Thursday, November 10, 2016

MADAKTARI MABINGWA WA UPASUAJI TOKA NCHINI INDIA WAANZA HUDUMA BURE YA KUTIBU NA UPASUAJI WAGONJWA WA MOYO KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO JIJINI MWANZA

Mkuu wa Kitengo cha upasuaji wa Kifua na Moyo BMC, Prof. William Mahalu akizungumza (kulia) kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuwakaribisha madaktari bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai, India katika hafla iliyofanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza, pembeni yake ni Rais wa Jumuiya ya Shia Imami Islaili Muslims, Kanda ya Magharibi Bw. Altaf Hirani.
 Gharama za upasuaji wa Moyo ni kubwa si chini ya shilingi Millioni 6 za Tanzania. Kwa wagonjwa hawa tunashukuru Wizara ya Afya,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Medical Centre (BMC) lakini shukurani nyingi ziende MMI ambao wamenunua vifaa vingi ba ambavyo watatuachia hapa, ili tuendelee naupasuaji huu.
Sehemu ya madaktari wageni toka nchini India wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuwakaribisha madaktari hao mabingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai, India katika hafla iliyofanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza. Wa pili kutoka kushoto ni Bingwa wa Moyo kwa watoto daktari mzalendo aliyerejea nchini Dr. Glory Joseph ambaye ndiye aliyekuwa akisimamia zoezi hilo. 

Kwa mujibu wa Rais wa Jumuiya ya Shia Imami Islaili Muslims, Kanda ya Magharibi Bw. Altaf Hirani (katikati) amesema kuwa kila mwaka Hospitali ya Aga Khan inatumia shilingi za Kitanzania bilioni 2 kuwahudumia wagonjwa bila malipo yoyote ambapo hadi sasa zaidi ya wagonjwa 600 wamefanyiwa upasuaji wa moyo.

Watanzania madaktari 10 walipelekwa nchi za nje kupata mafunzo zaidi. Aidha Wakfu wa Afya wa Aga Khan umewekeza shilingi za kitanzania bilioni 167 katika ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya kutoa mafunzo ya udaktari ambayo tayari imeanza kujengwa. 

Pia kujengwa vituo 35 vya afya vitajengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, vitano vikiwa katika mkoa wa Mwanza.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Bingwa wa Moyo kwa watoto daktari mzalendo aliyerejea nchini Dr. Glory Joseph ambaye ndiye aliyekuwa akisimamia zoezi hilo. Nini sababu za watoto kuzaliwa na maradhi ya moyo na vipi kuhusu dalili, Hapa anafunguka zaidi. BOFYA KUSIKILIZA.


  

 Timu ya madaktari mabingwa wapatao 14 wako kwenye mpango huu wa kupima na kutibu kwa dawa na timu kamili ya kutibu kwa kupasua ikitegemea katika muda wa siku 6 yaani kuanzia tarehe 7 hadi 12 mwezi November kupasua waonjwa 10 wakiwemo wakubwa wanne (4) na watoto 6.


Wakati huo huo mabingwa hao wa maradhi ya moyo wataendelea kupima na kuchunguza watoto wenye magonjwa hayo ambapo mpaka sasa wameshapima watoto 50.

Sehemu ya akinamama ambao wamejitokeza kupima afya za watoto wao na hapa wakisubiri matibabu mara baada ya watoto wao kugundulika kuwa na matatizo kwenye afya ya moyo.

Ni moja ya akinamama ambao watoto wao wanasubiri kufanyiwa oparesheni katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

"Nasubiri kuiona siku mpya kwa mwanangu, siku itakayo kuwa mwanzo wa maisha yake yaliyo salama" 
BOFYA KUSIKILIZA NINI WALICHOSEMA AKINAMAMA HAWA
Mzazi huyo anakesha hapa kusubiri upasuaji.

Rais wa Jumuiya ya Shia Imami Islaili Muslims, Kanda ya Magharibi Bw. Altaf Hirani akimjulia hali mtoto David Rashid anayesumbuliwa na maradhi ya moyo akisubiri upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Ndani ya chumba cha Upasuaji Oparesheni inaendelea chini ya madaktari mabingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai nchini India na madaktari wakizalendo kutoka nchini Tanzania.

Ndani ya chumba cha Upasuaji na hapa Oparesheni inaendelea chini ya madaktari mabingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai nchini India na madaktari wakizalendo kutoka nchini Tanzania.

Ndani ya chumba cha Upasuaji Oparesheni madaktari wasaidizi.

Kwa umakini zaidi ndani ya chumba cha Upasuaji hapa Oparesheni inaendelea chini ya madaktari mabingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai nchini India na madaktari wakizalendo kutoka nchini Tanzania.

Mmoja ya wanahabari wetu Zephania Mandia kikazi zaidi.

G. Sengo ndani ya chumba cha Upasuaji, Oparesheni inaendelea chini ya madaktari mabingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Madras Medical Mission, Chennai nchini India na madaktari wakizalendo kutoka nchini Tanzania.

No comments: