Kanyefu
No comments:
Post a Comment