Sunday, July 31, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Sia Pius ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka Miss Sinza na kufaikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali zilizotolewa na wadhamini wa shindano hilo.https://youtu.be/H3s12MVjf0k  

SIMU.TV: Timu ya Afrika media Group imefanikiwa kutoa sare ya goli moja kwa moja ilipocheza na timu ya umoja wa watuma salamu. https://youtu.be/1c9YuGRp1ek

SIMU.TV: Rais DR. John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa mikoa na wabunge kuwa wabunifu katika miradi mbalimbali ya Maendeleo. https://youtu.be/nAZ1a--vz5M

SIMU.TV: Waziri wa fedha na Mipango Dr Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na makamu wa rais wa benki ya afrika AfDB. https://youtu.be/6DW4H7-_e8s

SIMU.TV: Chuo cha sayansi ya ardhi kikishirikiana na chuo kikuu cha Dodoma vimeanzisha mradi wa kuteteza taka ngumu ili kulinda mazingira. https://youtu.be/XURlWP2taDY

SIMU.TV: Idara ya uhamiaji Tanzania ikishirikiana na idara ya uhamiaji nchini Zambia wameanzisha utaratibu wa kuthibiti nyaraka bandia za kusafiria katika nchi hizi.https://youtu.be/linhLJKIr18

SIMU.TV: Naibu waziri wa kilimo ufugaji na uvuvi amewaagiza maafisa ardhi katenga maeneo kwa ajili ya wafugaji wa samaki. https://youtu.be/Mm9msIFIg68

SIMU.TV: Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Kinondoni limemkamata mkazi mmoja aliyekua kajiunganishia huduma ya umeme kwa njia za wizi.https://youtu.be/_Fca8AFRCyA

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zalote Steven, ameagiza kukamatwa kwa watumishi wa umma wanaoshirikiana na wananchi katika vitendo vya uvuvi haramu;https://youtu.be/6z8OpzBMxpo

SIMU.TV: Wakazi wa mkoa wa Geita wameombwa kujitokeza kwa wingi kuchangia katika hospitali ya mkoa huo ambapo mpaka sasa zimebakia chupa nne;https://youtu.be/bcrz2Uf4FKc

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli amewaagiza viongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha kituo cha mabasi cha Igunga kinaanza kufanya kazi ifikapo Agosti 1 mwaka huu;https://youtu.be/B94FeFXDWOg

Rais Dr Magufuli amemtaka mkandarasi anayejenga barabara wilayani Manyoni, kuhakikisha anarudi kazini na kumaliza haraka ujenzi wa barabara hiyo;https://youtu.be/O_Ob6ltSyv8

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wanaoishi pembezoni mwa Barabara moja kuelekea wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameilalamikia serikali kwa kuchelewa kuwalipa fidia zao za kupisha ujenzi wa barabara; https://youtu.be/mSLzJhmYVt8

SIMU.TV: Serikali imesema itaifanyia ukarabati barabara ya Lusahunga kwenda Rusumo mkoani Kagera ambayo imeharibiwa sana kutokana na msongamano wa Malori;https://youtu.be/st5iKipEzkE

SIMU.TV: Zaidi ya wapangaji 1000 wamekosa makazi baada ya kulazimika kuondoka kwenye Nyumba zinazomilikiwa na CDA mkoani Dodoma kwa kushindwa kulipa kodi;https://youtu.be/8bb9uA3coH0

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango Dr Philip Mpango, amekutana na makamu wa rais wa benki ya maendeleo Afrika na kumshukuru kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali; https://youtu.be/MfXq-3-HTog

SIMU.TV: Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene amewasimamisha kazi afisa elimu pamoja na afisa elimu sekondari mkoani Mbeya baada ya wanafunzi wilayani Ileje kulala chini; https://youtu.be/BPKnpcpCA-M

SIMU.TV: Washiriki wa shindano la Klabu Raha Leo wametakiwa kuongeza bidii na kutokata tama kama wanataka kuibuka na ushindi katika shindano hilo;https://youtu.be/hTQJ2Mx993U

SIMU.TV: Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amelazimika kuhairisha kambi ya timu hiyo baada ya kuombwa kufanya hivyo na klabu mbalimbali nchini;https://youtu.be/LHxHulgh7sI

SIMU.TV: Wasanii wa Tanzania wameshauriwa kurekodi nyimbo zao kwa kutumia studio za hapa nchini baada ya kwenda kufanya hivyo nchi za nje; https://youtu.be/IaWjsJwufI0

SIMU.TV: Meya wa manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob, amewataka wachezaji wa timu ya KMC ambayo inamilikiwa na manispaa hiyo kuheshimu mikataba yao ya kazi;https://youtu.be/NTy5Ok8vvhQ

SIMU.TV: Tamasha la Tumaini Jipya lenye lengo la kuifundisha jamii kuwa na malezi bora kwa familia zao linatarajia kufanyika hii leo jijini Dar Es salaam katika uwanja wa Uhuru;https://youtu.be/pBsWgyH0unw

SIMU.TV: Mtunzi wa kitabu cha Historia ya soka la Tanzania Peter Ching’ole, amewataka watanzania kuwa na desturi ya kufanya utafiti ili waweze kuwa watunzi wazuri wa vitabu;https://youtu.be/DmISLH-WtK0

SIMU.TV: Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameanza kufungua akaunti ya magoli akiwa na klabu yake hiyo mpya baada ya hapo jana kufanikiwa kuisawazishia timu yake dhidi ya Galatasaray; https://youtu.be/sMtBAtwN7l0

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MKUTANO TINDE, ISAKA NA KAHAMA MKOANI SHINYANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea Nzega mkoa Tabora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza jukwaani wimbo wa kwaya ya Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT- Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga kabla ya Kuhutubia mamia ya wakazi Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli mara baada ya kuwasalimia wananchi waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais katika viwanja hivyo vya Kahama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia wa wakazi wa Isaka mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa zamani wa Kahama James Lembeli ambaye ni mwanachama wa Chadema mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akicheza pamoja na Wanakwaya wa Haleluya Kuu kutoka Kanisa la KKKT- Usharika wa Yeru Ndala Shinyanga mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano Kahama mjini mkoani Shinyanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuoneshwa picha na kijana mmoja aliyeishika picha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Tinde mkoani Sinyanga. PICHA NA IKULU

DC IKUNGI AMTAKA DED WAKE KUMPA TAARIFA YA KUTOANZA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU ZINAZOGHARAMIWA NA BENKI YA DUNIA

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa uchagiaji wa damu salama,mfuko wa afya ya jamii(CHF) pamoja na daftari la ufuatiliaji akina mama wajawazito uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Minyughe,wilayani Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida,Miraji Mtaturu(wa kwanza kushoto) akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi(CCM), Elibariki Kingu daftari la ufuatiliaji akina mama wajawazito,mara baada ya kuzindua mpango huo uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Minyughe,wilayani hapa.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Minyughe waliohudhuria uzinduzi wa uchangiaji wa damu salama lililofanyika kiwilaya katika kata ya Minyughe,tarafa ya Ihanja,wilaya ya Ikungi.
Mmoja wa wataalamu wa kitengo cha kukusanya damu salama akiwa katika jingo la darasa moja la shule ya msingi Minyughe,tarafa ya Ihanja wakati wa uzinduzi wa uchangiaji wa damu salama,mfuko wa afya ya jamii(CHF) na daftari la ufuatliji wajawazito kuhudhuria kliniki akikusanya chupa za damu zilizotolewa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata aya Minyughe. (Picha Na Jumbe Ismailly).

Na. Jumbe Ismailly, Ikungi 


MKUU wa Wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuwa ifikapo Agosti mwaka huu ampatie taarifa za sababu zilizochangia Mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa nyumba sita za shule ya msingi Minyughe kutoanza kazi kwa wakati uliopangwa ya ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Minyughe licha ya kupokea malipo ya kazi hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya, Miraji Mtaturu alitoa agizo hilo katika Kijiji cha Minyughe, muda mfupi baada ya uzinduzi wa uchangiaji wa damu salama, mfuko wa afya ya jamii (CHF) pamoja na daftari la ufuatiliaji akina mama wajawazito uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Minyughe,wilayani Ikungi.

Kwa mujibu wa Mtaturu kuchelewa kuanza kwa shughuli ya ujenzi huo wa nyumba za walimu utasababisha pia ukamilishaji wa nyumba hizo kutokamilika pia kwa wakati na huduma kwa walimu kucheleweshwa.

Akitoa taarifa kwa Mkuu huyo wa wilaya juu ya Mkandarasi kutoanza kazi za ujenzi wa nyumba hizo licha ya kupokea fedha za malipo ya shughuli hiyo, Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu alisema miradi inayofadhiliwa na Benki ya dunia yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 750 katika Halmashauri hiyo imekwamishwa na Mkandarasi licha ya kulipwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo za walimu, jambo linalosababisha walimu wa shule hizo kuishi katika nyumba zisizo na ubora unaotakiwa.

Hata hivyo Mbunge huyo kijana aliweka bayana kwamba baada ya kuonekana kila Mkandarasi anayetenda anatoa bei ya juu, yeye alimshawishi Waziri wa Tamisemi ili aweze kuiruhusu Halmashauri ifanye taratibu za manunuzi yenyewe ili kufanikisha shughuli hiyo iweze kufanyika mapema badala ya kuendelea kutegemea utaratibu wa wizara ambao unatumia fedha nyingi huku kukiwa na mwanya wa fedha za serikali kuliwa na baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Athumani Salumu akitoa utetezi wa sababu za kutoanza kwa shughuli hizo za ujenzi ni pamoja na ukosefu wa mchanga wa kuanzisha ujenzi wa nyumba hizo.

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAANGWA LEO JIJINI DAR

 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga liwa katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakiamuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya kufika. 
 Jeneza la Mwili wa Joseph Senga likipewa heshima ya mwisho.
 Wanahabari waliofika kumuaga mwenzao.
 Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni ya The Guardiun, Suleiman Mpochi akitoa salamu za rambirambi.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati wakiwa kwenye shughuli ya kuaga Mwili wa Aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Marehemu Joseph Senga, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam leo.
 Mhariri Mtendaji wa Gazeti ya Tanzania Daima, Neville Meena akizungumza.
 Familia ya Marehemu Joseph Senga ikiwa ni yenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao.
 Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa salamu za Rambirambi.
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akizungumza.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza.


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa salamu.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.







 Baadhi ya Wapiga Picha wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini, wakibeba Jeneza la Marehemu Joseph Senga wakati wakilipeleka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Kwimba, Jijini Mwanza kwa Mazishi.