Monday, September 26, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa awasimamisha kazi maafisa misitu wanne katika halmashauri ya wilaya ya Rufiji na kusitisha uvunaji wa misitu katika wilaya hiyo.https://youtu.be/wSga5mM2pXU

SIMU.TV: Rais Dr. John Pombe Magufuli atembelea bandari ya Dar es Salaam na kutoa miezi miwili kwa mamlaka ya bandari TPA kununua mashine 4 za kukakugulia migizo inayoingia na kutoka bandarini. https://youtu.be/yUbUQvPy1Mc

SIMU.TV: Wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu mkoani Kilimanjaro waiomba serikali kuimarisha ulinzi katika bwawa hilo ili kukomesha uvuvi haramu.https://youtu.be/5OhTpQMIi8E

SIMU.TV: Wakala wa ujenzi na majengo TBA umeanza kusafisha eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wakazi walioondolewa eneo hilo. https://youtu.be/_fNEF25AQqY

SIMU.TV: Shule ya msingi Mtendeni iliopo katika manispaa ya Ilala yamaliza tatizo la madawati leo baada ya kamati ya madawati ya mkoa kuisaidia madawati 40.https://youtu.be/KikNTTbuu3I

SIMU.TV: Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC chaiomba serikali kufanya marekebisho ya sheria ya mtoto na kutilia mkazo malezi bora ya mtoto kwa kuweka kipengele kinachotilia mkazo malezi ya watoto. https://youtu.be/fHQH-jtDqQo

SIMU.TV: Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba awataka wanachama wa chama hicho kumaliza migogoro ya chama kwa mazungumzo.https://youtu.be/A36HVWMGjMM

SIMU.TV: Licha ya serikali kuboresha vituo vingi vya daladala jijini Dar es Salaam bado changamoto ya barabara zinazofikia vituo hivyo haijatatuliwa.https://youtu.be/BWcPn6VozZw

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa auagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mafia kuimarisha doria eneo la bahari ili kuthibiti uvuvi haramu. https://youtu.be/Y86m-BFEWNE

SIMU.TV: Wauzaji wa vifaa maalumu vya kuhifadhia maji vinavyozalishwa na kampuni ya SIMTANK wakabidhiwa zawadi kama shukrani kutoka kwa kampuni hiyo.https://youtu.be/x9efLmSKsjs

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam awakumbusha wananchi umuhimu wa michezo kama chanzo cha msikamano na amani. https://youtu.be/StdiW9W6P70

SIMU.TV: Umoja wa wasanii wa kizazi kipya waandaa tamasha la hisani litakalo fanyika mkoani Kagera ili kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.https://youtu.be/RShBvI8Kpdg

SIMU.TV: Timu ya Mgambo JKT kutoka Tanga jana ilikubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Singida United katika uwanja wa Namfua mkoani Singida.https://youtu.be/npRwxH3DxL0

SIMU.TV: Bingwa wa masumbwi ya uzani mkubwa kutoka Uingereza Tyson Fury ameairisha pamabano lake la marudiano dhidi ya Vladimir Klitschko kwa sababu za kiafya.https://youtu.be/k52hMfAQz6U

No comments: