Thursday, January 18, 2018

DKT. NDUGULILE AZINDUA SACOSS YA WANAWAKE MKOANI MBEYA

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tea Masala wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Tomato Sauce wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa aevaa koti lililotengenezwa na wajasiliamali wadogo wakati alipotembelea moja ya Kikundi cha wanawake wajasiriamali kilichopo Manispaa ya Jiji la Mbeya, mkoani Mbeya, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na wanawake wajasiliamali walioshiriki kikao cha siku moja katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya huku akiwa ameshika moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali hao wakati wa ziara yake iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa motisha kwa Vikundi ‘walelewa’ chenye mtaji mdogo na kuwaunganisha kwa ‘Vikundi Mlezi’ ambacho mtaji wake umeimarika ili waweze kusaidia katika kukuza biashara zao wakati wa ziara yake Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanyakazi za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa mkopo wa Shillingi Million 1 kwa mmoja wa mwananchama wa Saccoss ya wanawake Mbeya wakati wa Uzunduzi wa Saccoss hiyo wakati wa ziara yake ya Mkoani Mbeya iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi za maendeleo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amezidua Saccoss ya Wanawake katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo ili kuweza kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupa mbinu mbalimbali za kufanikisha matarajio yao na kupata maendeleo.

Ameizindua Saccoss hiyo Mkoani Mbeya wakati akiitambulisha Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika Manispaa ya ya Jiji la Mbeya yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana kati yao wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo linaenda sambamba na uwezeshwaji wa wanawake katika kuwashirikisha wanawake wenyewe katika kuibua miradi na kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya fursa na weledi wa wananchi wenyewe. 

Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake kuwaweza kuanzisha vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na kuzalisha bidhaa zitakazo uzwa ndani na nje ya mkoa wa Mbeya na hivyo kuutangaza mkoa kupitia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia ubunifu na rasilimali zilizopo.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saxccoss ya Wanawake ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali kiuchumi na kuwashirikisha wajasiliamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na vifaa.

“Niseme uzinduzi wa Saccoss hii kwa ajili ya wajasiriamali ni muhimu kwenu wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na mitaji ya kufanya shughuli zao pamoja na kuwawezesha kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara na kusaidia kuhamasisha Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa wanawake na vijana ambazo zitatumika kama mtaji wenye masharti nafuu wa kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw. amesema kuwa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ na Saccoss ya wanawake itasaidia kuwainua wanawake ikiwa halmashauri zitashirikiana na wadau wa maendeleo kuwawezesha wanawake kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kumwahakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa wa Mbeya.

Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Manispaa ya Jiji la Mbeya Bi. ameishukuru Serikali kwa kuzindua Progarmu ya kikundi Mlezi na kuanzishwa kwa Saccoss hiyo utakaowawezesha wanawake kusaidiana katika kuanzisha na kuboresha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) anafanya ziara mkoani Mbeya kwa kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kuchangia lengo la kuanzisha biashara ndogo na za kati kwa manufaa ya Taifa. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

No comments: