Wednesday, September 21, 2016

SERIKALI YAREJESHA ENEO LA HEKELI 50 KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIPARA MPAKANI MKOANI PWANI.

 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, baada ya kuwasili katika kijiji cha Kipara Mpakani kwa ajili ya kukabidhi eneo la hekali 50 kwa wanakijiji hicho, Mkuranga, Mkoani Pwani.
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akisaini kitabu cha wageni kabla ya mkutano na wanakijiji cha Kipara Mpakani. Kushoto ni Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega.
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akihutubia wanakijiji cha Kipara Mpakani kabla ya Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Maghembe kukabidhi eneo la hekali 50 kwa kijiji hicho kwa ajili ya huduma za kijamii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akihutubia wanakijiji cha Kipara Mpakani katika mkutano huo kabla ya makabidhiano.
  Mzee wa Kijiji cha Kipara Mpakani akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, kwaniaba ya wanakijiji hicho.
 Wanakijiji wakimpongeza Mbunge wao, Ulega baada kufanikiwa kupewa eneo hilo la hekali 50.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, wakikata majani kuashiria kukabidhi rasmi eneo hilo kwa ajili ya huduma za kijamii.


Na Mwandishi Wetu.
SERIKALI imerejesha eneo la hekeli 50 Kwa wananchi wa kijiji cha kipara mpakani kilichopo Kata ya Mwandege,Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ili wajenge huduma za kijamii.

Akikabidhi eneo hilo Waziri wa Maliasi na Utalii Profesa  Jumanne Maghembe aliwaeleza wananchi hao ambo walijitokeza Kwa wingi katika mkutano amesema kuwa wamponge Mbunge  wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwani amefanya jitihada kubwa za kuhakikisha Serikili inatoa Kwa wananchi eneo hilo.

Amesema kuwa wakati wako Bungeni mbunge huyo pamoja na baadhi viongozi wa kata  hiyo walikwenda Bungeni na kuiomba Serikali kuwapa eneo hilo ambapo lilikuwa pori tengefu la  maliasili ili wananchi wa kata ya Mwandege waweze kujenga Masoko.Shule,na miundombinu mingine.

"Nawapa eneo hili leo kwaniaba ya Serikali kwani najuwa Mh.rais Dkt.Magufuli wakati wakampeni alipita hapa nakuzungumzia eneo hili hivyo tunahitaji mjenge huduma mbalimbali na sio baadae watu wajitokeze na kusema eneo la kwenu."amesema Profesa Maghembe.

Naye Mbunge Ulega akizungumza katika mkutano huo amesema kuwa wananchi hao niwastaratibu kwani.mbali na kukosa maeneo ya kujenga huduma za jamii bado walikuwa wamekituza eneo hilo hadi leo Serikali wanapoamua kuwapa wananchi.

No comments: