Saturday, September 17, 2016

DAVID KAFULILA AONGOZA MAAFALI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA GOSHEN NURSERY AND PRIMARY SCHOOL BUNJU JIJINI DAR


 Mwanafunzi Eugene Kephasi, akimvika skafu, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alikuwa  mgeni rasmi katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School  Bunju jijini Dar es Salaam leo mchana.
 David Kafulila akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu wakati akipewa historia fupi ya shule hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu (hayupo pichani).
 Kafulila (katikati) na viongozi wa shule hiyo wakielekea meza kuu tayari kwa maafali hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu, Mkurugenzi wa Shule, Nipael Mrutu, Lupi Kiyabo na Mchungaji Elisifa Kephasi.
 Wanafunzi wakiwa tayari kwa gwaride.
 Wanafunzi wa darasa la saba wakiwa kwenye maafali yao.
 Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu (kushoto), akimuongoza mgeni rasmi David Kafulila wakati wa kukagua shule hiyo.
 Skauti akionesha namna ya kupika katika kambi yao waliyoiweka katika shule hiyo kunogesha maafali hayo.
 Magari yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi yakiwa shuleni hapo
 walimu wakiwa kwenye maafali hayo.
 Wahitimu wa darasa la saba wakiimba wimbo wa shule.
 Wanafunzi wa darasa la tatu wakiimba kwenye maafali hayo.
 Wanafunzi wakiimba wimbo wa kuwaaga darasa la saba.
 Majadiliano meza kuu na mgeni rasmi. Kulia ni Mchungaji Elisifa Kephasi na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu.
 wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani.
 Hapa ni furaha tupu kwa wanafunzi wa darasa la pili baada ya kutoa burudani.



 Sarakasi zikifanyika katika maafali hayo.
 Wageni waalikwa, wazazi na walezi wa watoto hao wakijumuika na watoto wao kwenye maafali hayo.
 Sarakasi zikiendelea.
 Hapa ni Karate kwa kwenda mbele "madogo wapo vizuri sana katika mchezo huo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa Kamanda Mduma wa Skauti"
Skauti wakionesha namna ya kumuokoa mtu aliyepoteza fahamu ambaye yupo kwenye eneo la kikwazo kumfikia. Hapa muokoaji akipita chini ya moto kwenda kumchukua mgonjwa.

Na Dotto Mwaibale


MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amesema urithi pekee wa watoto ni elimu na sio mali kama ilivyozoeleka.


Kafuli ametoa kauli hiyo katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Dar es Salaam leo mchana.

"Napenda kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwapa elimu watoto wenu kwani ndio msingi wa maisha yao badala ya kuwarithisha magari, nyumba na vitu vingine vya thamani" alisema Kafulila.
Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hayo alitoa shukurani zake kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi hao ambao watakuja kuwa wataalamu na viongozi wa baadae.
Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali bila ya kujali dini wala uraia na inazingatia maadili jambo linalowavutia watu wengi kuwapeleka watoto wao wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.
Katika maafali hayo wanafunzi wa shule hiyo walionesha burudani mbalimbali kama kuimba, gwaride, sarakasi, karate na michezo mingine ya ukakamavu waliyofundishwa na vijana kutoka chama cha Skauti Tanzania.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments: