Monday, October 10, 2016

DC KASESELA ASIFU KAZI ZA LASWA IRINGA ATAKA MATAPELI WA MIKOPO YA RIBA KUBWA KUFICHULIWA

Mkuu  wa   wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela  akifungua  warsha ya  LASWA  katika ukumbi wa chuo  kikuu huria cha Tanzania.
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw  Kasesela  Kushoto akipokelewa na mkurugenzi wa LASWA Francis Mwilafi
Mkuu  wa  wilaya na  viongozi  mbali mbali wa  LASWA na  Halmashauri
Dr Theoboro Kipilimba  mwenyekiti  wa  bodi ya Laswa  akitoa  neno la  shukurani kwa mgeni rasmi
Madiwani  wa Manispaa ya  Iringa wakiwa katika  picha ya  pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela  wa  tano  kulia pamoja na  viongozi wa Laswa  na wale  wa Halmashauri za Manispaa na  Iringa
Madiwani  wa Halmashauri ya   Iringa wakiwa katika  picha ya  pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela  wa  tano  kulia pamoja na  viongozi wa Laswa  na wale  wa Halmashauri za Manispaa na  Iringa
Madiwani  wa Halmashauri ya   Iringa wakiwa katika  picha ya  pamoja na mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela  wa  tano  kulia pamoja na  viongozi wa Laswa  na wale  wa Halmashauri za Manispaa na  Iringa
maofisa  Watendaji wa Halmashauri ya  Iringa  wakiwa katika  picha ya  pamoja na  mgeni  rasmi  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa
 Wafanyakazi wa Laswa  wakiwa katika  picha ya pamoja na mkuu wa  wilaya  ya  Iringa
DC  Kasesela  akiteta  jambo na naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa Bw Lyata


Na Matukiodaima BLOG
SERIKALI wilayani  Iringa imepongeza   jitihada  mbali  mbali  zinazofanywa na kituo  cha msaada  wa  kisheria  cha  LASWA mkoani  Iringa na  kutaka  kituo   hicho kuendelea  kupeleka vijijini  wasaidizi wa  kisheria  ili  kuwasaidia  wananchi  kujua  haki  zao na  kuagiza  wananchi  kuwafichua matapeli  wanaokopesha wananchi mikopo ya riba  kubwa .

Akizungumza  wakati wa  uzinduzi wa  warsha  ya ufunguzi wa  mradi wa  kuimarisha  huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa  ajili ya kuboresha  upatikanaji  wa haki kwa  wananchi wote hasa  kina mama  wajawazito iliyotolewa kwa madiwani wa wilaya nzima ya  Iringa na watendaji wa kata jana katika  ukumbi wa  chuo kikuu  huria cha  Tanzania , mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  alisema  kuwa  kumekuwepo na utapeli unaofanywa na baadhi ya  watu  kupitia mikopo  hiyo kwa  kuwatoza wananchi riba  kubwa jambo ambalo halitavumiliwa .
Kwani  alisema  kuwa  kumkopesha  mwananchi mkopo si  kosa  ila pale inapotokea mkopeshaji  kumtaka mwananchi  huyo  kulipa riba  mara  mbili ama tano  ya  mkopo aliokopa ni sawa na utapeli   hivyo  wananchi  wasisite  kuwafichua  wale  wote  wanaofanya  utapeli  wa aina   hiyo .


" Nawaagiza  wale  wote  wanaofanya utapeli  wa  kukopesha  wananchi mikopo ya  riba  kubwa  kuacha mara  moja  vinginevyo nitawashughulikia  kwa  kuwachukulia hatua  kali ......haiwezekani  wananchi  kuendelea  kuumizwa na mikopo  hiyo na baadhi yao  kupokonywa  nyumba  zao kwa  kushindwa  kulipa riba kubwa  wanazodaiwa "

Mkuu   huyo  wa   wilaya  alitaka LASWA  kupitia  wasaidizi  wake wa  kisheria  mijini na  vijijini  kuendelea  kuwasaidia  wananchi ambao  wananyanyasika kwa  kutojua  sheria  pamoja na  kutetea  wale  wote  wanaokandamizwa na matapeli  hao  wa mikopo hiyo ya  riba  kubwa .

Kuhusu watendaji   wa  serikalini na  baadhi ya mahakini wa mahakama  za mwanzo   zilizopo  vijijini  wanaotumika  kuwakandamiza  wananchi  wasiojua  sheria  mkuu  huyo alitaka kila  diwani kufikisha taarifa  ofisini  kwake  ili mahakimu hao na  watendaji wanaopindisha  sheria  kwa kujinufaisha  kuchukulia  hatua za  kinidhamu .

Alisema  kuna  baadhi ya mahakimu vijijini  wanatumika  kunyanyasa  wananchi kwa  kupindisha sheria  kusudi  ili  kujipatia   fedha .

"Kuna  hakimu  mmoja sitaki kumtaja  jina ila yupo  Halmashauri ya  Iringa  vijijini  kwa  kusudi anatumika   kutoa  hukumu kandamizi na  kwa  kushirikiana na mteja   wake anashinikiza aliyeshinda kesi  kufungua  kesi ya madai ili  fedha   hizo wagawane......huu ni unyanyasaji mkubwa  kwa  kumpokonya haki mwenye haki ili kumpa asiye na haki"

Hivyo  alisema mafunzo  hayo  kwa  madiwani na watendaji  hao  wa kata ni vema  yakatumika  kuwakomboa  wananchi kwa  kuwasaidia kujua  sheria na  kuwafichua wale wanaokiuka  sheria na  kuomba LASWA  kuweka  vijana  wao  waliopewa  mafunzo ya  kisheria kila ofisi ya  mkuu wa  wilaya ili  kusaidia mambo ya  kisheria badala ya kuwategemea  wanasheria  wa Halmashauri .


Mkurugenzi  wa LASWA  Francis Mwilafi  alisema  kuwa  mafunzo  hayo yameandaliwa na asasi  yake ya LASWA  kwa  ufadhili wa LSF ya  jijini Dar es  salaam kwa  chini  ya  ubalozi  wa Denmark   kuwa  sifa  ya  msaidizi  wa  kisheria ni  kuwa na akili timamu  pia  sifa ya kuheshimu na  kulinda  sheria za mbali  mbali  za nchi na haki za  binadamu

Mkurugenzi   huyo  alisema hadi  sasa  wamekwisha  toa mafunzo  na  kuwa na vijana katika  wilaya zote tatu  za  mkoa  wa Iringa  ikiwemo ya  Kilolo, Mufindi na Iringa kwa kuwa na vijana wasaidizi wa  kisheria

Aidha  alisema faida  kubwa ya  msaidizi wa  kisheria  ni kupunguza na kuziba pengo  la ukosefu wa huduma za msaada  wa kisheria katika jamii anayoishi  kwa  kutoa usaidizi wa  awali wa kisheria.

No comments: