Friday, August 26, 2016

Watanzania washauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili kuutangaza Utamaduni

Watanzania wameshauriwa kutumia Lugha ya Kiswahili katika ulimwengu wa uandishi ili kuutangaza Utamaduni wa nchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI).

Mkurugenzi amesema kuwa kwa kutumia Lugha ya Kiswahili kutasaidia kuendeleza na kuenzi juhudi za kuenzi na kuendeleza juhudi za watetezi za masuala ya lugha wa masuala ya Lugha na Utamaduni wa mtanzania.

Ameongeza kuwa Serikali kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa imeandaa kanuni za Sheria ya BAKITA ya mwaka 1967 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi karibuni ambayo itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili waandishi hapa nchini pamoja na haki zao katika kuendeleza fani mbalimbali za Lugha.

“Katika azma ya kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili tuige mfano wa Rais wetu Mhe.Dkt John Pombe Magufuli wa kutumia Lugha ya kiswahili katika hotuba zake mbalimbali za kitaifa na kimataifa” alisema Bibi. Hajjat Shani.

Kwa upande wake mmoja ya wajumbe wa kamati kuu Bi. Matilda Sendwa katika risala yao kwa mgeni rasmi amesema kuwa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania(UWARIDI) wameamua kutafuta njia ya kurudisha, kutetea, kulinda na kuipandisha heshima yetu kama waandishi na heshima ya kazi zetu zote.

“Tumeamua kutafuta mbinu za kuweza kuhakikisha kuwa heshima ya kazi zetu zinatambuliwa rasmi kiserikali na kijamii kwa ujumla kwa kuanzisha umoja wetu ambao utakuwa na sauti katika kutetea haki za waandishi na kazi zao alisisitiza Bi. Matilda.

Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) umeanzishwa kwa lengo la kuwatetea waandishi wa Riwaya nchini ili waweze kunufaika na kazi zao.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Rais wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Bw. Hussein Tuwa akitoa neno wakati wa uzinduzi wa Umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) Ibrahim Gama akitoa maelezo kwa mgeni rasmi kuhusu Umoja wao wakati wa uzinduzi wa Umoja wa huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo akionesha cheti cha usajili wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya kuuzindua umoja huo huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) wakimsikiliza mwakilishi wa mgeni rasmi Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(hayupo pichani) katika uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.
Mkurugezi Msaidizi Lugha Bibi Hajjat Shani Kitogo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamojja na viongozi na wajumbe wa kamati kuu ya Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI) mara baada ya uzinduzi wa umoja huo katika ukumbi wa Nafasi Arts Space Jijini Dar es Salaam Agosti 25,2016.

Baadhi ya vitabu vya Riwaya vilivyoandikwa na wanachama wa Umoja wa Waandishi wa Riwaya wenye Dira Tanzania (UWARIDI). (Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)

No comments: